Hosea · Biblia (Kiswahili)

Hosea 14

1Rudi, ee Israeli, kwa Bwana Mungu wako. 2 Dhambi zako zimekuwa 2 ndilo anguko lako! 1

2Chukueni maneno pamoja nanyi, 2 mkamrudie Bwana. 1 Mwambieni: 2 “Samehe dhambi zetu zote 1 na utupokee kwa neema, 2 ili tuweze kutoa matunda yetu 2 kama sadaka za mafahali. 1

3Ashuru hawezi kutuokoa, 2 hatutapanda farasi wa vita. 1 Kamwe hatutasema tena ‘Miungu yetu’ 2 kwa kile ambacho mikono yetu wenyewe imetengeneza, 2 kwa kuwa kwako wewe yatima hupata huruma.” 1

4“Nitaponya ukaidi wao 2 na kuwapenda kwa hiari yangu, 2 kwa kuwa hasira yangu imeondoka kwao. 1

5Nitakuwa kama umande kwa Israeli; 2 atachanua kama yungiyungi. 1 Kama mwerezi wa Lebanoni 2 atashusha mizizi yake chini; 1

6matawi yake yatatanda. 1 Fahari yake itakuwa kama mti wa mzeituni, 2 harufu yake nzuri kama mwerezi wa Lebanoni. 1

7Watu wataishi tena kwenye kivuli chake. 2 Atastawi kama nafaka. 1 Atachanua kama mzabibu, 2 nao umaarufu wake utakuwa 2 kama divai itokayo Lebanoni. 1

8Ee Efraimu, nina shughuli gani tena na sanamu? 2 Nitamjibu na kumtunza. 1 Mimi ni kama msunobari wenye majani mabichi; 2 kuzaa kwako matunda kunatoka kwangu.” 1

9Ni nani mwenye hekima? Atayatambua mambo haya. 2 Ni nani mwenye ufahamu? Huyu atayaelewa. 1 Njia za Bwana ni adili; 2 wenye haki huenda katika njia hizo, 2 lakini waasi watajikwaa ndani yake.

← Hosea 13Read In The App, Free →Joel 1 →

Study Hosea 14

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

1234567891011121314