Amos 9
1Nilimwona Bwana akiwa amesimama kando ya madhabahu, naye akasema: 1 “Piga vichwa vya nguzo 2 ili vizingiti vitikisike. 1 Viangushe juu ya vichwa vya watu wote; 2 na wale watakaosalia nitawaua kwa upanga. 1 Hakuna awaye yote atakayekimbia, 2 hakuna atakayetoroka. 1
2Wajapojichimbia chini mpaka kwenye vina vya kuzimu, 2 kutoka huko mkono wangu utawatoa. 1 Wajapopanda juu hadi kwenye mbingu, 2 kutoka huko nitawashusha. 1
3Wajapojificha juu ya kilele cha Karmeli, 2 huko nitawawinda na kuwakamata. 1 Wajapojificha kutoka kwenye uso wangu 2 katika vilindi vya bahari, 2 huko nako nitaamuru joka kuwauma. 1
4Wajapopelekwa uhamishoni na adui zao, 2 huko nako nitaamuru upanga uwaue. 1 Nitawakazia macho yangu kwa mabaya 2 wala si kwa mazuri.” 1
5Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 yeye agusaye dunia nayo ikayeyuka, 2 na wote wakaao ndani mwake wakaomboleza: 1 nayo nchi yote huinuka kama Naili, 2 kisha hushuka kama mto wa Misri; 1
6yeye ambaye hujenga jumba lake la kifalme katika mbingu 2 na kuisimika misingi yake juu ya dunia, 1 yeye aitaye maji ya bahari 2 na kuyamwaga juu ya uso wa nchi: 2 Bwana ndilo jina lake. 1
7“Je, Waisraeli, 2 ninyi si sawa kwangu kama Wakushi?” 4 asema Bwana. 1 “Je, sikuleta Israeli kutoka Misri, 2 Wafilisti kutoka Kaftori, + 9:7 Yaani Krete. 2 na Washamu kutoka Kiri? 1
8“Hakika macho ya Bwana Mwenyezi 2 yako juu ya ufalme wenye dhambi. 1 Nami nitauangamiza 2 kutoka kwenye uso wa dunia: 1 hata hivyo sitaiangamiza kabisa 2 nyumba ya Yakobo,” 4 asema Bwana. 1
9“Kwa kuwa nitatoa amri, 2 na nitaipepeta nyumba ya Israeli 2 miongoni mwa mataifa yote, 1 kama vile nafaka ipepetwavyo katika ungo, 2 na hakuna hata punje moja itakayoanguka chini. 1
10Watenda dhambi wote miongoni mwa watu wangu 2 watauawa kwa upanga, 1 wale wote wasemao, 2 ‘Maafa hayatatupata wala kutukuta.’ 1 Kurejezwa Kwa Israeli 1
11“Katika siku ile nitaisimamisha 2 hema ya Daudi iliyoanguka. 1 Nitakarabati mahali palipobomoka 2 na kujenga upya magofu yake, 2 na kuijenga kama ilivyokuwa awali, 1
12ili wapate kuyamiliki mabaki ya Edomu, 2 na mataifa yote yale yanayobeba Jina langu,” 4 asema Bwana ambaye atafanya mambo haya.
13“Siku zinakuja,” asema Bwana, 1 “wakati mvunaji atatanguliwa na mkulima, 2 naye mpanzi atatanguliwa na yeye akamuaye zabibu. 1 Divai mpya itadondoka kutoka milimani, 2 na kutiririka kutoka vilima vyote. 1
14Nitawarejesha tena watu wangu Israeli waliohamishwa; 2 wataijenga tena miji iliyoachwa magofu, 2 nao wataishi ndani mwake. 1 Watapanda mizabibu na kunywa divai yake; 2 watalima bustani na kula matunda yake. 1
15Nitaipanda Israeli katika nchi yao wenyewe, 2 hawatangʼolewa tena 2 kutoka nchi ambayo nimewapa,” 4 asema Bwana Mungu wenu.