Nahum · Biblia (Kiswahili)

Nahum 1

1Neno alilosema Mungu kuhusu Ninawi. Kitabu cha maono cha Nahumu, Mwelkoshi. 1 Hasira Ya Mungu Dhidi Ya Ninawi 1

2Bwana ni mwenye wivu na Mungu mlipiza kisasi; 2 Bwana hulipiza kisasi na amejaa ghadhabu. 1 Bwana hulipiza kisasi juu ya watesi wake, 2 naye anadumisha ghadhabu yake dhidi ya adui zake. 1

3Bwana si mwepesi wa hasira naye ni mwenye nguvu, 2 Bwana hataacha kuadhibu wenye hatia. 1 Njia yake ipo katika kisulisuli na tufani, 2 na mawingu ni vumbi la miguu yake. 1

4Anakemea bahari na kuikausha, 2 anafanya mito yote kukauka. 1 Bashani na Karmeli zinanyauka 2 na maua ya Lebanoni hukauka. 1

5Milima hutikisika mbele yake 2 na vilima huyeyuka. 1 Nchi hutetemeka mbele yake, 2 dunia na wote waishio ndani yake. 1

6Ni nani awezaye kuzuia hasira yake yenye uchungu? 2 Nani awezaye kuvumilia hasira yake kali? 1 Ghadhabu yake imemiminwa kama moto, 2 na miamba inapasuka mbele zake. 1

7Bwana ni Mwema, 2 kimbilio wakati wa taabu. 1 Huwatunza wale wanaomtegemea, 2

8lakini kwa mafuriko makubwa, 1 ataangamiza Ninawi; 2 atafuatilia adui zake hadi gizani. 1

9Shauri baya lolote wapangalo dhidi ya Bwana 2 yeye atalikomesha; 2 taabu haitatokea mara ya pili. 1

10Watasongwa katikati ya miiba 2 na kulewa kwa mvinyo wao. 2 Watateketezwa kama mabua makavu. 1

11Ee Ninawi, kutoka kwako amejitokeza mmoja, 2 ambaye anapanga shauri baya 1 dhidi ya Bwana 2 na kushauri uovu.

12Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Ingawa wana muungano nao ni wengi sana, 2 watakatiliwa mbali na kuangamia. 1 Ingawa nimekutesa wewe, ee Yuda, 2 sitakutesa tena. 1

13Sasa nitavunja nira zao kutoka shingo yako, 2 nami nitazivunjilia mbali pingu zako.” 1

14Hii ndiyo amri Bwana aliyoitoa kukuhusu wewe, Ninawi: 2 “Hutakuwa na wazao 2 watakaoendeleza jina lako. 1 Nitaharibu sanamu za kuchonga na sanamu za kuyeyusha 2 ambazo zipo katika hekalu la miungu yenu. 1 Nitaandaa kaburi lako, 2 kwa maana wewe ni mwovu kabisa.” 1

15Tazama, huko juu milimani, 2 miguu ya huyo mmoja aletaye habari njema, 2 ambaye anatangaza amani! 1 Ee Yuda, sherehekea sikukuu zako, 2 nawe utimize nadhiri zako. 1 Waovu hawatakuvamia tena; 2 wataangamizwa kabisa.

← Micah 7Read In The App, Free →Nahum 2 →

Study Nahum 1

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123