Joel · Biblia (Kiswahili)

Joel 2

1Pigeni tarumbeta katika Sayuni; 2 pigeni mbiu katika mlima wangu mtakatifu. 1 Wote waishio katika nchi na watetemeke, 2 kwa kuwa siku ya Bwana inakuja. Iko karibu, 1

2siku ya giza na huzuni, 2 siku ya mawingu na utusitusi. 1 Kama mapambazuko yasambaavyo 2 toka upande huu wa milima 2 hata upande mwingine 2 jeshi kubwa na lenye nguvu linakuja. 1 Jambo kama hili halijakuwepo tangu zamani 2 wala halitakuwepo tena kamwe 2 kwa vizazi vijavyo. 1

3Mbele yao moto unateketeza, 2 nyuma yao miali ya moto 2 inawaka kwa nguvu. 1 Mbele yao nchi iko kama bustani ya Edeni, 2 nyuma yao ni jangwa lisilofaa: 2 hakuna kitu kinachowaepuka. 1

4Wanaonekana kama farasi; 2 wanakwenda mbio 2 kama askari wapanda farasi. 1

5Wanatoa sauti kama magari ya vita, 2 wanaporukaruka juu ya vilele vya milima, 1 kama mlio wa miali ya moto ilayo mabua, 2 kama jeshi kubwa lililojipanga kwa ajili ya vita. 1

6Wanapoonekana, mataifa yanakuwa katika maumivu makuu; 2 kila uso unabadilika rangi. 1

7Wanashambulia kama wapiganaji wa vita; 2 wanapanda kuta kama askari. 1 Wote wanatembea katika safu, 2 hawapotoshi safu zao. 1

8Hakuna anayemsukuma mwenzake; 2 kila mmoja anakwenda mbele moja kwa moja. 1 Wanapita katika vizuizi 2 bila kuharibu safu zao. 1

9Wanaenda kasi kuingia mjini; 2 wanakimbia ukutani. 1 Wanaingia ndani ya nyumba; 2 kwa kuingilia madirishani kama wevi. 1

10Mbele yao dunia inatikisika, 2 anga linatetemeka, 1 jua na mwezi vinatiwa giza, 2 na nyota hazitoi mwanga wake tena. 1

11Bwana anatoa mshindo wa ngurumo 2 mbele ya jeshi lake; 1 majeshi yake hayana idadi, 2 ni wenye nguvu nyingi 2 wale ambao hutii agizo lake. 1 Siku ya Bwana ni kuu, 2 ni ya kutisha. 2 Ni nani anayeweza kuistahimili? 1 Rarueni Mioyo Yenu 1

12“Hata sasa,” asema Bwana, 2 “nirudieni kwa mioyo yenu yote, 2 kwa kufunga, kwa kulia na kuomboleza.” 1

13Rarueni mioyo yenu 2 na siyo mavazi yenu. 1 Mrudieni Bwana, Mungu wenu, 2 kwa maana yeye ndiye mwenye neema 2 na mwingi wa huruma, 1 si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo, 2 huona huruma, hujizuia kuleta maafa. 1

14Ni nani ajuaye? Yeye aweza kugeuka na kuwa na huruma 2 na kuacha baraka nyuma yake: 1 sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji 2 kwa ajili ya Bwana Mungu wenu. 1

15Pigeni tarumbeta katika Sayuni, 2 tangazeni saumu takatifu, 2 liiteni kusanyiko takatifu. 1

16Wakusanyeni watu, 2 wekeni wakfu kusanyiko; 1 waleteni pamoja wazee, 2 wakusanyeni watoto, 2 wale wanyonyao maziwa. 1 Bwana arusi na atoke chumbani mwake 2 na bibi arusi naye atoke katika chumba chake. 1

17Makuhani, ambao wanahudumu mbele za Bwana, 2 na walie katikati ya ukumbi 2 wa Hekalu na madhabahu. 1 Waseme, “Wahurumie watu wako, Ee Bwana. 2 Usifanye urithi wako kitu cha kudharauliwa, 2 neno la dhihaka kati ya mataifa. 1 Kwa nini wasemezane miongoni mwao, 2 ‘Yuko wapi Mungu wao?’ ” 1 Jibu La Bwana 1

18Kisha Bwana atakuwa na wivu kwa ajili ya nchi yake 2 na kuwa na huruma juu ya watu wake. 1

19Bwana atawajibu: 2 “Ninawapelekea nafaka, 2 mvinyo mpya na mafuta, 1 vya kuwatosha ninyi 2 hadi mridhike kabisa; 1 kamwe sitawafanya tena 2 kitu cha kudharauliwa na mataifa. 1

20“Nitafukuza jeshi la kaskazini likae mbali nanyi, 2 nikilisukuma ndani ya jangwa, 1 askari wa safu za mbele wakienda 2 ndani ya bahari ya mashariki 1 na wale wa safu za nyuma 2 katika bahari ya magharibi. 1 Uvundo wake utapaa juu; 2 harufu yake itapanda juu.” 1 Hakika ametenda mambo makubwa. 2

21Usiogope, ee nchi; 2 furahi na kushangilia. 1 Hakika Bwana ametenda mambo makubwa. 2

22Msiogope, enyi wanyama pori, 1 kwa kuwa mbuga za malisho yenu 2 zinarudia ubichi. 1 Miti nayo inazaa matunda, 2 mtini na mzabibu inatoa utajiri wake. 1

23Furahini, enyi watu wa Sayuni, 2 shangilieni katika Bwana Mungu wenu, 1 kwa kuwa amewapa mvua za vuli 2 kwa kipimo cha haki. 1 Anawapelekea mvua nyingi, 2 mvua ya vuli na ya masika, kama mwanzoni. 1

24Sakafu za kupuria zitajaa nafaka, 2 mapipa yatafurika mvinyo mpya na mafuta. 1

25“Nitawalipa kwa ajili ya miaka ile iliyoliwa na nzige: 2 parare, madumadu na tunutu, 1 jeshi langu kubwa ambalo 2 nililituma katikati yenu. 1

26Mtakuwa na wingi wa vyakula mpaka mshibe, 2 na mtalisifu jina la Bwana Mungu wenu, 1 ambaye amefanya maajabu kwa ajili yenu; 2 kamwe watu wangu hawataaibishwa tena. 1

27Ndipo mtakapojua kwamba mimi niko katika Israeli 2 kwamba mimi ndimi Bwana Mungu wenu, 2 na kwamba hakuna mwingine; 1 kamwe watu wangu hawataaibika tena. 1 Siku Ya Bwana 1

28“Hata itakuwa, baada ya hayo, 2 nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili. 1 Wana wenu na binti zenu watatabiri, 2 wazee wenu wataota ndoto, 2 na vijana wenu wataona maono. 1

29Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake, 2 katika siku zile nitamimina Roho wangu. 1

30Nami nitaonyesha maajabu katika mbingu 2 na duniani: 2 damu, moto na mawimbi ya moshi. 1

31Jua litageuzwa kuwa giza 2 na mwezi kuwa mwekundu kama damu, 1 kabla ya kuja siku ya Bwana 2 ile kuu na ya kutisha. 1

32Na kila mtu atakayeliitia 2 jina la Bwana ataokolewa. 1 Kwa maana juu ya Mlima Sayuni na katika Yerusalemu 2 kutakuwepo wokovu, 2 kama Bwana alivyosema, 1 miongoni mwa walionusurika 2 ambao Bwana awaita.

← Joel 1Read In The App, Free →Joel 3 →

Study Joel 2

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123