Jeremiah 10
1Sikieni lile ambalo Bwana, anena nanyi ee nyumba ya Israeli.
2Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Usijifunze njia za mataifa 2 wala usitishwe na ishara katika anga, 2 ingawa mataifa yanatishwa nazo. 1
3Kwa maana desturi za mataifa hazina maana, 2 wanakata mti msituni, 2 na fundi anauchonga kwa patasi. 1
4Wanaparemba kwa fedha na dhahabu, 2 wanakikaza kwa nyundo na misumari ili kisitikisike. 1
5Sanamu zao ni kama sanamu 2 iliyowekwa shambani la matango kutishia ndege 2 nazo haziwezi kuongea; 1 sharti zibebwe 2 sababu haziwezi kutembea. 1 Usiziogope; haziwezi kudhuru, 2 wala kutenda lolote jema.” 1
6Hakuna aliye kama wewe, Ee Bwana; 2 wewe ni mkuu, 2 jina lako ni lenye nguvu katika uweza. 1
7Ni nani ambaye haimpasi kukuheshimu wewe, 2 Ee Mfalme wa mataifa? 2 Hii ni stahili yako. 1 Miongoni mwa watu wote wenye hekima 2 katika mataifa na katika falme zao zote, 2 hakuna aliye kama wewe. 1
8Wote hawana akili, tena ni wapumbavu, 2 wanafundishwa na sanamu za miti zisizofaa lolote. 1
9Huleta fedha iliyofuliwa kutoka Tarshishi 2 na dhahabu kutoka Ufazi. 1 Kile ambacho fundi na sonara wametengeneza 2 huvikwa mavazi ya rangi ya samawi na urujuani: 1 vyote vikiwa vimetengenezwa 2 na mafundi stadi. 1
10Lakini Bwana ni Mungu wa kweli, 2 yeye ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele. 1 Anapokasirika, dunia hutetemeka, 2 mataifa hayawezi kustahimili hasira yake.
11“Waambie hivi: ‘Miungu hii, ambayo haikuumba mbingu na dunia, itaangamia kutoka dunia na kutoka chini ya mbingu.’ ” 1
12Lakini Mungu aliiumba dunia kwa uweza wake, 2 akaweka misingi ya ulimwengu kwa hekima yake, 2 na akazitandaza mbingu kwa ufahamu wake. 1
13Atoapo sauti yake, maji yaliyo katika mbingu hunguruma; 2 huyafanya mawingu yainuke kutoka miisho ya dunia. 1 Hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua, 2 naye huuleta upepo kutoka ghala zake. 1
14Kila mmoja ni mjinga na hana maarifa, 2 kila sonara ameaibishwa na sanamu zake. 1 Vinyago vyake ni vya udanganyifu, 2 havina pumzi ndani yavyo. 1
15Havifai kitu, ni vitu vya kufanyia mzaha tu, 2 hukumu yavyo itakapowadia, vitaangamia. 1
16Yeye aliye Fungu la Yakobo sivyo alivyo, 2 kwani ndiye Muumba wa vitu vyote, 1 pamoja na Israeli, kabila la urithi wake: 2 Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake. 1 Maangamizi Yajayo 1
17Kusanyeni mali na vitu vyenu mwondoke nchi hii, 2 enyi mnaoishi katika hali ya kuzingirwa na jeshi. 1
18Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana: 2 “Wakati huu, nitawatupa nje kwa nguvu 2 wote waishio katika nchi hii; 1 nitawataabisha 2 ili waweze kutekwa.” 1
19Ole wangu mimi kwa ajili ya kuumia kwangu! 2 Jeraha langu ni kubwa! 1 Lakini nilisema, 2 “Kweli hii ni adhabu yangu, 2 nami sharti niistahimili.” 1
20Hema langu limeangamizwa; 2 kamba zake zote zimekatwa. 1 Wana wangu wametekwa na hawapo tena; 2 hakuna hata mmoja aliyebaki wa kusimamisha hema langu 2 wala wa kusimamisha kibanda changu. 1
21Wachungaji hawana akili 2 wala hawamuulizi Bwana, 1 hivyo hawastawi 2 na kundi lao lote la kondoo limetawanyika. 1
22Sikilizeni! Taarifa inakuja: 2 ghasia kubwa kutoka nchi ya kaskazini! 1 Hii itafanya miji ya Yuda ukiwa, 2 makao ya mbweha. 1 Maombi Ya Yeremia 1
23Ninajua, Ee Bwana, kwamba maisha ya mwanadamu si yake mwenyewe; 2 hawezi kuziongoza hatua zake mwenyewe. 1
24Unirudi, Ee Bwana, lakini kwa kipimo cha haki: 2 si katika hasira yako, 2 usije ukaniangamiza. 1
25Umwage ghadhabu yako juu ya mataifa 2 wasiokujua wewe, 2 juu ya mataifa wasioliitia jina lako. 1 Kwa kuwa wamemwangamiza Yakobo; 2 wamemwangamiza kabisa 2 na kuiharibu nchi yake.