Ufunuo 21:9
Kisha mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba yaliyokuwa yamejaa mabaa saba ya mwisho, akaja na kuniambia, “Njoo! Mimi nitakuonyesha bibi arusi, mkewe Mwanakondoo!”
Biblia Takatifu
In The King James Version
In Context
Cross References
Revelation 15:1Kisha nikaona ishara nyingine mbinguni, kubwa na ya kushangaza. Palikuwa hapo malaika saba wenye mabaa makubwa saba ya mwisho. Kwa mabaa hayo makubwa saba, ghadhabu ya Mungu imekamilishwa.
Revelation 17:1Mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na bakuli akaja, akaniambia, “Njoo, mimi nitakuonyesha adhabu aliyopewa yule mzinzi mkuu, mji ule uliojengwa juu ya maji mengi.
Revelation 21:2Nikaona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni. Ulikuwa umetayarishwa vizuri kama bibi arusi aliyepambwa tayari kukutana na mumewe.