Ezra 2
1Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,
2wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana): 4 Orodha ya wanaume kati ya watu wa Israeli ilikuwa: 1
3wazao wa Paroshi 2 2,172 1
4wazao wa Shefatia 2 372 1
5wazao wa Ara 2 775 1
6wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2 2,812 1
7wazao wa Elamu 2 1,254 1
8wazao wa Zatu 2 945 1
9wazao wa Zakai 2 760 1
10wazao wa Bani 2 642 1
11wazao wa Bebai 2 623 1
12wazao wa Azgadi 2 1,222 1
13wazao wa Adonikamu 2 666 1
14wazao wa Bigwai 2 2,056 1
15wazao wa Adini 2 454 1
16wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) 2 98 1
17wazao wa Besai 2 323 1
18wazao wa Yora 2 112 1
19wazao wa Hashumu 2 223 1
20wazao wa Gibari 2 95 1
21watu wa Bethlehemu 2 123 1
22watu wa Netofa 2 56 1
23watu wa Anathothi 2 128 1
24watu wa Azmawethi 2 42 1
25wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 2 743 1
26wazao wa Rama na Geba 2 621 1
27watu wa Mikmashi 2 122 1
28watu wa Betheli na Ai 2 223 1
29wazao wa Nebo 2 52 1
30wazao wa Magbishi 2 156 1
31wazao wa Elamu ile ingine 2 1,254 1
32wazao wa Harimu 2 320 1
33wazao wa Lodi, Hadidi na Ono 2 725 1
34wazao wa Yeriko 2 345 1
35wazao wa Senaa 2 3,630 4
36Makuhani: 1 wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) 2 973 1
37wazao wa Imeri 2 1,052 1
38wazao wa Pashuri 2 1,247 1
39wazao wa Harimu 2 1,017 4
40Walawi: 1 wazao wa Yeshua na Kadmieli (kupitia jamaa ya Hodavia) 2 74 4
41Waimbaji: 1 wazao wa Asafu 2 128 4
42Mabawabu wa lango la Hekalu: 1 wazao wa // Shalumu, Ateri, Talmoni, // Akubu, Hatita na Shobai 2 139 4
43Watumishi wa Hekalu: + 2:43 Yaani Wanethini (pia 2:58, 70 ). 1 wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi, 1
44wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni, 1
45wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu, 1
46wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani, 1
47wazao wa Gideli, Gahari, Reaya, 1
48wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu, 1
49wazao wa Uza, Pasea, Besai, 1
50wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu, 1
51wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri, 1
52wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha, 1
53wazao wa Barkosi, Sisera, Tema, 1
54wazao wa Nesia na Hatifa. 4
55Wazao wa watumishi wa Solomoni: 1 wazao wa Sotai, Hasaferethi, Peruda, 1
56wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli, 1
57wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami. 1
58Watumishi wa Hekalu wote na // wazao wa watumishi // wa Solomoni 2 392 4
59Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli: 1
60wazao wa // Delaya, Tobia na Nekoda 2 652 4
61Kutoka miongoni mwa makuhani: 1 Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo). 4
62Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi.
63Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu. + 2:63 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha kifuani cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha. 4
64Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360;
65tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200.
66Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245,
67ngamia 435 na punda 6,720.
68Walipofika kwenye nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake.
69Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,000 + 2:69 Darkoni 61,000 za dhahabu ni sawa na kilo 500. za dhahabu, mane 5,000 + 2:69 Mane 5,000 za fedha ni sawa na kilo 2,900. za fedha, na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo.
70Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.