Wagalatia 6:13
Maana, hao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki Sheria; huwataka ninyi mtahiriwe wapate kujivunia alama hiyo mwilini mwenu.
Biblia Takatifu
In The King James Version
In Context
Cross References
Matthew 23:3Kwa hiyo shikeni na kutekeleza chochote watakachowaambieni. Lakini msiyaige matendo yao, maana hawatekelezi yale wanayoyahubiri.
Matthew 23:23Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnatoza watu zaka, hata juu ya majani yenye harufu nzuri, bizari na jira, na huku mnaacha mambo muhimu ya Sheria kama vile haki, huruma na imani. Haya ndiyo hasa mliyopaswa kuyazingatia bila kusahau yale mengine.
Romans 2:17Na wewe, je? Wewe mwenyewe unajiita Myahudi; unaitumainia Sheria na kujivunia kuwa wa Mungu;
1 Corinthians 3:21Basi, mtu asijivunie watu. Maana kila kitu ni chenu.
2 Corinthians 11:18Maadam wengi hujivuna kwa sababu za kidunia, nami pia nitajivuna.
2 Peter 2:19Huwaahidi watu wengine eti watakuwa huru, kumbe wao wenyewe ni watumwa wa upotovu—maana mtu ni mtumwa wa chochote kile kinachomtawala.