Zephaniah · Biblia (Kiswahili)

Zephaniah 2

1Kusanyikeni pamoja, kusanyikeni pamoja, 2 enyi taifa lisilo na aibu, 1

2kabla ya wakati ulioamriwa haujafika 2 na siku ile inayopeperusha kama makapi, 1 kabla hasira kali ya Bwana haijaja juu yenu, 2 kabla siku ya ghadhabu ya Bwana 2 haijaja juu yenu. 1

3Mtafuteni Bwana, enyi nyote wanyenyekevu wa nchi, 2 ninyi ambao hufanya lile analoamuru. 1 Tafuteni haki, tafuteni unyenyekevu; 2 labda mtahifadhiwa 2 siku ya hasira ya Bwana. 1 Dhidi Ya Ufilisti 1

4Gaza utaachwa 2 na Ashkeloni utaachwa magofu. 1 Wakati wa adhuhuri Ashdodi utaachwa mtupu 2 na Ekroni utangʼolewa. 1

5Ole wenu ninyi ambao mnaishi kando ya bahari, 2 enyi Wakerethi; 1 neno la Bwana liko dhidi yenu, 2 ee Kanaani, nchi ya Wafilisti. 1 “Mimi nitawaangamiza, 2 na hakuna atakayebaki.” 1

6Nchi kando ya bahari, mahali ambapo wanaishi Wakerethi, 2 patakuwa mahali pa wachungaji 2 na mazizi ya kondoo. 1

7Itakuwa mali ya mabaki ya nyumba ya Yuda, 2 hapo watapata malisho. 1 Wakati wa jioni watajilaza chini 2 katika nyumba za Ashkeloni. 1 Bwana Mungu wao atawatunza, 2 naye atawarudishia wafungwa wao. 1 Dhidi Ya Moabu Na Amoni 1

8“Nimeyasikia matukano ya Moabu 2 nazo dhihaka za Waamoni, 1 ambao waliwatukana watu wangu 2 na kutoa vitisho dhidi ya nchi yao. 1

9Hakika, kama niishivyo,” 2 asema Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 Mungu wa Israeli, 1 “hakika Moabu itakuwa kama Sodoma, 2 Waamoni kama Gomora: 1 mahali pa magugu na mashimo ya chumvi, 2 nchi ya ukiwa milele. 1 Mabaki ya watu wangu watawateka nyara; 2 mabaki ya taifa langu watarithi nchi yao.” 1

10Hiki ndicho watarudishiwa kwa ajili ya kiburi chao, 2 kwa kutukana na kudhihaki 2 watu wa Bwana Mwenye Nguvu Zote. 1

11Bwana atakuwa wa kuhofisha kwao 2 atakapoangamiza miungu yote ya nchi. 1 Mataifa katika kila pwani yatamwabudu, 2 kila moja katika nchi yake. 1 Dhidi Ya Kushi 1

12“Ninyi pia, ee Wakushi, 2 mtauawa kwa upanga wangu.” 1 Dhidi Ya Ashuru 1

13Mungu atanyoosha mkono wake dhidi ya kaskazini 2 na kuangamiza Waashuru, 1 akiiacha Ninawi ukiwa 2 na pakame kama jangwa. 1

14Makundi ya kondoo na ngʼombe yatajilaza pale, 2 viumbe vya kila aina. 1 Bundi wa jangwani na bundi waliao kwa sauti nyembamba 2 wataishi juu ya nguzo zake. 1 Mwangwi wa kuita kwao utapita madirishani, 2 kifusi kitakuwa milangoni, 2 boriti za mierezi zitaachwa wazi. 1

15Huu ndio mji uliotukuka na kuishi kwa furaha 2 wakijisikia salama. 1 Ulisema moyoni mwako, 2 “Mimi ndimi, na wala hapana mwingine ila mimi.” 1 Jinsi gani umekuwa gofu, 2 mahali pa kulala wanyama pori! 1 Wote wanaopita kando yake wanauzomea 2 na kutikisa mkono kwa dharau.

← Zephaniah 1Read In The App, Free →Zephaniah 3 →

Study Zephaniah 2

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123