Deuteronomy 33
1Hii ndiyo baraka Mose mtu wa Mungu aliyotamka kwa Waisraeli kabla ya kifo chake.
2Alisema: 1 “ Bwana alikuja kutoka Mlima Sinai, 2 akachomoza kama jua juu yao 2 kutoka Mlima Seiri, 2 akaangaza kutoka Mlima Parani. 1 Alikuja pamoja na watakatifu makumi elfu 2 kutoka kusini, 2 kutoka materemko ya mlima wake. 1
3Hakika ni wewe ambaye huwapenda watu, 2 watakatifu wako wote wamo mkononi mwako. 1 Miguuni pako wote wanasujudu 2 na kutoka kwako wanapokea mafundisho, 1
4sheria ile Mose aliyotupa sisi, 2 tulio milki ya kusanyiko la Yakobo. 1
5Alikuwa mfalme juu ya Yeshuruni + 33:5 Yeshuruni maana yake ni Yeye aliye mnyofu, yaani Israeli. 2 wakati viongozi wa watu walipokusanyika, 2 pamoja na makabila ya Israeli. 1
6“Reubeni na aishi, asife, 2 wala watu wake wasiwe wachache.”
7Akasema hili kuhusu Yuda: 1 “Ee Bwana, sikia kilio cha Yuda, 2 mlete kwa watu wake. 1 Kwa mikono yake mwenyewe hujitetea. 2 Naam, uwe msaada wake 2 dhidi ya adui zake!”
8Kuhusu Lawi alisema: 1 “Thumimu yako na Urimu + 33:8 Thumimu na Urimu maana yake Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha kifuani cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha. yako ulimpa, 2 mtu yule uliyemfadhili. 1 Ulimjaribu huko Masa 2 na kushindana naye 2 kwenye maji ya Meriba. 1
9Alinena hivi kuhusu baba yake na mama yake, 2 ‘Mimi siwahitaji kamwe.’ 1 Akawasahau jamaa zake, 2 asiwatambue hata watoto wake, 1 lakini akaliangalia neno lako 2 na kulilinda Agano lako. 1
10Humfundisha Yakobo mausia yako 2 na Israeli sheria yako. 1 Hufukiza uvumba mbele zako 2 na sadaka nzima za kuteketezwa 2 juu ya madhabahu yako. 1
11Ee Bwana, bariki ustadi wake wote, 2 nawe upendezwe na kazi ya mikono yake. 1 Vipige viuno vya wale wainukao dhidi yake; 2 wapige adui zake hata wasiinuke tena.”
12Kuhusu Benyamini akasema: 1 “Mwache mpenzi wa Bwana 2 apumzike salama kwake, 1 kwa maana humkinga mchana kutwa, 2 na yule Bwana ampendaye 2 hupumzika kati ya mabega yake.”
13Kuhusu Yosefu akasema: 1 “ Bwana na aibariki nchi yake 2 kwa umande wa thamani 2 kutoka mbinguni juu, 1 na vilindi vya maji 2 vilivyotulia chini; 1
14pamoja na vitu vilivyo bora sana 2 viletwavyo na jua, 1 na vitu vizuri sana vinavyoweza 2 kutolewa na mwezi; 1
15pamoja na zawadi bora sana 2 za milima ya zamani 1 na kwa wingi wa baraka 2 za vilima vya milele; 1
16pamoja na baraka nzuri mno 2 za ardhi na ukamilifu wake, 1 na upendeleo wake yeye 2 aliyeishi kwenye kichaka 2 kilichokuwa kinawaka moto. 1 Hivi vyote na vikae juu ya kichwa cha Yosefu, 2 juu ya paji la uso la aliye mkuu 2 miongoni mwa ndugu zake. 1
17Katika fahari yeye ni kama fahali mzaliwa wa kwanza; 2 pembe zake ni pembe za nyati, 1 na kwa pembe hizo atapiga mataifa, 2 hata yaliyo miisho ya dunia. 1 Hivyo ndivyo yalivyo makumi elfu ya Efraimu; 2 hivyo ndivyo yalivyo maelfu ya Manase.”
18Kuhusu Zabuloni akasema: 1 “Shangilia, Zabuloni, wakati wa kutoka nje, 2 nawe Isakari, katika mahema yako. 1
19Watawaita mataifa kwenye mlima, 2 na huko mtatoa dhabihu za haki; 1 watajifurahisha kwa wingi uliojaza bahari, 2 kwa hazina zilizofichwa mchangani.”
20Kuhusu Gadi akasema: 1 “Atabarikiwa yeye aongezaye milki ya Gadi! 2 Gadi huishi huko kama simba, 2 akirarua kwenye mkono au kichwa. 1
21Alijichagulia nchi nzuri kuliko zote 2 kwa ajili yake mwenyewe; 1 fungu la kiongozi lilikuwa limehifadhiwa 2 kwa ajili yake. 1 Viongozi wa watu walipokusanyika, 2 alitimiza haki ya mapenzi ya Bwana, 2 na hukumu zake kuhusu Israeli.”
22Kuhusu Dani akasema: 1 “Dani ni mwana simba, 2 akiruka kutoka Bashani.”
23Kuhusu Naftali akasema: 1 “Naftali amejaa tele upendeleo wa Bwana, 2 naye amejaa baraka yake; 2 atarithi magharibi na kusini.”
24Kuhusu Asheri akasema: 1 “Aliyebarikiwa zaidi sana katika wana ni Asheri; 2 yeye na apate upendeleo kwa ndugu zake, 2 yeye na anawe miguu yake kwenye mafuta. 1
25Makomeo ya malango yako yawe chuma na shaba, 2 nazo nguvu zako zitakuwa sawa na siku zako. 1
26“Hakuna mwingine kama Mungu wa Yeshuruni, 2 ambaye hupanda juu ya mbingu ili akusaidie, 2 na juu ya mawingu katika utukufu wake. 1
27Mungu wa milele ni kimbilio lako, 2 na chini kuna mikono ya milele. 1 Atamfukuza adui yako mbele yako, 2 akisema, ‘Mwangamize yeye!’ 1
28Hivyo Israeli ataishi salama peke yake. 2 Mzao wa Yakobo ni salama 1 katika nchi ya nafaka na divai mpya, 2 mahali ambapo mbingu 2 hudondosha umande. 1
29Ee Israeli, wewe umebarikiwa! 2 Ni nani kama wewe, 2 taifa lililookolewa na Bwana? 1 Yeye ni ngao yako na msaada wako, 2 na upanga wako uliotukuka. 1 Adui zako watatetemeka mbele yako, 2 nawe utapakanyaga 2 mahali pao pa juu.” + 33:29 Utapakanyaga mahali pao pa juu maana yake mtakanyaga juu ya miili yao.