Nahum · Biblia (Kiswahili)

Nahum 3

1Ole wa mji umwagao damu, 2 uliojaa uongo, 1 umejaa nyara, 2 usiokosa kuwa na vitu vya kuteka nyara. 1

2Kelele za mijeledi, 2 vishindo vya magurudumu, 1 farasi waendao mbio 2 na mshtuo wa magari ya vita! 1

3Wapanda farasi wanaenda mbio, 2 panga zinameremeta, 2 na mikuki inangʼaa! 1 Majeruhi wengi, 2 malundo ya maiti, 1 idadi kubwa ya miili isiyohesabika, 2 watu wanajikwaa juu ya mizoga: 1

4yote haya kwa sababu ya wingi wa tamaa za kahaba, 2 anayeshawishi, bibi wa mambo ya uchawi, 1 anayewatia utumwani mataifa kwa ukahaba wake 2 na pia jamaa za watu kwa ulozi wake. 1

5Bwana Mwenye Nguvu Zote anasema, 2 “Mimi ni kinyume na ninyi. 2 Nitafunika uso wako kwa gauni lako. 1 Nitaonyesha mataifa uchi wako 2 na falme aibu yako. 1

6Nitakutupia uchafu, 2 nitakufanyia dharau 2 na kukufanya kioja. 1

7Wote wanaokuona watakukimbia na kusema, 2 ‘Ninawi ipo katika kuangamia: 1 ni nani atakayeomboleza kwa ajili yake?’ 2 Nitampata wapi yeyote wa kukufariji?” 1

8Je, wewe ni bora kuliko No-Amoni, 2 uliopo katika Mto Naili, 2 uliozungukwa na maji? 1 Mto ulikuwa kinga yake, 2 nayo maji yalikuwa ukuta wake. 1

9Kushi + 3:9 Kushi ni Ethiopia. na Misri walikuwa nguvu zake zisizo na mpaka; 2 Putu na Libia walikuwa miongoni mwa wale walioungana naye. 1

10Hata hivyo alichukuliwa mateka 2 na kwenda uhamishoni. 1 Watoto wake wachanga walivunjwa vunjwa vipande 2 kwenye mwanzo wa kila barabara. 1 Kura zilipigwa kwa watu wake wenye heshima, 2 na watu wake wote wakuu walifungwa kwa minyororo. 1

11Wewe pia utalewa; 2 utakwenda mafichoni 2 na kutafuta kimbilio kutoka kwa adui. 1

12Ngome zako zote ni kama mitini 2 yenye matunda yake ya kwanza yaliyoiva; 1 wakati inapotikiswa, 2 tini huanguka kwenye kinywa chake alaye. 1

13Tazama vikosi vyako: 2 wote ni wanawake! 1 Malango ya nchi yako 2 yamekuwa wazi kwa adui zako; 2 moto umeteketeza mapingo yake. 1

14Teka maji kwa ajili ya kuzingirwa kwako, 2 imarisha ulinzi wako, 1 Ufanyie udongo wa mfinyanzi kazi, 2 yakanyage matope, 2 karabati tanuru la kuchomea matofali! 1

15Huko moto utakuteketeza, 2 huko upanga utakuangusha chini 2 na kama vile panzi, watakumaliza. 1 Ongezeka kama panzi, 2 ongezeka kama nzige! 1

16Umeongeza idadi ya wafanyabiashara wako 2 mpaka wamekuwa wengi kuliko nyota za angani, 1 lakini kama nzige wanaacha nchi tupu 2 kisha huruka na kwenda zake. 1

17Walinzi wako ni kama nzige, 2 maafisa wako ni kama makundi ya nzige 2 watuao kwenye kuta wakati wa siku ya baridi: 1 lakini wakati jua linapotokea wanaruka kwenda zao, 2 na hakuna ajuaye waendako. 1

18Ee mfalme wa Ashuru, wachungaji wako wanasinzia; 2 wakuu wako wanalala chini mavumbini kupumzika. 1 Watu wako wametawanyika juu ya milima 2 bila kuwa na mtu yeyote wa kuwakusanya. 1

19Hakuna kitu kinachoweza kuponya jeraha lako; 2 jeraha lako ni la kukuua. 1 Kila anayesikia habari zako, 2 hupiga makofi kwa kuanguka kwako, 1 kwa kuwa ni nani ambaye hajaguswa 2 na ukatili wako usio na mwisho?

← Nahum 2Read In The App, Free →Habakkuk 1 →

Study Nahum 3

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123