Ecclesiastes 10
1Kama vile nzi waliokufa huacha harufu mbaya kwenye manukato, 2 ndivyo upumbavu kidogo huzidi nguvu hekima na heshima. 1
2Moyo wa mwenye hekima huelekea kuume, 2 lakini moyo wa mpumbavu huelekea kushoto. 1
3Hata anapotembea barabarani, 2 mpumbavu hukosa ufahamu 1 na kudhihirisha kwa kila mmoja 2 jinsi alivyo mpumbavu. 1
4Kama hasira ya mtawala ikiwaka dhidi yako, 2 usiache mahali pako, 2 utulivu huweza kuzuia makosa mengi. 1
5Kuna ubaya niliouona chini ya jua, 2 aina ya kosa litokalo kwa mtawala: 1
6Wapumbavu kuwekwa kwenye nafasi nyingi za juu, 2 wakati matajiri hushika nafasi za chini. 1
7Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, 2 wakati wakuu wakitembea 2 kwa miguu kama watumwa. 1
8Yeye achimbaye shimo 2 aweza kutumbukia ndani yake, 1 yeyote abomoaye ukuta 2 anaweza kuumwa na nyoka. 1
9Yeyote apasuaye mawe 2 inawezekana yakamuumiza, 1 yeyote apasuaye magogo 2 inawezekana yakamuumiza. 1
10Kama shoka ni butu 2 na halikunolewa, 1 nguvu nyingi zinahitajika, 2 lakini ustadi utaleta mafanikio. 1
11Kama nyoka akiuma kabla ya kufanyiwa uaguzi, 2 mwaguzi hatahitajika tena. 1
12Maneno yatokayo kinywani mwa mtu mwenye hekima 2 yana neema, 2 bali mpumbavu huangamizwa 2 na midomo yake mwenyewe. 1
13Mwanzoni maneno yake ni upumbavu, 2 mwishoni ni wazimu mbaya, 2
14naye mpumbavu huzidisha maneno. 1 Hakuna yeyote ajuaye linalokuja, 2 ni nani awezaye kueleza ni jambo gani 2 litakalotokea baada yake? 1
15Kazi ya mpumbavu humchosha mwenyewe, 2 hajui njia iendayo mjini. 1
16Ole wako, ee nchi ambayo mfalme wako alikuwa mtumwa 2 na ambayo wakuu wako hufanya karamu asubuhi. 1
17Heri wewe, ee nchi ambayo mfalme wako ni wa uzao wenye kuheshimika 2 na ambayo wakuu wako hula chakula kwa wakati unaofaa: 2 ili kupata nguvu na si kwa ajili ya ulevi. 1
18Kama mtu ni mvivu paa la nyumba huinama, 2 kutokana na mikono milegevu, nyumba huvuja. 1
19Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, 2 nao mvinyo hufurahisha maisha, 2 lakini fedha ni jawabu la mambo yote. 1
20Usimshutumu mfalme hata ikiwa ni katika mawazo yako, 2 au kumlaani tajiri katika chumba chako cha kulala, 1 kwa sababu ndege wa angani wanaweza kuchukua maneno yako, 2 naye ndege anayeruka anaweza kutoa taarifa ya yale uliyosema.