Obadiah · Biblia (Kiswahili)

Obadiah 1

1Maono ya Obadia. Hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi kuhusu Edomu: 1 Tumesikia ujumbe kutoka kwa Bwana: 2 Mjumbe alitumwa kwa mataifa kusema, 1 “Inukeni, twendeni tukapigane vita dhidi yake.” 1

2“Angalieni, nitawafanya wadogo miongoni mwa mataifa, 2 mtadharauliwa kabisa. 1

3Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, 2 wewe unayeishi katika majabali ya miamba 2 na kufanya makao yako juu, 1 wewe unayejiambia mwenyewe, 2 ‘Ni nani awezaye kunishusha chini?’ 1

4Ingawa unapaa juu kama tai 2 na kufanya kiota chako kati ya nyota, 2 nitakushusha chini kutoka huko,” 4 asema Bwana. 1

5“Ikiwa wevi wangekuja kwako, 2 ikiwa wanyangʼanyi wangekujia usiku: 1 Lo! Tazama ni maafa kiasi gani yangekuwa yanakungojea: 2 je, si wangeiba tu kiasi ambacho wangehitaji? 1 Kama wachuma zabibu wangekuja kwako, 2 je, wasingebakiza zabibu chache? 1

6Lakini tazama jinsi Esau atakavyotekwa, 2 jinsi hazina zake zilizofichwa zitatekwa nyara! 1

7Wote ulioungana nao watakufukuza hadi mpakani, 2 rafiki zako watakudanganya na kukushinda, 1 wale wanaokula mkate wako watakutegea mtego, 2 lakini hutaweza kuugundua. 1

8“Katika siku hiyo,” asema Bwana, 2 “je, sitaangamiza watu wenye hekima wa Edomu, 2 watu wenye ufahamu katika milima ya Esau? 1

9Ee Temani, mashujaa wako watatiwa hofu, 2 kila mmoja katika milima ya Esau 2 ataangushwa chini kwa kuchinjwa. 1

10Kwa sababu ya jeuri uliyofanya dhidi ya ndugu yako Yakobo, 2 aibu itakufunika; 2 utaangamizwa milele. 1

11Siku ile ulisimama mbali ukiangalia 2 wakati wageni walipojichukulia utajiri wake 1 na watu wa nchi nyingine walipoingia malango yake 2 wakipiga kura kwa ajili ya Yerusalemu, 2 ulikuwa kama mmoja wao. 1

12Usingemdharau ndugu yako 2 katika siku ya msiba wake, 1 wala kufurahia juu ya watu wa Yuda 2 katika siku ya maangamizi yao, 1 wala kujigamba sana 2 katika siku ya taabu yao. 1

13Usingeingia katika malango ya watu wangu 2 katika siku ya maafa yao, 1 wala kuwadharau katika janga lao 2 katika siku ya maafa yao, 1 wala kunyangʼanya mali zao 2 katika siku ya maafa yao. 1

14Usingengoja kwenye njia panda 2 na kuwaua wakimbizi wao, 1 wala kuwatoa watu wake waliosalia 2 katika siku ya shida yao. 1

15“Siku ya Bwana iko karibu 2 kwa mataifa yote. 1 Kama ulivyofanya, nawe utafanyiwa vivyo hivyo, 2 matendo yako yatakurudia juu ya kichwa chako. 1

16Kama vile ulivyokunywa juu ya mlima wangu mtakatifu, 2 vivyo hivyo mataifa yote watakunywa mfululizo, 1 watakunywa na kunywa, 2 nao watatoweka kana kwamba hawajawahi kuwepo. 1

17Lakini katika Mlima Sayuni kutakuwepo 2 na wale watakaookoka; 2 nao utakuwa mtakatifu, 1 nayo nyumba ya Yakobo 2 itamiliki urithi wake. 1

18Nyumba ya Yakobo itakuwa moto, 2 na nyumba ya Yosefu itakuwa mwali wa moto; 1 nayo nyumba ya Esau itakuwa bua kavu, 2 nao wataiwasha moto na kuiteketeza. 1 Hakutakuwa na watakaosalimika 2 kutoka nyumba ya Esau.” 4 Bwana amesema. 1

19Watu kutoka nchi ya Negebu 2 wataikalia milima ya Esau, 1 na watu kutoka miteremko ya vilima 2 watamiliki nchi ya Wafilisti. 1 Watayakalia mashamba ya Efraimu na Samaria, 2 naye Benyamini atamiliki Gileadi. 1

20Kundi la Waisraeli walioko uhamishoni Kanaani 2 watarudi na kumiliki nchi mpaka Sarepta. 1 Walioko uhamishoni Sefaradi kutoka Yerusalemu 2 watamiliki miji ya Negebu. 1

21Waokoaji watakwea juu ya Mlima Sayuni 2 kutawala milima ya Esau. 2 Nao ufalme utakuwa wa Bwana.

← Amos 9Read In The App, Free →Jonah 1 →

Study Obadiah 1

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

1