Zechariah 9
1Neno: 1 Neno la Bwana liko kinyume na nchi ya Hadraki 2 na Dameski itakuwa mahali pa kupumzika, 1 kwa kuwa macho ya watu na ya kabila zote 2 za Israeli yako kwa Bwana, 1
2pia juu ya Hamathi inayopakana nayo, 2 juu ya Tiro na Sidoni, 2 ingawa wana ujuzi mwingi sana. 1
3Tiro amejijengea ngome imara, 2 amelundika fedha kama mavumbi 2 na dhahabu kama taka za mitaani. 1
4Lakini Bwana atamwondolea mali zake 2 na kuuangamiza uwezo wake wa baharini, 2 naye atateketezwa kwa moto. 1
5Ashkeloni ataona hili na kuogopa; 2 Gaza atagaagaa kwa maumivu makali, 1 pia Ekroni, kwa sababu 2 matumaini yake yatanyauka. 1 Gaza atampoteza mfalme wake 2 na Ashkeloni ataachwa pweke. 1
6Wageni watakalia mji wa Ashdodi, 2 nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti. 1
7Nitaondoa damu vinywani mwao, 2 chakula kile walichokatazwa kati ya meno yao. 1 Mabaki yao yatakuwa mali ya Mungu wetu, 2 nao watakuwa viongozi katika Yuda, 2 naye Ekroni atakuwa kama Wayebusi. 1
8Lakini nitailinda nyumba yangu 2 dhidi ya majeshi ya wanyangʼanyi. 1 Kamwe mdhalimu hatashambulia watu wangu tena, 2 kwa maana sasa ninawachunga. 1 Kuja Kwa Mfalme Wa Sayuni 1
9Shangilia sana, ee Binti Sayuni! 2 Piga kelele, Binti Yerusalemu! 1 Tazama, Mfalme wako anakuja kwako, 2 ni mwenye haki, naye ana wokovu, 2 ni mpole, naye amepanda punda, 2 mwana-punda, mtoto wa punda. 1
10Nitaondoa magari ya vita kutoka Efraimu 2 na farasi wa vita kutoka Yerusalemu, 2 nao upinde wa vita utavunjwa. 1 Atatangaza amani kwa mataifa. 2 Utawala wake utaenea kutoka bahari hadi bahari, 2 na kutoka Mto Frati hadi mwisho wa dunia. 1
11Kwako wewe, kwa sababu ya damu ya Agano langu nawe, 2 nitawaacha huru wafungwa wako 2 watoke kwenye shimo lisilo na maji. 1
12Rudieni ngome yenu, enyi wafungwa wa tumaini; 2 hata sasa ninatangaza kwamba 2 nitawarejesheeni maradufu. 1
13Nitampinda Yuda kama nipindavyo upinde wangu, 2 nitamfanya Efraimu mshale wangu. 1 Nitawainua wana wako, ee Sayuni, 2 dhidi ya wana wako, ee Uyunani, 2 na kukufanya kama upanga wa shujaa wa vita. 1 Bwana Atatokea 1
14Kisha Bwana atawatokea; 2 mshale wake utamulika 2 kama umeme wa radi. 1 Bwana Mwenyezi atapiga tarumbeta, 2 naye atatembea katika tufani za kusini, 2
15na Bwana Mwenye Nguvu Zote atawalinda. 1 Wataangamiza na kushinda 2 kwa mawe ya kutupa kwa kombeo. 1 Watakunywa na kunguruma kama waliolewa mvinyo; 2 watajaa kama bakuli linalotumika kunyunyizia 2 kwenye pembe za madhabahu. 1
16Bwana Mungu wao atawaokoa siku hiyo 2 kama kundi la watu wake. 1 Watangʼara katika nchi yake 2 kama vito vya thamani kwenye taji. 1
17Jinsi gani watavutia na kuwa wazuri! 2 Nafaka itawastawisha vijana wanaume, 2 nayo divai mpya vijana wanawake.