Nahum · Biblia (Kiswahili)

Nahum 2

1Mshambuliaji anasogea dhidi yako, Ninawi. 2 Linda ngome, 2 chunga barabara, 2 jitieni nguvu wenyewe, 2 kusanya nguvu zako zote! 1

2Bwana atarudisha fahari ya Yakobo, 2 kama fahari ya Israeli, 1 ingawa waangamizi wamewaacha ukiwa 2 na wameharibu mizabibu yao. 1

3Ngao za askari wake ni nyekundu, 2 mashujaa wamevaa nguo nyekundu. 1 Chuma kwenye magari ya vita chametameta, 2 katika siku aliyoyaweka tayari, 2 mikuki ya mierezi inametameta. 1

4Magari ya vita yanafanya msukosuko barabarani, 2 yakikimbia nyuma na mbele uwanjani. 1 Yanaonekana kama mienge ya moto; 2 yanakwenda kasi kama umeme. 1

5Anaita vikosi vilivyochaguliwa, 2 lakini bado wanajikwaa njiani. 1 Wanakimbilia haraka kwenye ukuta wa mji, 2 ile ngao ya kuwakinga imetayarishwa. 1

6Malango ya mto yamefunguliwa wazi, 2 na jumba la kifalme limeanguka. 1

7Imeagizwa kwamba mji uchukuliwe 2 na upelekwe uhamishoni. 1 Vijakazi wake wanaomboleza kama hua 2 na kupigapiga vifua vyao. 1

8Ninawi ni kama dimbwi, 2 nayo maji yake yanakauka. 1 Wanalia, “Simama! Simama!” 2 Lakini hakuna anayegeuka nyuma. 1

9Chukueni nyara za fedha! 2 Chukueni nyara za dhahabu! 1 Wingi wake hauna mwisho, 2 utajiri kutoka hazina zake zote! 1

10Ameharibiwa, ametekwa nyara, ameachwa uchi! 2 Mioyo inayeyuka, magoti yanalegea, 1 miili inatetemeka, 2 na kila uso umebadilika rangi. 1

11Liko wapi sasa pango la simba, 2 mahali ambapo waliwalisha watoto wao, 1 ambapo simba dume na simba jike walikwenda 2 na ambapo wana simba walikwenda 2 bila kuogopa chochote? 1

12Simba aliua mawindo ya kutosha watoto wake, 2 alinyonga mawindo kwa ajili ya mwenzi wake, 1 akijaza makao yake kwa alivyoua 2 na mapango yake kwa mawindo. 1

13Bwana Mwenye Nguvu Zote anatangaza, 2 “Mimi ni kinyume na ninyi. 1 Magari yenu ya vita nitayateketeza kwa moto, 2 na upanga utakula wana simba wako. 2 Sitawaachia mawindo juu ya nchi. 1 Sauti za wajumbe wako 2 hazitasikika tena.”

← Nahum 1Read In The App, Free →Nahum 3 →

Study Nahum 2

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123