Ecclesiastes 11
1Tupa mkate wako juu ya maji, 2 kwa maana baada ya siku nyingi 2 utaupata tena. 1
2Wape sehemu watu saba, naam hata wanane, 2 kwa maana hujui ni baa gani 2 litakalokuwa juu ya nchi. 1
3Kama mawingu yamejaa maji, 2 hunyesha mvua juu ya nchi. 1 Kama mti ukianguka kuelekea kusini 2 au kuelekea kaskazini, 1 mahali ulipoangukia, 2 hapo ndipo utakapolala. 1
4Yeyote atazamaye upepo hatapanda, 2 yeyote aangaliaye mawingu hatavuna. 1
5Kama vile usivyofahamu njia ya upepo, 2 au jinsi mwili uumbwavyo 2 ndani ya tumbo la mama, 1 vivyo hivyo huwezi kufahamu kazi ya Mungu, 2 Muumba wa vitu vyote. 1
6Panda mbegu yako asubuhi, 2 nako jioni usiruhusu mikono yako ilegee, 1 kwa maana hujui ni ipi itakayofanikiwa, 2 kwamba ni hii au ni ile, 2 au kwamba zote zitafanikiwa sawasawa. 1 Mkumbuke Muumba Wako Ukiwa Bado Kijana 1
7Nuru ni tamu, 2 tena inafurahisha macho kuona jua. 1
8Hata kama mtu ataishi miaka mingi kiasi gani, 2 na aifurahie yote. 1 Lakini na akumbuke siku za giza, 2 kwa maana zitakuwa nyingi. 2 Kila kitu kitakachokuja ni ubatili. 1
9Furahi ewe kijana, wakati ungali kijana, 2 moyo wako na ukupe furaha 2 katika siku za ujana wako. 1 Fuata njia za moyo wako 2 na chochote macho yako yaonayo, 1 lakini ujue kwamba kwa ajili ya haya yote 2 Mungu atakuleta hukumuni. 1
10Kwa hiyo basi, ondoa wasiwasi moyoni mwako 2 na utupilie mbali masumbufu ya mwili wako, 2 kwa kuwa ujana na nguvu ni ubatili.