Mathayo 27:24
Basi, Pilato alipotambua kwamba hafanikiwi chochote na kwamba maasi yalikuwa yanaanza, alichukua maji, akanawa mikono mbele ya ule umati wa watu, akasema, “Mimi sina lawama juu ya kifo cha mtu huyu; shauri lenu wenyewe.”
Biblia Takatifu
In The King James Version
In Context
23Pilato akauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Wao wakazidi kupaaza sauti: “Asulubiwe!”
25Watu wote wakasema, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!”
Cross References
Matthew 26:5Lakini wakaamua jambo hilo lisifanyike wakati wa sikukuu, kusije kukatokea ghasia kati ya watu.
Matthew 27:9Hivyo maneno ya nabii Yeremia yakatimia: “Walizichukua sarafu thelathini za fedha, thamani ya yule ambaye watu wa Israeli walipanga bei,
Matthew 27:54Basi, jemadari na wale waliokuwa wakimlinda Yesu walipoona tetemeko la ardhi na yale mambo yaliyotukia, wakaogopa sana, wakasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”
John 19:4Pilato akatoka tena nje, akawaambia, “Tazameni, namleta nje kwenu, mpate kujua kwamba mimi sikuona hatia yoyote kwake.”