Zephaniah 3
1Ole mji wa wadhalimu, 2 waasi na waliotiwa unajisi! 1
2Hautii mtu yeyote, 2 haukubali maonyo. 1 Haumtumaini Bwana, 2 haukaribii karibu na Mungu wake. 1
3Maafisa wake ni simba wangurumao, 2 watawala wake ni mbwa mwitu wa jioni, 1 ambao hawabakizi chochote 2 kwa ajili ya asubuhi. 1
4Manabii wake ni wenye kiburi, 2 ni wadanganyifu. 1 Makuhani wake hunajisi patakatifu 2 na kuihalifu sheria. 1
5Bwana aliye ndani yake ni mwenye haki, 2 hafanyi kosa. 1 Asubuhi kwa asubuhi hutoa haki yake, 2 kila kukipambazuka huitimiza, 2 bali mtu dhalimu hana aibu. 1
6“Nimeyafutilia mbali mataifa, 2 ngome zao zimebomolewa. 1 Nimeziacha barabara ukiwa, 2 hakuna anayepita humo. 1 Miji yao imeharibiwa; 2 hakuna mmoja atakayeachwa: 2 hakuna hata mmoja. 1
7Niliuambia huo mji, 2 ‘Hakika utaniogopa na kukubali maonyo!’ 1 Ndipo makao yake hayatafutiliwa mbali, 2 wala adhabu zangu zote hazitakuja juu yake. 1 Lakini walikuwa bado na shauku 2 kutenda kwa upotovu katika yote waliyofanya.” 1
8Bwana anasema, 2 “Kwa hiyo ningojee mimi, 2 siku nitakayosimama kuteka nyara. 1 Nimeamua kukusanya mataifa, 2 kukusanya falme 1 na kumimina ghadhabu yangu juu yao, 2 hasira yangu kali yote. 1 Dunia yote itateketezwa 2 kwa moto wa wivu wa hasira yangu. 1
9“Ndipo nitatakasa midomo ya mataifa, 2 kwamba wote waweze kuliitia jina la Bwana 2 na kumtumikia kwa pamoja. 1
10Kutoka ngʼambo ya mito ya Kushi 2 watu wangu wanaoniabudu, 1 watu wangu waliotawanyika, 2 wataniletea sadaka. 1
11Siku hiyo hutaaibishwa 2 kwa ajili ya makosa yote ulionitendea, 1 kwa sababu nitawaondoa kutoka mji huu 2 wale wote wanaoshangilia 2 katika kiburi chao. 1 Kamwe hutajivuna tena 2 katika kilima changu kitakatifu. 1
12Lakini nitakuachia ndani yako 2 wapole na wanyenyekevu, 2 ambao wanatumaini jina la Bwana. 1
13Mabaki ya Israeli hayatafanya kosa; 2 hawatasema uongo, 1 wala udanganyifu hautakuwa 2 katika vinywa vyao. 1 Watakula na kulala 2 wala hakuna yeyote 2 atakayewaogopesha.” 1
14Imba, ee Binti Sayuni; 2 paza sauti, ee Israeli! 1 Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, 2 ee Binti Yerusalemu! 1
15Bwana amekuondolea adhabu yako, 2 amewarudisha nyuma adui zako. 1 Bwana, Mfalme wa Israeli, yu pamoja nawe; 2 kamwe hutaogopa tena madhara yoyote. 1
16Katika siku hiyo watauambia Yerusalemu, 2 “Usiogope, ee Sayuni; 2 usiiache mikono yako ilegee. 1
17Bwana Mungu wako yu pamoja nawe, 2 yeye ni mwenye nguvu kuokoa. 1 Atakufurahia kwa furaha kubwa, 2 atakutuliza kwa pendo lake, 2 atakufurahia kwa kuimba.” 1
18“Huzuni katika sikukuu zilizoamriwa 2 nitaziondoa kwenu; 2 hizo ni mzigo na fedheha kwenu. 1
19Wakati huo nitawashughulikia 2 wote waliokudhulumu; 1 nitaokoa vilema na kukusanya 2 wale ambao wametawanywa. 1 Nitawapa sifa na heshima 2 katika kila nchi ambayo waliaibishwa. 1
20Wakati huo nitawakusanya; 2 wakati huo nitawaleta nyumbani. 1 Nitawapa sifa na heshima 2 miongoni mwa mataifa yote ya dunia 1 wakati nitakapowarudishia mateka yenu 2 mbele ya macho yenu hasa,” 4 asema Bwana.