Habakkuk · Biblia (Kiswahili)

Habakkuk 2

1Nitasimama katika zamu yangu, 2 na kujiweka mwenyewe juu ya maboma; 1 nitatazama nione atakaloniambia, 2 na ni jibu gani nitakalotoa kuhusu lalamiko hili. 1 Jibu La Bwana

2Kisha Bwana akajibu: 1 “Andika ufunuo huu, 2 na ukaufanye wazi juu ya vibao, 2 ili mpiga mbiu akimbie nao. 1

3Kwa kuwa ufunuo huu unasubiri wakati uliokubalika; 2 unazungumzia mambo ya mwisho, 2 na kamwe hautakosea. 1 Iwapo utakawia, wewe usubiri; 2 kwa hakika utakuja na hautachelewa. 1

4“Tazama, amejaa majivuno; 2 anavyovitamani si vya unyofu: 2 lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake: 1

5hakika mvinyo humsaliti; 2 ni mwenye kiburi na hana amani. 1 Kwa sababu ni mlafi kama kuzimu 2 na kama kifo kamwe hatosheki; 1 anajikusanyia mataifa yote 2 na kuchukua watu wote mateka.

6“Je, watu wote hawatamsuta kwa dhihaka na kumbeza, wakisema, 1 “ ‘Ole wake yeye akusanyaye bidhaa zilizoibwa 2 na kujifanyia utajiri kwa kutoza kwa nguvu! 2 Ataendelea hivi kwa muda gani?’ 1

7Je, wadai wako hawatainuka ghafula? 2 Je, hawataamka na kukufanya utetemeke? 2 Kisha utakuwa mhanga kwao. 1

8Kwa kuwa umeteka nyara mataifa mengi, 2 watu waliobaki watakuteka nyara wewe. 1 Kwa kuwa umemwaga damu ya mtu; 2 umeharibu nchi na miji, na kila mmoja ndani yake. 1

9“Ole wake yeye ajengaye milki yake kwa mapato ya udhalimu, 2 awekaye kiota chake juu, 2 ili kukimbia makucha ya uharibifu! 1

10Umefanya shauri la maangamizi ya watu wengi, 2 ukiaibisha nyumba yako mwenyewe, na kupotewa na maisha yako. 1

11Mawe ya kuta yatapiga kelele, 2 na mihimili ya kazi ya mbao itarudisha mwangwi wake. 1

12“Ole wake yeye ajengaye mji kwa kumwaga 2 damu na kuusimamisha mji kwa uhalifu! 1

13Je, Bwana Mwenye Nguvu Zote hakuonyesha 2 kwamba kazi ya wanadamu ni mafuta tu kwa ajili ya moto, 1 na kwamba mataifa 2 yanajichosha bure? 1

14Kwa kuwa dunia itajazwa na maarifa ya utukufu wa Bwana, 2 kama maji yaifunikavyo bahari. 1

15“Ole wake yeye awapaye jirani zake kileo, 2 akiimimina kutoka kwenye kiriba 2 cha mvinyo mpaka wamelewa, 2 ili apate kutazama miili yao iliyo uchi. 1

16Utajazwa na aibu badala ya utukufu. 2 Sasa ni zamu yako! Kunywa na ujifunue! 1 Kikombe kutoka kwenye mkono wa kuume wa Bwana kinakujia, 2 na aibu itafunika utukufu wako. 1

17Ukatili ulioifanyia Lebanoni utakufunika, 2 na uharibifu uliowafanyia wanyama utakutisha. 1 Kwa sababu umemwaga damu ya mtu; 2 umeharibu nchi na miji na kila mmoja aliyeko ndani yake. 1

18“Sanamu ina thamani gani, 2 kwani mwanadamu ndiye alichonga? 1 Ama kinyago kinachofundisha uongo? 2 Kwa kuwa yeye aliyekitengeneza 1 hutegemea kazi ya mikono yake mwenyewe; 2 hutengeneza sanamu zisizoweza kuzungumza. 1

19Ole wake yeye auambiaye mti, ‘Uwe hai!’ 2 Ama asemaye na jiwe lisilo na uhai, ‘Amka!’ 1 Je, linaweza kuongoza? 2 Limefunikwa kwa dhahabu na fedha; 2 hakuna pumzi ndani yake. 1

20Lakini Bwana yuko katika Hekalu lake takatifu; 2 dunia yote na inyamaze mbele yake.”

← Habakkuk 1Read In The App, Free →Habakkuk 3 →

Study Habakkuk 2

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123