Ecclesiastes 7
1Afadhali sifa nzuri kuliko manukato safi, 2 nayo siku ya kufa kuliko ya kuzaliwa. 1
2Afadhali kwenda kwenye nyumba ya msiba 2 kuliko kwenda kwenye nyumba ya karamu, 1 kwa kuwa kifo ni hatima ya kila mwanadamu, 2 imewapasa walio hai kuliweka hili mioyoni mwao. 1
3Huzuni ni afadhali kuliko kicheko, 2 kwa sababu uso wenye huzuni wafaa kwa moyo. 1
4Moyo wa wenye hekima uko katika nyumba ya msiba, 2 lakini moyo wa wapumbavu uko katika nyumba ya anasa. 1
5Afadhali kusikia karipio la mtu mwenye hekima, 2 kuliko kusikiliza wimbo wa wapumbavu. 1
6Kama ilivyo kuvunjika kwa miiba chini ya sufuria, 2 ndivyo kilivyo kicheko cha wapumbavu. 2 Hili nalo pia ni ubatili. 1
7Dhuluma humfanya mtu mwenye hekima kuwa mpumbavu, 2 nayo rushwa huuharibu moyo. 1
8Mwisho wa jambo ni bora kuliko mwanzo wake, 2 uvumilivu ni bora kuliko kiburi. 1
9Usiwe mwepesi kukasirika rohoni mwako, 2 kwa kuwa hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu. 1
10Usiseme, “Kwa nini siku za kale zilikuwa bora kuliko siku hizi?” 2 Kwa maana si hekima kuuliza maswali kama hayo. 1
11Hekima, kama ulivyo urithi, ni kitu chema 2 na huwafaidia wale walionalo jua. 1
12Hekima ni ulinzi kama fedha ilivyo ulinzi, 2 lakini faida ya maarifa ni hii: 2 kwamba hekima huhifadhi maisha ya aliye nayo.
13Tafakari kile Mungu alichokitenda: 1 Nani awezaye kunyoosha 2 kile ambacho yeye amekipinda? 1
14Nyakati zikiwa nzuri, ufurahi, 2 lakini nyakati zikiwa mbaya, tafakari: 1 Mungu amefanya hiyo moja, 2 naam, sanjari + 7:14 Sanjari hapa maana yake mwandamano wa vitu, wanyama au watu. na hiyo nyingine. 1 Kwa hiyo, mwanadamu hawezi kugundua 2 kitu chochote kuhusu maisha yake ya baadaye.
15Katika maisha haya yangu ya ubatili nimeshaona haya mawili: 1 mtu mwadilifu akiangamia katika uadilifu wake, 2 naye mtu mwovu akiishi maisha marefu katika uovu wake. 1
16Usiwe mwenye haki kupita kiasi, 2 wala usiwe na hekima kupita kiasi: 2 kwa nini kujiangamiza mwenyewe? 1
17Usiwe mwovu kupita kiasi, 2 wala usiwe mpumbavu: 2 kwa nini kufa kabla ya wakati wako? 1
18Ni vyema kushika hilo moja 2 na wala usiache hilo jingine likupite. 2 Mtu amchaye Mungu ataepuka huko kupita kiasi. + 7:18 Au: atafuata hayo yote mawili. 1
19Hekima humfanya yeye aliye nayo kuwa na uwezo zaidi 2 kuliko watawala kumi katika mji. 1
20Hakuna mtu mwenye haki duniani 2 ambaye hufanya mambo ya haki 2 na kamwe asitende dhambi. 1
21Usitie maanani kila neno linalosemwa na watu, 2 la sivyo, waweza kumsikia 2 mtumishi wako akikulaani: 1
22kwa kuwa unafahamu moyoni mwako 2 kwamba wewe mwenyewe mara nyingi 2 umewalaani wengine.
23Yote haya niliyajaribu kwa hekima, nikasema, 1 “Nimeamua kuwa na hekima”: 2 lakini hii ilikuwa nje ya uwezo wangu. 1
24Vyovyote hekima ilivyo, 2 hekima iko mbali sana na imejificha, 2 ni nani awezaye kuigundua? 1
25Nikageuza fikira zangu ili kuelewa, 2 kuchunguza na kuitafuta hekima 2 na kusudi la mambo, 1 na ili kuelewa ujinga wa uovu, 2 na wazimu wa upumbavu. 1
26Nimeona jambo lililo chungu kuliko mauti, 2 mwanamke ambaye ni mtego, 1 ambaye moyo wake ni wavu wa kutegea 2 na mikono yake ni minyororo. 1 Mtu ampendezaye Mungu atamkwepa, 2 bali mwenye dhambi atanaswa naye.
27Mhubiri anasema, “Tazama, hili ndilo nililogundua: 1 “Nimegundua kitu kimoja baada ya kingine nilipokuwa katika kusudi la mambo: 2
28ningali natafiti 2 lakini sipati: 1 nilimpata mwanaume mmoja mnyofu miongoni mwa elfu, 2 lakini hakuna mwanamke mmoja mnyofu miongoni mwao. 1
29Hili ndilo peke yake nililolipata: 2 Mungu amemuumba mwanadamu mnyofu, 2 lakini mwanadamu amebuni mambo mengi.”