Zechariah 10
1Mwombeni Bwana mvua wakati wa vuli; 2 ndiye Bwana atengenezaye mawingu ya tufani. 1 Huwapa watu manyunyu ya mvua, 2 pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila mtu. 1
2Sanamu huzungumza udanganyifu, 2 waaguzi huona maono ya uongo; 1 husimulia ndoto ambazo si za kweli, 2 wanatoa faraja batili. 1 Kwa hiyo watu wanatangatanga kama kondoo 2 walioonewa kwa kukosa mchungaji. 1
3“Hasira yangu inawaka dhidi ya wachungaji, 2 nami nitawaadhibu viongozi; 1 kwa kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote 2 atalichunga kundi lake, 2 nyumba ya Yuda, 1 naye atawafanya kuwa kama farasi 2 mwenye kiburi akiwa vitani. 1
4Kutoka Yuda litatokea Jiwe la pembeni, 2 kutoka kwake vitatoka vigingi vya hema, 2 kutoka kwake utatoka upinde wa vita, 2 kutoka kwake atatoka kila mtawala. 1
5Kwa pamoja watakuwa kama mashujaa 2 wanaokanyaga barabara za matope 2 wakati wa vita. 1 Kwa sababu Bwana yu pamoja nao, 2 watapigana na kuwashinda wapanda farasi. 1
6“Nitaiimarisha nyumba ya Yuda 2 na kuiokoa nyumba ya Yosefu. 1 Nitawarejesha kwa sababu 2 nina huruma juu yao. 1 Watakuwa kama watu ambao 2 sijawahi kuwakataa 1 kwa sababu mimi ndimi Bwana Mungu wao, 2 nami nitawajibu. 1
7Waefraimu watakuwa kama mashujaa, 2 mioyo yao itafurahi kana kwamba ni kwa divai. 1 Watoto wao wataona na kufurahi, 2 mioyo yao itashangilia katika Bwana. 1
8Nitawaashiria na kuwakusanya ndani. 2 Hakika nitawakomboa, 1 nao watakuwa wengi 2 kama walivyokuwa mwanzoni. 1
9Ijapokuwa niliwatawanya miongoni mwa mataifa, 2 hata hivyo wakiwa katika nchi za mbali 2 watanikumbuka mimi. 1 Wao na watoto wao watanusurika katika hatari 2 nao watarudi. 1
10Nitawarudisha kutoka Misri 2 na kuwakusanya toka Ashuru. 1 Nitawaleta katika nchi ya Gileadi na Lebanoni, 2 na hapo hapatakuwa na nafasi ya kuwatosha. 1
11Watapita katika bahari ya mateso; 2 bahari iliyochafuka itatulizwa 2 na vilindi vyote vya Mto Naili vitakauka. 1 Kiburi cha Ashuru kitashushwa, 2 nayo fimbo ya utawala ya Misri itatoweka. 1
12Nitawaimarisha katika Bwana, 2 na katika jina lake watatembea,” 4 asema Bwana.