Matendo 15:40
Naye Paulo akamchagua Sila, na baada ya ndugu wa mahali hapo kumweka chini ya ulinzi wa neema ya Bwana, akaondoka.
Biblia Takatifu
In The King James Version
And Paul chose Silas, and departed, being recommended by the brethren unto the grace of God.
In Context
41Katika safari hiyo alipitia Siria na Kilikia akiyaimarisha makanisa.
Cross References
Acts 13:3Basi, baada ya kusali na kufunga zaidi, wakawawekea mikono, wakawaacha waende zao.
Acts 15:22Mitume, wazee na kanisa lote waliamua kuwachagua watu fulani miongoni mwao na kuwatuma Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba. Basi, wakamchagua Yuda aitwaye pia Barsaba, na Sila ambao wote walikuwa wanajulikana zaidi kati ya ndugu.
Acts 16:1Paulo alifika Derbe na Lustra, ambako aliishi mfuasi mmoja aitwaye Timotheo. Mama yake ambaye pia alikuwa mfuasi, alikuwa Myahudi; lakini baba yake alikuwa Mgiriki.
1 Corinthians 15:10Lakini, kwa neema yake Mungu, nimekuwa kama nilivyo. Na neema yake kwangu haikuwa bure. Mimi nimefanya kazi kuliko wote; si mimi hasa, ila ni neema ya Mungu ifanyayo kazi pamoja nami.
2 Timothy 4:22Bwana awe nawe rohoni mwako. Nawatakieni nyote neema.
2 John 1:10Basi, kama mtu akija kwenu bila kuwaleteeni mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani kwenu, wala msimsalimu.