Joel 1
1Neno la Bwana ambalo lilimjia Yoeli mwana wa Pethueli. 1 Uvamizi Wa Nzige 1
2Sikilizeni hili, enyi wazee; 2 sikilizeni, ninyi nyote mnaoishi katika nchi. 1 Je, jambo kama hili lilishawahi kutokea 2 katika siku zenu au katika siku za babu zenu? 1
3Waelezeni watoto wenu, 2 na watoto wenu wawaambie watoto wao, 2 na watoto wao kwa kizazi kitakachofuata. 1
4Kilichosazwa na kundi la tunutu 2 nzige wakubwa wamekula, 1 kilichosazwa na nzige wakubwa 2 parare wamekula, 1 kilichosazwa na parare 2 madumadu wamekula. 1
5Amkeni, enyi walevi, mlie! 2 Pigeni yowe enyi wanywaji wote wa mvinyo, 1 pigeni yowe kwa sababu ya mvinyo mpya, 2 kwa kuwa mmenyangʼanywa 2 kutoka midomoni mwenu. 1
6Taifa limevamia nchi yangu, 2 lenye nguvu tena lisilo na idadi; 1 lina meno ya simba, 2 magego ya simba jike. 1
7Limeharibu mizabibu yangu 2 na kuangamiza mitini yangu. 1 Limebambua magome yake 2 na kuyatupilia mbali, 2 likayaacha matawi yake yakiwa meupe. 1
8Omboleza kama bikira aliyevaa nguo ya gunia 2 anayehuzunika kwa ajili ya mume wa ujana wake. 1
9Sadaka za nafaka na sadaka za kinywaji 2 zimekatiliwa mbali kutoka nyumba ya Bwana. 1 Makuhani wanaomboleza, 2 wale wanaohudumu mbele za Bwana. 1
10Mashamba yameharibiwa, 2 ardhi imekauka; 1 nafaka imeharibiwa, 2 mvinyo mpya umekauka, 2 mafuta yamekoma. 1
11Kateni tamaa, enyi wakulima, 2 lieni, enyi mlimao mizabibu; 1 huzunikeni kwa ajili ya ngano na shayiri, 2 kwa sababu mavuno ya shambani yameharibiwa. 1
12Mzabibu umekauka 2 na mtini umenyauka; 1 mkomamanga, mtende na mtofaa, 2 miti yote shambani, imekauka. 1 Hakika furaha yote ya mwanadamu 2 imeondoka. 1 Wito Wa Toba 1
13Vaeni nguo ya gunia, enyi makuhani, muomboleze; 2 pigeni yowe, enyi mnaohudumu madhabahuni. 1 Njooni, vaeni nguo ya gunia usiku kucha, 2 enyi mnaohudumu mbele za Mungu wangu; 1 kwa kuwa sadaka za nafaka na sadaka za kinywaji 2 zimezuiliwa kufika katika nyumba ya Mungu wenu. 1
14Tangazeni saumu takatifu; 2 liiteni kusanyiko takatifu. 1 Iteni wazee 2 na wote waishio katika nchi 1 waende katika nyumba ya Bwana Mungu wenu, 2 wakamlilie Bwana. 1
15Ole kwa siku hiyo! 2 Kwa kuwa siku ya Bwana iko karibu; 1 itakuja kama uharibifu 2 kutoka kwa Mwenyezi. + 1:15 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania. 1
16Je, chakula hakikukatiliwa mbali 2 mbele ya macho yetu: 1 furaha na shangwe 2 kutoka nyumba ya Mungu wetu? 1
17Mbegu zinakauka 2 chini ya mabonge ya udongo. 1 Ghala zimeachwa katika uharibifu, 2 ghala za nafaka zimebomolewa, 2 kwa maana hakuna nafaka. 1
18Jinsi gani ngʼombe wanavyolia! 2 Makundi ya mifugo yanahangaika 1 kwa sababu hawana malisho; 2 hata makundi ya kondoo yanateseka. 1
19Kwako, Ee Bwana, naita, 2 kwa kuwa moto umeteketeza 2 malisho ya mbugani 1 na miali ya moto imeunguza 2 miti yote shambani. 1
20Hata wanyama wa porini wanakuonea shauku; 2 vijito vya maji vimekauka, 1 na moto umeteketeza 2 malisho yote ya mbugani.