2 Samuel · Biblia (Kiswahili)

2 Samuel 22

1Daudi alimwimbia Bwana maneno ya wimbo huu wakati Bwana alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na pia mkononi mwa Sauli.

2Akasema: 1 “ Bwana ni mwamba wangu, 2 ngome yangu na mwokozi wangu, 1

3Mungu wangu ni mwamba wangu, 2 ambaye kwake ninakimbilia, 2 ngao yangu na pembe ya wokovu wangu. 1 Yeye ni ngome yangu, kimbilio langu 2 na mwokozi wangu, 2 huniokoa kutoka kwa watu wenye jeuri. 1

4Ninamwita Bwana, anayestahili kusifiwa, 2 nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu. 1

5“Mawimbi ya mauti yalinizunguka, 2 mafuriko ya maangamizi yalinilemea. 1

6Kamba za kuzimu + 22:6 Kuzimu kwa Kiebrania ni Sheol, maana yake ni Shimo lisilo na mwisho. zilinizunguka, 2 mitego ya mauti ilinikabili. 1

7Katika shida yangu nalimwita Bwana, 2 nilimlilia Mungu wangu. 1 Kutoka Hekaluni mwake alisikia sauti yangu, 2 kilio changu kikafika masikioni mwake. 1

8“Dunia ilitetemeka na kutikisika, 2 misingi ya mbingu ikatikisika, 1 vilitetemeka kwa sababu 2 alikuwa amekasirika. 1

9Moshi ukapanda kutoka puani mwake, 2 moto uteketezao ukatoka kinywani mwake, 1 makaa ya moto yawakayo 2 yakatoka ndani mwake. 1

10Akazipasua mbingu akashuka chini, 2 mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake. 1

11Alipanda juu ya kerubi akaruka, 2 akapaa juu kwa mbawa za upepo. 1

12Alifanya giza hema lake la kujifunika: 2 mawingu meusi ya mvua ya angani. 1

13Kutokana na mwanga wa uwepo wake 2 mawingu yalisogea, 1 ikanyesha mvua ya mawe 2 na umeme wa radi. 1

14Bwana alinguruma kutoka mbinguni, 2 sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika. 1

15Aliipiga mishale na kutawanya adui, 2 umeme wa radi na kuwafukuza. 1

16Mabonde ya bahari yalifunuliwa, 2 na misingi ya dunia ikawa wazi 1 kwa kukaripia kwake Bwana, 2 kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwake. 1

17“Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika; 2 alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu. 1

18Aliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi, 2 kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi. 1

19Walinikabili siku ya msiba wangu, 2 lakini Bwana alikuwa msaada wangu. 1

20Alinileta nje mahali penye nafasi tele, 2 akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami. 1

21“ Bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu; 2 sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa. 1

22Kwa maana nimezishika njia za Bwana; 2 sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu. 1

23Sheria zake zote zi mbele yangu, 2 wala sijayaacha maagizo yake. 1

24Nimekuwa sina hatia mbele zake, 2 nami nimejilinda nisitende dhambi. 1

25Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu, 2 sawasawa na usafi wangu machoni pake. 1

26“Kwa yeye aliye mwaminifu unajionyesha kuwa mwaminifu, 2 kwa asiye na hatia unajionyesha kutokuwa na hatia, 1

27kwa aliye mtakatifu unajionyesha kuwa mtakatifu, 2 lakini kwa aliyepotoka unajionyesha kuwa mkaidi. 1

28Wewe huwaokoa wanyenyekevu, 2 lakini macho yako ni juu ya wenye kiburi 2 ili uwashushe. 1

29Wewe ni taa yangu, Ee Bwana. 2 Bwana hulifanya giza langu 2 kuwa mwanga. 1

30Kwa msaada wako naweza kushinda jeshi, 2 nikiwa pamoja na Mungu wangu 2 nitaweza kuruka ukuta. 1

31“Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu; 2 neno la Bwana halina dosari. 1 Yeye ni ngao kwa wote 2 wanaokimbilia kwake. 1

32Kwa maana ni nani aliye Mungu 2 zaidi ya Bwana? 1 Ni nani aliye Mwamba 2 isipokuwa Mungu wetu? 1

33Mungu ndiye anivikaye nguvu 2 na kufanya njia yangu kuwa kamilifu. 1

34Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, 2 huniwezesha kusimama mahali palipo juu. 1

35Huifundisha mikono yangu kupigana vita; 2 mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba. 1

36Hunipa ngao yako ya ushindi, 2 unajishusha chini ili kuniinua. 1

37Huyapanua mapito yangu, 2 ili miguu yangu isiteleze. 1

38“Niliwafuatia adui zangu na nikawaseta, 2 sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa. 1

39Niliwaseta kabisa, nao hawakuweza kuinuka tena; 2 walianguka chini ya miguu yangu. 1

40Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita; 2 uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu. 1

41Uliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia, 2 nami nikawaangamiza adui zangu. 1

42Walipiga yowe, lakini hapakuwepo na yeyote wa kuwaokoa; 2 walimlilia Bwana, lakini hakuwajibu. 1

43Niliwaponda kama mavumbi ya nchi; 2 niliwaponda na kuwakanyaga kama tope barabarani. 1

44“Umeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu wangu; 2 umenihifadhi mimi kama kiongozi wa mataifa. 1 Watu ambao sikuwajua wananitumikia, 2

45nao wageni huja wakininyenyekea, 2 mara wanisikiapo, hunitii. 1

46Wote wanalegea, 2 wanatoka katika ngome zao wakitetemeka. 1

47“ Bwana yu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu! 2 Atukuzwe Mungu, 2 Mwamba, Mwokozi wangu! 1

48Yeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi, 2 ayawekaye mataifa chini yangu, 2

49aniwekaye huru toka kwa adui zangu. 1 Uliniinua juu ya adui zangu; 2 uliniokoa toka kwa watu wajeuri. 1

50Kwa hiyo nitakusifu, Ee Bwana, 2 katikati ya mataifa; 2 nitaliimbia sifa jina lako. 1

51Humpa mfalme wake ushindi mkuu; 2 huonyesha fadhili zake kwa mpakwa mafuta wake, 2 kwa Daudi na wazao wake milele.”

← 2 Samuel 21Read In The App, Free →2 Samuel 23 →

Study 2 Samuel 22

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324