Micah · Biblia (Kiswahili)

Micah 7

1Taabu gani hii niliyo nayo! 1 Nimefanana na yule akusanyaye 2 matunda ya kiangazi, 1 aokotaye masazo baada ya kuvunwa 2 shamba la mizabibu; 1 hakuna kishada chenye matunda ya kula, 2 hakuna hata ile tini ya mwanzoni ninayoitamani. 1

2Wanaomcha Mungu wameondolewa kutoka nchi; 2 hakuna mtu mnyofu hata mmoja aliyebaki. 1 Watu wote wanavizia kumwaga damu, 2 kila mmoja anamwinda ndugu yake kwa wavu. 1

3Mikono yote miwili ni hodari katika kufanya ubaya, 2 mtawala anadai zawadi, 1 hakimu anapokea rushwa, 2 wenye nguvu wanaamuru wanachotaka: 2 wote wanafanya shauri baya pamoja. 1

4Aliye mwema kupita wote kati yao 2 ni kama mchongoma, 1 anayeonekana mnyofu zaidi miongoni mwao 2 ni mbaya kuliko uzio wa miiba. 1 Siku ya walinzi wako imewadia, 2 siku atakayokutembelea Mungu. 1 Sasa ni wakati wao 2 wa kuchanganyikiwa. 1

5Usimtumaini jirani; 2 usiweke matumaini kwa rafiki. 1 Hata kwa yule alalaye kifuani mwako 2 uwe mwangalifu kwa maneno yako. 1

6Kwa kuwa mwana humdharau baba yake, 2 naye binti huinuka dhidi ya mama yake, 1 mkwe kuwa kinyume na mama mkwe wake: 2 adui wa mtu ni wale wa nyumbani mwake hasa. 1

7Lakini mimi, namtazama Bwana kwa matumaini, 2 namngoja Mungu Mwokozi wangu; 2 Mungu wangu atanisikia mimi. 1 Israeli Atainuka 1

8Usifurahie msiba wangu, ee adui yangu! 2 Ingawa nimeanguka, nitainuka. 1 Japo ninaketi gizani, 2 Bwana atakuwa nuru yangu. 1

9Kwa sababu nimetenda dhambi dhidi yake, 2 nitabeba ghadhabu ya Bwana, 1 mpaka atakaponitetea shauri langu 2 na kuithibitisha haki yangu. 1 Atanileta nje kwenye mwanga, 2 nami nitaiona haki yake. 1

10Kisha adui yangu ataliona 2 naye atafunikwa na aibu, 1 yule aliyeniambia, 2 “Yu wapi Bwana Mungu wako?” 1 Macho yangu yataona kuanguka kwake, 2 hata sasa atakanyagwa chini ya mguu 2 kama tope barabarani. 1

11Siku ya kujenga kuta zako itawadia, 2 siku ya kupanua mipaka yako. 1

12Siku hiyo watu watakuja kwako 2 kutoka Ashuru na miji ya Misri, 1 hata kutoka Misri hadi Frati 2 na kutoka bahari hadi bahari 2 na kutoka mlima hadi mlima. 1

13Dunia itakuwa ukiwa kwa sababu ya wakazi wake, 2 kwa sababu ya matunda ya matendo yao. 1 Sala Na Sifa 1

14Wachunge watu wako kwa fimbo yako, 2 kundi la urithi wako, 1 ambalo linaishi peke yake msituni, 2 katika nchi ya malisho yenye rutuba. 1 Waache walishe katika Bashani na Gileadi 2 kama ilivyokuwa siku za kale. 1

15“Kama siku zile mlipotoka Misri, 2 nitawaonyesha maajabu yangu.” 1

16Mataifa yataona na kuaibika, 2 waliondolewa nguvu zao zote. 1 Wataweka mikono yao kwenye vinywa vyao 2 na masikio yao yatakuwa na uziwi. 1

17Wataramba mavumbi kama nyoka, 2 kama viumbe vitambaavyo juu ya ardhi. 1 Watatoka nje ya mapango yao wakitetemeka; 2 watamgeukia Bwana Mungu wetu kwa hofu 2 nao watakuogopa. 1

18Ni nani Mungu kama wewe, 2 ambaye anaachilia dhambi 1 na kusamehe makosa 2 ya mabaki ya urithi wake? 1 Wewe huwi na hasira milele, 2 bali unafurahia kuonyesha rehema. 1

19Utatuhurumia tena, 2 utazikanyaga dhambi zetu 2 chini ya nyayo zako, 1 na kutupa maovu yetu yote 2 katika vilindi vya bahari. 1

20Utakuwa wa kweli kwa Yakobo, 2 nawe utamwonyesha Abrahamu rehema, 1 kama ulivyowaahidi kwa kiapo baba zetu 2 siku za kale.

← Micah 6Read In The App, Free →Nahum 1 →

Study Micah 7

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

1234567