Zephaniah · Biblia (Kiswahili)

Zephaniah 1

1Neno la Bwana lililomjia Sefania mwana wa Kushi, mwana wa Gedalia, mwana wa Amaria, mwana wa Hezekia, wakati wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda: 1 Onyo La Maangamizi Yanayokuja 1

2Bwana asema, 2 “Nitafagia kila kitu 2 kutoka kwenye uso wa dunia.” 1

3“Nitafagilia mbali watu na wanyama; 2 nitafagilia mbali ndege wa angani 2 na samaki wa baharini. 1 Wafanyao maovu watapata tu kokoto, 2 nami nitamkatilia mbali mwanadamu atoke katika dunia,” 4 asema Bwana. 1 Dhidi Ya Yuda 1

4“Nitaiadhibu Yuda 2 na wote wakaao Yerusalemu. 1 Kutoka mahali hapa nitakatilia mbali 2 kila mabaki ya Baali, 1 majina ya wapagani na makuhani 2 waabuduo sanamu: 1

5wale ambao husujudu juu ya mapaa 2 kuabudu jeshi la vitu vya angani, 1 wale ambao husujudu na kuapa kwa Bwana 2 na ambao pia huapa kwa Malkamu, 1

6wale wanaoacha kumfuata Bwana, 2 wala hawamtafuti Bwana 2 wala kutaka shauri lake. 1

7Nyamazeni mbele za Bwana Mwenyezi, 2 kwa maana siku ya Bwana iko karibu. 1 Bwana ameandaa dhabihu, 2 amewaweka wakfu wale aliowaalika. 1

8Katika siku ya dhabihu ya Bwana 2 nitawaadhibu wakuu 2 na wana wa mfalme 1 na wale wote wanaovaa 2 nguo za kigeni. 1

9Katika siku hiyo nitaadhibu wote ambao 2 hukwepa kukanyaga kizingiti, 1 ambao hujaza hekalu la miungu yao 2 kwa dhuluma na udanganyifu.” 1

10Bwana asema, “Katika siku hiyo 2 kilio kitapanda juu kutoka lango la Samaki, 2 maombolezo kutoka mtaa wa pili, 2 na mshindo mkubwa kutoka vilimani. 1

11Ombolezeni, ninyi mnaoishi katika eneo la sokoni; 2 wafanyabiashara wenu wote wameangamizwa, 1 wote ambao wanafanya biashara ya fedha 2 wataangamizwa. 1

12Wakati huo nitasaka mji wa Yerusalemu kwa taa, 2 na kuwaadhibu wale ambao 2 wanakaa katika hali ya kuridhika, 1 ambao ni kama divai 2 iliyobaki kwenye machicha, 1 ambao hudhani, ‘ Bwana hatafanya lolote, 2 jema au baya.’ 1

13Utajiri wao utatekwa nyara, 2 nyumba zao zitabomolewa. 1 Watajenga nyumba, 2 lakini hawataishi ndani yake; 1 watapanda mizabibu 2 lakini hawatakunywa divai yake. 1 Siku Kubwa Ya Bwana 1

14“Siku kubwa ya Bwana iko karibu: 2 iko karibu na inakuja haraka. 1 Sikilizeni! Kilio katika siku ya Bwana 2 kitakuwa kichungu, 2 hata shujaa atapiga kelele. 1

15Siku ile ni siku ya ghadhabu, 2 siku ya fadhaa na dhiki, 1 siku ya uharibifu na ukiwa, 2 siku ya giza na utusitusi, 2 siku ya mawingu na giza nene, 1

16siku ya tarumbeta na mlio wa vita 2 dhidi ya miji yenye ngome 2 na dhidi ya minara mirefu. 1

17Nitawaletea watu dhiki, 2 nao watatembea kama vipofu, 1 kwa sababu wametenda dhambi 2 dhidi ya Bwana. 1 Damu yao itamwagwa kama vumbi 2 na matumbo yao kama taka. 1

18Fedha yao wala dhahabu yao 2 hazitaweza kuwaokoa 2 katika siku hiyo ya ghadhabu ya Bwana. 1 Katika moto wa wivu wake 2 dunia yote itateketezwa, 1 kwa maana ataleta mwisho 2 wa wote wanaoishi katika dunia ghafula.”

← Habakkuk 3Read In The App, Free →Zephaniah 2 →

Study Zephaniah 1

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123