Matendo 11:12
Roho aliniambia niende pamoja nao bila kusita. Hawa ndugu sita waliandamana nami pia kwenda Kaisarea na huko tuliingia nyumbani mwa Kornelio.
Biblia Takatifu
In The King James Version
In Context
Cross References
John 16:13Lakini atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza kwenye ukweli wote; maana hatasema kwa mamlaka yake mwenyewe, bali atawaambieni yote atakayosikia, na atasema mambo yatakayokuwa yanakuja.
Acts 10:19Petro alikuwa bado anajaribu kuelewa lile maono, na hapo Roho akamwambia, “Sikiliza! kuna watu watatu hapa, wanakutafuta.
Acts 10:45Wale Wayahudi waumini waliokuja pamoja na Petro kutoka Yopa walishangaa kuona kuwa Mungu aliwamiminia zawadi ya Roho Mtakatifu watu wa mataifa mengine pia;
Acts 13:4Basi, Barnaba na Saulo walipokwisha tumwa na Roho Mtakatifu, walishuka hadi Seleukia, na kutoka huko walipanda meli hadi kisiwa cha Kupro.
Acts 15:9Hakufanya ubaguzi wowote kati yetu na wao; aliitakasa mioyo yao kwa imani.
Romans 3:22Mungu huwakubali watu kuwa waadilifu kwa njia ya imani yao kwa Yesu Kristo; Mungu hufanya hivyo kwa wote wanaoamini; hakuna ubaguzi wowote.