Habakkuk 1
1Neno alilopokea nabii Habakuki. 1 Lalamiko La Habakuki 1
2Ee Bwana, hata lini nitakuomba msaada, 2 lakini wewe husikilizi? 1 Au kukulilia, “Udhalimu!” 2 Lakini hutaki kuokoa? 1
3Kwa nini unanifanya nitazame dhuluma? 2 Kwa nini unavumilia makosa? 1 Uharibifu na udhalimu viko mbele yangu; 2 kuna mabishano na mapambano kwa wingi. 1
4Kwa hiyo sheria imepotoshwa, 2 nayo haki haipo kabisa. 1 Waovu wanawazunguka wenye haki, 2 kwa hiyo haki imepotoshwa. 1 Jibu La Bwana 1
5“Yatazame mataifa, 2 uangalie na ushangae kabisa. 1 Kwa sababu katika siku zako nitafanya kitu 2 ambacho hungeamini, 2 hata kama ungeambiwa. 1
6Nitawainua Wakaldayo, 2 watu hao wakatili na wenye haraka, 1 ambao hupita dunia yote 2 kuteka mahali pa kuishi pasipo pao wenyewe. 1
7Ni watu wanoogopwa na wanaotisha; 2 wenyewe ndio sheria yao, 2 na huinua heshima yao wenyewe. 1
8Farasi wao ni wepesi kuliko chui, 2 na wakali kuliko mbwa mwitu wakati wa machweo. 1 Askari wapanda farasi wao huenda mbio; 2 waendesha farasi wao wanatoka mbali. 1 Wanaruka kasi kama tai ili kurarua; 2
9wote wanakuja tayari kwa fujo. 1 Makundi yao ya wajeuri yanasonga mbele 2 kama upepo wa jangwani, 1 na kukusanya wafungwa 2 kama mchanga. 1
10Wanawabeza wafalme, 2 na kuwadhihaki watawala. 1 Wanaicheka miji yote iliyozungushiwa maboma; 1 wanafanya malundo ya udongo na kuiteka hiyo miji. 1
11Kisha wanapita kasi kama upepo na kusonga mbele: 2 watu wenye hatia, ambao nguvu zao ndio mungu wao.” 1 Lalamiko La Pili La Habakuki 1
12Ee Bwana, je, wewe sio wa tangu milele? 2 Mungu wangu, Uliye Mtakatifu wangu, hatutakufa. 1 Ee Bwana, umewachagua wao ili watekeleze hukumu; 2 Ee Mwamba, umewaamuru watuadhibu. 1
13Macho yako ni safi mno hata yasiweze kuutazama uovu, 2 wala huwezi kuvumilia makosa. 1 Kwa nini basi unawavumilia wadanganyifu? 2 Kwa nini unakuwa kimya wakati waovu 1 wanawameza wale wenye haki 2 kuliko wao wenyewe? 1
14Umewafanya watu kama samaki baharini, 2 kama viumbe wa bahari wasio na mtawala. 1
15Adui mwovu anawavuta wote kwa ndoana, 2 anawakamata katika wavu wake, 1 anawakusanya katika juya lake; 2 kwa hiyo anashangilia na anafurahi. 1
16Kwa hiyo anatoa kafara kwa wavu wake, 2 na kuchoma uvumba kwa juya lake, 1 kwa kuwa kwa wavu wake anaishi kwa starehe, 2 na anafurahia chakula kizuri. 1
17Je, aendelee kuwatoa walio katika wavu wake, 2 akiangamiza mataifa bila huruma?