Habakkuk · Biblia (Kiswahili)

Habakkuk 3

1Sala ya nabii Habakuki iliyoimbwa kwa shigionothi. + 3:1 Ni kifaa cha uimbaji chenye nyuzi; pia maombi kutumia kifaa hiki. 1

2Bwana, nimezisikia sifa zako; 2 nami naogopa kwa matendo yako, Ee Bwana. 1 Fufua kazi yako katikati ya miaka, 2 katikati ya miaka tangaza habari yako; 2 katika ghadhabu kumbuka rehema. 1

3Mungu alitoka Temani, 2 yeye Aliye Mtakatifu kutoka Mlima Parani. 1 Utukufu wake ulifunika mbingu, 2 na sifa zake zikaifunika dunia. 1

4Mngʼao wake ulikuwa kama jua lichomozalo; 2 mionzi ilimulika kutoka mkononi mwake, 2 ambako nguvu zake zilifichwa. 1

5Tauni ilimtangulia; 2 maradhi ya kuambukiza yalifuata nyayo zake. 1

6Alisimama, akaitikisa dunia; 2 alitazama, na kuyafanya mataifa yatetemeke. 1 Milima ya zamani iligeuka mavumbi 2 na vilima vilivyozeeka vikaanguka. 2 Njia zake ni za milele. 1

7Niliona watu wa Kushani katika dhiki, 2 na makazi ya Midiani katika maumivu makali. 1

8Ee Bwana, uliikasirikia mito? 2 Je, ghadhabu yako ilikuwa dhidi ya vijito? 1 Je, ulighadhibikia bahari 2 ulipoendesha farasi wako 2 na magari yako ya ushindi? 1

9Uliufunua upinde wako 2 na kuita mishale mingi. 1 Uliigawa dunia kwa mito; 2

10milima ilikuona ikatetemeka. 1 Mafuriko ya maji yakapita huko; 2 vilindi vilinguruma 2 na kuinua mawimbi yake juu. 1

11Jua na mwezi vilisimama kimya mbinguni 2 katika mngʼao wa mishale yako inayoruka, 2 na katika mngʼao wa mkuki wako umeremetao. 1

12Kwa ghadhabu ulipita juu ya dunia, 2 na katika hasira ulikanyaga mataifa. 1

13Ulikuja kuwaokoa watu wako, 2 kumwokoa uliyemtia mafuta. 1 Ulimponda kiongozi wa nchi ya uovu, 2 ukamvua toka kichwani hadi wayo. 1

14Kwa mkuki wake mwenyewe ulitoboa kichwa chake 2 wakati mashujaa wake walifurika nje kwa kishindo kututawanya, 1 wakifurahi kama walio karibu kutafuna 2 wale wanyonge waliokuwa mafichoni. 1

15Ulikanyaga bahari kwa farasi wako, 2 ukisukasuka maji makuu. 1

16Nilisikia na moyo wangu ukagonga kwa nguvu, 2 midomo yangu ikatetemeka kwa hofu niliposikia sauti; 1 uchakavu ukanyemelea mifupa yangu, 2 na miguu yangu ikatetemeka. 1 Hata hivyo nitasubiri kwa uvumilivu siku ya maafa 2 kuyajilia mataifa yaliyotuvamia. 1

17Ingawa mtini hauchanui maua 2 na hakuna zabibu juu ya mizabibu, 1 ingawaje mzeituni hauzai, 2 na hata mashamba hayatoi chakula, 1 iwapo hakuna kondoo katika banda, 2 wala ngʼombe katika zizi, 1

18hata hivyo nitashangilia katika Bwana, 2 nitamfurahia Mungu Mwokozi wangu. 1

19Bwana Mwenyezi ni nguvu yangu; 2 huifanya miguu yangu kama miguu ya ayala, 2 huniwezesha kupita juu ya vilima. 1 Kwa kiongozi wa uimbaji. Kwa vinanda vyangu vya nyuzi.

← Habakkuk 2Read In The App, Free →Zephaniah 1 →

Study Habakkuk 3

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123