Jeremiah 2
1Neno la Bwana lilinijia kusema,
2“Nenda ukahubiri masikioni mwa watu wa Yerusalemu: 1 “ ‘Nakumbuka moyo wako wa uchaji katika ujana wako, 2 jinsi ulivyonipenda kama bibi arusi 1 na kunifuata katika jangwa lile lote, 2 katika nchi isiyopandwa mbegu. 1
3Israeli alikuwa mtakatifu kwa Bwana, 2 kama malimbuko ya kwanza ya mavuno yake; 1 wote waliowaangamiza walihesabiwa kuwa na hatia, 2 nayo maafa yaliwakumba,’ ” 4 asema Bwana. 1
4Sikia neno la Bwana, ee nyumba ya Yakobo, 2 nanyi nyote jamaa za nyumba ya Israeli.
5Hivi ndivyo asemavyo Bwana: 1 “Je, baba zenu waliona kosa gani kwangu, 2 hata wakatangatanga mbali nami hivyo? 1 Walifuata sanamu zisizofaa, 2 nao wenyewe wakawa hawafai. 1
6Hawakuuliza, ‘Yuko wapi Bwana, 2 aliyetupandisha kutoka Misri 1 na kutuongoza kupitia nyika kame, 2 kupitia nchi ya majangwa na mabonde, 1 nchi ya ukame na giza, 2 nchi ambayo hakuna mtu asafiriye ndani yake 2 wala hakuna mtu aishiye humo?’ 1
7Niliwaleta katika nchi yenye wingi wa vitu 2 ili mpate kula matunda yake 2 na utajiri wa mazao yake. 1 Lakini mkaja na kuinajisi nchi yangu, 2 na kuufanya urithi wangu chukizo. 1
8Makuhani hawakuuliza, 2 ‘Yuko wapi Bwana?’ 1 Wale wanaoshughulikia sheria hawakunijua mimi; 2 viongozi waliasi dhidi yangu. 1 Manabii walitabiri kwa jina la Baali, 2 wakifuata sanamu zisizofaa. 1
9“Kwa hiyo naleta tena mashtaka dhidi yako,” 4 asema Bwana. 2 “Nami nitaleta mashtaka dhidi ya watoto wa watoto wako. 1
10Vuka, nenda ngʼambo mpaka pwani ya Kitimu + 2:10 Kitimu hapa ni Kipro, kisiwa katika Bahari ya Mediterania. nawe uangalie, 2 tuma watu waende Kedari, wachunguze kwa makini, 2 uone kama kumekuwepo kitu kama hiki. 1
11Je, taifa limebadili miungu yake wakati wowote? 2 (Hata ingawa hao si miungu kamwe.) 1 Lakini watu wangu wamebadili Utukufu wao 2 kwa sanamu zisizofaa kitu. 1
12Shangaeni katika hili, ee mbingu, 2 nanyi tetemekeni kwa hofu kuu,” 4 asema Bwana. 1
13“Watu wangu wametenda dhambi mbili: 2 Wameniacha mimi, 2 niliye chemchemi ya maji yaliyo hai, 1 nao wamejichimbia visima vyao wenyewe, 2 visima vilivyobomoka, visivyoweza kuhifadhi maji. 1
14Je, Israeli ni mtumishi, yaani mtumwa kwa kuzaliwa? 2 Kwa nini basi amekuwa mateka? 1
15Simba wamenguruma; 2 wamemngurumia. 1 Wameifanya nchi yake kuwa ukiwa; 2 miji yake imeteketezwa, nayo imeachwa haina watu. 1
16Pia watu wa Memfisi + 2:16 Memfisi kwa Kiebrania ni Nofu. na Tahpanhesi + 2:16 Tahpanhesi ni mji katika nchi ya Misri. 2 wamevunja taji ya kichwa chako. 1
17Je, hukujiletea hili wewe mwenyewe 2 kwa kumwacha Bwana, Mungu wako 2 alipowaongoza njiani? 1
18Sasa kwa nini uende Misri 2 kunywa maji ya Shihori? + 2:18 Kijito kinachoelekeza maji katika Mto Naili. 1 Nawe kwa nini kwenda Ashuru 2 kunywa maji ya Mto Frati? 1
19Uovu wako utakuadhibu; 2 kurudi nyuma kwako kutakukemea. 1 Basi kumbuka, utambue 2 jinsi lilivyo ovu na chungu kwako 1 unapomwacha Bwana Mungu wako 2 na kutokuwa na hofu yangu,” 4 asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote. 1
20“Zamani nilivunja nira yako 2 na kukatilia mbali vifungo vyako; 2 ukasema, ‘Sitakutumikia!’ 1 Naam kweli, kwenye kila kilima kirefu 2 na chini ya kila mti uliotanda matawi yake 2 ulijilaza kama kahaba. 1
21Nilikupanda ukiwa mzabibu ulio bora sana, 2 mkamilifu na wa mbegu nzuri. 1 Ilikuwaje basi ukawa kinyume nami, 2 ukaharibika na kuwa mzabibu mwitu? 1
22Hata ujisafishe kwa magadi 2 na kutumia sabuni nyingi, 2 bado doa la hatia yako liko mbele zangu,” 4 asema Bwana Mwenyezi. 1
23“Wawezaje kusema, ‘Mimi si najisi, 2 sijawafuata Mabaali’? 1 Kumbuka jinsi ulivyotenda kule bondeni; 2 fikiri uliyoyafanya. 1 Wewe ni ngamia jike mwenye mbio 2 ukikimbia hapa na pale, 1
24punda-mwitu aliyezoea jangwa, 2 anayenusa upepo katika tamaa yake kubwa: 1 katika wakati wake wa kuhitaji mbegu 2 ni nani awezaye kumzuia? 1 Madume yoyote yanayomfuatilia 2 hayana haja ya kujichosha; 2 wakati wa kupandwa kwake watampata tu. 1
25Usikimbie hadi miguu yako iwe haina viatu, 2 na koo lako liwe limekauka. 1 Lakini ulisema, ‘Haina maana! 2 Ninaipenda miungu ya kigeni, 2 nami lazima niifuatie.’ 1
26“Kama vile mwizi aaibikavyo wakati amekamatwa, 2 hivyo ndivyo nyumba ya Israeli inavyoaibishwa: 1 wao wenyewe, wafalme wao na maafisa wao, 2 makuhani wao na manabii wao. 1
27Wanaiambia miti, ‘Wewe ndiwe baba yangu,’ 2 nalo jiwe, ‘Wewe ndiwe uliyenizaa.’ 1 Wamenipa visogo vyao 2 wala hawakunigeuzia nyuso zao; 1 lakini wakiwa katika taabu, wanasema, 2 ‘Njoo utuokoe!’ 1
28Iko wapi basi ile miungu mliyojitengenezea? 2 Yenyewe na ije kama inaweza kuwaokoa 2 wakati mko katika taabu! 1 Kwa maana mna miungu mingi 2 kama mlivyo na miji, ee Yuda. 1
29“Kwa nini mnaleta mashtaka dhidi yangu? 2 Ninyi nyote mmeniasi,” 4 asema Bwana. 1
30“Nimeadhibu watu wako bure tu, 2 hawakujirekebisha. 1 Upanga wako umewala manabii wako 2 kama simba mwenye njaa.
31“Enyi wa kizazi hiki, tafakarini neno la Bwana: 1 “Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli 2 au nchi ya giza kuu? 1 Kwa nini watu wangu wanasema, ‘Sisi tuko huru kuzurura, 2 hatutarudi kwako tena’? 1
32Je, mwanamwali husahau vito vyake, 2 au bibi arusi mapambo yake ya arusi? 1 Lakini watu wangu wamenisahau mimi, 2 tena kwa siku zisizo na hesabu. 1
33Je, wewe una ustadi kiasi gani katika kufuatia mapenzi! 2 Hata wale wanawake wabaya kuliko wote 2 wanaweza kujifunza kutokana na njia zako. 1
34Katika nguo zako watu huona 2 damu ya uhai ya maskini wasio na hatia, 2 ingawa hukuwakamata wakivunja nyumba. 1 Lakini katika haya yote 2
35unasema, ‘Sina hatia; 2 Mungu hajanikasirikia.’ 1 Lakini nitakuhukumu kwa sababu unasema, 2 ‘Mimi sijatenda dhambi.’ 1
36Kwa nini unatangatanga sana, 2 kubadili njia zako? 1 Utakatishwa tamaa na Misri 2 kama ulivyokatishwa na Ashuru. 1
37Pia utaondoka mahali hapo 2 ukiwa umeweka mikono kichwani, 1 kwa kuwa Bwana amewakataa wale unaowatumainia; 2 hutasaidiwa nao.