Yohana 8:31
Basi, Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Kama mkiyazingatia mafundisho yangu mtakuwa kweli wanafunzi wangu.
Biblia Takatifu
In The King James Version
In Context
30Baada ya kusema hayo watu wengi walimwamini.
32Mtaujua ukweli, nao ukweli utawapeni uhuru.”
Cross References
Matthew 24:13Lakini atakayevumilia mpaka mwisho, ataokoka.
John 6:55Maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.
John 8:36Kama mwana akiwapeni uhuru mtakuwa huru kweli.
Acts 13:43Mkutano huo ulipomalizika, Wayahudi wengi na watu wa mataifa mengine waliokuwa wameongokea dini ya Kiyahudi waliwafuata Paulo na Barnaba. Hao mitume waliongea nao, wakawatia moyo waendelee kuishi wakitegemea neema ya Mungu.
Acts 26:22Lakini Mungu alinisaidia; na hivyo mpaka siku ya leo nimesimama imara nikitoa ushuhuda kwa wote, wakubwa na wadogo. Ninayosema ni yale ambayo manabii na Mose walisema yatatukia;
Romans 11:22Kumbuka, basi, jinsi Mungu alivyo mwema na mkali. Yeye ni mkali kwa wale walioanguka, na ni mwema kwako wewe ikiwa utaendelea katika wema wake; la sivyo, nawe pia utakatwa.