Jeremiah · Biblia (Kiswahili)

Jeremiah 47

1Hili ndilo neno la Bwana lililomjia nabii Yeremia kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajaishambulia Gaza:

2Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Tazama jinsi maji yanavyoinuka huko kaskazini, 2 yatakuwa mafuriko yenye nguvu sana. 1 Yataifurikia nchi na vitu vyote vilivyomo ndani yake, 2 miji na wale waishio ndani yake. 1 Watu watapiga kelele; 2 wote waishio katika nchi wataomboleza 1

3kwa sauti ya kwato za farasi waendao mbio, 2 kwa sauti ya magari ya adui 2 na mngurumo wa magurudumu yake. 1 Baba hawatageuka kuwasaidia watoto wao, 2 mikono yao italegea. 1

4Kwa maana siku imewadia 2 kuwaangamiza Wafilisti wote 1 na kuwakatilia mbali walionusurika wote 2 ambao wangeweza kusaidia Tiro na Sidoni. 1 Bwana anakaribia kuwaangamiza Wafilisti, 2 mabaki toka pwani za Kaftori. + 47:4 Kaftori ndio Krete. 1

5Gaza atanyoa kichwa chake katika kuomboleza, 2 Ashkeloni atanyamazishwa. 1 Enyi mabaki kwenye tambarare, 2 mtajikatakata wenyewe mpaka lini? 1

6“Mnalia, ‘Aa, upanga wa Bwana, 2 utaendelea mpaka lini ndipo upumzike? 1 Rudi ndani ya ala yako; 2 acha na utulie.’ 1

7Lakini upanga utatuliaje 2 wakati Bwana ameuamuru, 1 wakati ameuagiza kuishambulia Ashkeloni 2 pamoja na pwani yake?”

← Jeremiah 46Read In The App, Free →Jeremiah 48 →

Study Jeremiah 47

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345678910111213141516171819202122232425262728293031323334353637383940414243444546474849505152