Jonah · Biblia (Kiswahili)

Jonah 2

1Akiwa ndani ya tumbo la nyangumi, Yona alimwomba Bwana Mungu wake.

2Akasema: 1 “Katika shida yangu nalimwita Bwana, 2 naye akanijibu. 1 Kutoka kina cha kaburi + 2:2 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. niliomba msaada, 2 nawe ukasikiliza kilio changu. 1

3Ulinitupa kwenye kilindi, 2 ndani kabisa ya moyo wa bahari, 2 mikondo ya maji ilinizunguka, 1 mawimbi yako yote na viwimbi 2 vilipita juu yangu. 1

4Nikasema, ‘Nimefukuziwa 2 mbali na uso wako, 1 hata hivyo nitatazama tena 2 kuelekea Hekalu lako takatifu.’ 1

5Maji yaliyonimeza yalinitisha, 2 kilindi kilinizunguka; 2 mwani + 2:5 Mwani hapa maana yake ni magugu yaotayo kwenye sakafu ya kilindi cha bahari. ulijisokota kichwani pangu. 1

6Nilizama chini sana mpaka pande za mwisho za milima, 2 makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele. 1 Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni, 2 Ee Bwana Mungu wangu. 1

7“Wakati uhai wangu ulipokuwa unatoka, 2 nilikukumbuka wewe, Bwana, 1 nayo maombi yangu yalikufikia wewe, 2 katika Hekalu lako takatifu. 1

8“Wale watu wanaongʼangʼana na sanamu zisizofaa 2 hupoteza neema ile ambayo ingekuwa yao. 1

9Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani, 2 nitakutolea dhabihu. 1 Lile nililowekea nadhiri nitalitimiza. 2 Wokovu watoka kwa Bwana.”

10Basi Bwana akamwamuru yule nyangumi, naye akamtapika Yona katika nchi kavu.

← Jonah 1Read In The App, Free →Jonah 3 →

Study Jonah 2

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

1234