Ezekiel · Biblia (Kiswahili)

Ezekiel 19

1“Wewe fanya maombolezo kuhusu wakuu wa Israeli

2na useme: 1 “ ‘Tazama jinsi gani mama yako alivyokuwa simba jike 2 miongoni mwa simba! 1 Alilala katikati ya wana simba 2 na kulisha watoto wake. 1

3Alimlea mmoja wa watoto wake, 2 naye akawa simba mwenye nguvu. 1 Akajifunza kurarua mawindo 2 naye akala watu. 1

4Mataifa wakasikia habari zake, 2 naye akanaswa katika shimo lao. 1 Wakamwongoza kwa ndoana 2 mpaka nchi ya Misri. 1

5“ ‘Mama yake alipongoja na kuona tumaini lake halitimiziki, 2 nayo matarajio yake yametoweka, 1 akamchukua mwanawe mwingine 2 na kumfanya simba mwenye nguvu. 1

6Alizungukazunguka miongoni mwa simba, 2 kwa kuwa sasa alikuwa simba mwenye nguvu. 1 Akajifunza kurarua mawindo 2 naye akala watu. 1

7Akabomoa ngome zao 2 na kuiharibu miji yao. 1 Nchi na wote waliokuwa ndani yake 2 wakatiwa hofu kwa kunguruma kwake. 1

8Kisha mataifa wakaja dhidi yake 2 kutoka sehemu zilizomzunguka. 1 Wakatanda nyavu zao kwa ajili yake, 2 naye akanaswa katika shimo lao. 1

9Kwa kutumia ndoana wakamvutia kwenye tundu 2 na kumleta mpaka kwa mfalme wa Babeli. 1 Wakamtia gerezani, hivyo kunguruma kwake 2 hakukusikika tena 2 katika milima ya Israeli. 1

10“ ‘Mama yako alikuwa kama mzabibu 2 katika shamba lako la mizabibu 2 uliopandwa kando ya maji, 1 ukiwa unazaa sana na wenye matawi mengi 2 kwa sababu ya wingi wa maji. 1

11Matawi yake yalikuwa na nguvu, 2 yaliyofaa kuwa fimbo ya enzi ya mtawala. 1 Ulikuwa mrefu kupita miti mingine 2 katikati ya matawi manene; 1 ulionekana kwa urahisi 2 kwa ajili ya urefu wake 2 na wingi wa matawi yake. 1

12Lakini ulingʼolewa kwa hasira kali 2 na kutupwa chini. 1 Upepo wa mashariki uliufanya usinyae, 2 matunda yake yakapukutika, 1 matawi yake yenye nguvu yakanyauka 2 na moto ukayateketeza. 1

13Sasa umepandwa jangwani 2 katika nchi kame na ya kiu. 1

14Moto ulienea kuanzia katika mmojawapo ya matawi yake makubwa 2 na kuteketeza matunda yake. 1 Hakuna tawi lenye nguvu lililobaki juu yake 2 lifaalo kuwa fimbo ya enzi ya mtawala.’ Hili ndilo ombolezo, na litumike kama ombolezo.”

← Ezekiel 18Read In The App, Free →Ezekiel 20 →

Study Ezekiel 19

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748