Judges · Biblia (Kiswahili)

Judges 5

1Ndipo Debora na Baraka mwana wa Abinoamu wakaimba wimbo huu: 1

2“Wakuu katika Israeli wanapoongoza, 2 wakati watu wanapojitoa 2 kwa hiari yao wenyewe: 2 mhimidini Bwana! 1

3“Sikieni hili, enyi wafalme! 2 Sikilizeni, enyi watawala! 1 Nitamwimbia Bwana, nitaimba; 2 kwa wimbo nitamhimidi Bwana, 2 Mungu wa Israeli. 1

4“Ee Bwana, ulipotoka katika Seiri, 2 ulipopita katika mashamba ya Edomu, 1 nchi ilitetemeka, mbingu nazo zikamwaga, 2 naam, mawingu yakamwaga maji. 1

5Milima ilitetemeka mbele za Bwana, 2 hata ule wa Sinai, 2 mbele za Bwana, 2 Mungu wa Israeli. 1

6“Katika siku za Shamgari mwana wa Anathi, 2 katika siku za Yaeli, 1 barabara kuu hazikuwa na watu; 2 wasafiri walipita njia za kando. 1

7Mashujaa walikoma katika Israeli, 2 walikoma mpaka mimi, Debora, nilipoinuka, 2 nilipoinuka kama mama katika Israeli. 1

8Walipochagua miungu migeni, 2 vita vilikuja katika malango ya mji, 1 hapakuonekana ngao wala mkuki 2 miongoni mwa mashujaa 40,000 katika Israeli. 1

9Moyo wangu u pamoja na wakuu wa Israeli, 2 pamoja na wale wanaojitoa wenyewe 2 kwa hiari yao miongoni mwa watu. 2 Mhimidini Bwana! 1

10“Nanyi mpandao punda weupe, 2 mkiketi juu ya matandiko ya thamani, 2 nanyi mtembeao barabarani, 1 fikirini

11juu ya sauti za waimbaji 2 mahali pa kunyweshea maji. 1 Wanasimulia matendo ya haki ya Bwana, 2 matendo ya haki ya mashujaa wake 2 katika Israeli. 1 “Ndipo watu wa Bwana 2 walipoteremka malangoni pa mji. 1

12‘Amka, amka! Debora! 2 Amka, amka, uimbe! 1 Ee Baraka! Inuka, 2 chukua mateka wako uliowateka, 2 ee mwana wa Abinoamu.’ 1

13“Ndipo mabaki ya watu 2 wakashuka dhidi ya wenye nguvu, 1 watu wa Bwana, 2 wakashuka dhidi ya mashujaa wenye nguvu. 1

14Kutoka Efraimu wakaja watu, ambao chimbuko lao ni Amaleki; 2 Benyamini akiwa miongoni 2 mwa watu waliokufuata. 1 Kutoka Makiri wakashuka viongozi, 2 na kutoka Zabuloni wale washikao 2 fimbo ya jemadari. 1

15Wakuu wa Isakari walikuwa pamoja na Debora; 2 naam, Isakari alikuwa pamoja na Baraka, 1 wakija nyuma yake kwa mbio 2 wakielekea bondeni. 1 Katika jamaa za Reubeni, 2 palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni. 1

16Kwa nini ulikaa katikati ya mazizi ya kondoo 2 kusikiliza sauti ya filimbi zinazoita makundi? 1 Kwa jamaa za Reubeni, 2 palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni. 1

17Gileadi alikaa ngʼambo ya Yordani. 2 Naye Dani, kwa nini alikaa 2 kwenye merikebu siku nyingi? 1 Asheri alikaa kwa utulivu ufuoni mwa bahari, 2 akikaa kwenye ghuba zake ndogo. 1

18Watu wa Zabuloni walihatarisha maisha yao, 2 vilevile nao watu wa Naftali. 1

19“Wafalme walikuja na kufanya vita; 2 wafalme wa Kanaani walipigana 2 huko Taanaki karibu na maji ya Megido, 2 lakini hawakuchukua fedha wala nyara. 1

20Kutoka mbinguni nyota zilipigana, 2 nyota kutoka njia zake 2 zilipigana na Sisera. 1

21Mto wa Kishoni uliwasomba, 2 ule mto wa zamani, mto wa Kishoni. 1 Songa mbele, ee nafsi yangu, 2 kwa ujasiri! 1

22Ndipo kwato za farasi zikafanya mshindo: 2 farasi wake wenye nguvu 2 huenda mbio kwa kurukaruka. 1

23Malaika wa Bwana akasema, ‘Merozi alaaniwe. 2 Walaaniwe watu wake kwa uchungu, 1 kwa kuwa hawakuja kumsaidia Bwana, 2 kumsaidia Bwana dhidi ya hao wenye nguvu.’ 1

24“Yaeli abarikiwe kuliko wanawake wote, 2 mkewe Heberi, Mkeni, 1 abarikiwe kuliko wanawake wote 2 waishio kwenye mahema. 1

25Aliomba maji, naye akampa maziwa; 2 kwenye bakuli la heshima 2 akamletea maziwa mgando. 1

26Akanyoosha mkono wake 2 akashika kigingi cha hema, 1 mkono wake wa kuume 2 ukashika nyundo ya fundi. 1 Akampiga Sisera kwa nyundo, 2 akamponda kichwa chake, 1 akamvunjavunja na kumtoboa 2 paji lake la uso. 1

27Aliinama miguuni pa Yaeli, 2 akaanguka; akalala hapo. 1 Pale alipoinama miguuni pake, 2 alianguka; 1 pale alipoinamia, ndipo alipoanguka, 2 akiwa amekufa. 1

28“Kupitia dirishani mamaye Sisera alichungulia; 2 nyuma ya dirisha alilia, akasema, 1 ‘Mbona gari lake linachelewa kufika? 2 Mbona vishindo vya magari yake 2 vimechelewa?’ 1

29Wanawake wenye busara 2 kuliko wengine wote wakamjibu; 2 naam, husema moyoni mwake, 1

30‘Je, hawapati na kugawanya nyara: 2 msichana mmoja au wawili kwa kila mtu, 2 mavazi ya rangi mbalimbali kwa Sisera kuwa nyara, 2 mavazi ya rangi mbalimbali yaliyotariziwa, 2 mavazi yaliyotariziwa vizuri kwa ajili ya shingo yangu: 1 yote haya yakiwa nyara?’ 1

31“Adui zako wote na waangamie, Ee Bwana! 2 Bali wote wakupendao na wawe kama jua 2 lichomozavyo kwa nguvu zake.” Hivyo nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini.

← Judges 4Read In The App, Free →Judges 6 →

Study Judges 5

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021