Jeremiah · Biblia (Kiswahili)

Jeremiah 50

1Hili ndilo neno alilosema Bwana kupitia nabii Yeremia kuhusu Babeli na nchi ya Wakaldayo: 1

2“Tangazeni na mhubiri katikati ya mataifa, 2 twekeni bendera na mkahubiri; 2 msiache kitu chochote, bali semeni, 1 ‘Babeli utatekwa; 2 Beli ataaibishwa, 2 Merodaki atajazwa na hofu kuu. 1 Sanamu zake zitaaibishwa 2 na vinyago vyake vitajazwa hofu kuu.’ 1

3Taifa kutoka kaskazini litamshambulia, 2 na kuifanya nchi yake ukiwa. 1 Hakuna hata mmoja atakayeishi ndani yake, 2 watu na wanyama wataikimbia. 1

4“Katika siku hizo, wakati huo,” 2 asema Bwana, 1 “watu wa Israeli pamoja na watu wa Yuda 2 wataenda wakilia ili kumtafuta Bwana Mungu wao. 1

5Wataiuliza njia iendayo Sayuni 2 na kuelekeza nyuso zao huko. 1 Watakuja na kuambatana na Bwana 2 katika agano la milele 2 ambalo halitasahaulika. 1

6“Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea; 2 wachungaji wao wamewapotosha 1 na kuwasababisha kuzurura 2 juu ya milima. 1 Walitangatanga juu ya mlima na kilima, 2 na kusahau mahali pao wenyewe pa kupumzikia. 1

7Yeyote aliyewakuta aliwala; 2 adui zao walisema, ‘Sisi hatuna hatia, 1 kwa kuwa wao walitenda dhambi dhidi ya Bwana, malisho yao halisi, 2 Bwana, aliye tumaini la baba zao.’ 1

8“Kimbieni kutoka Babeli; 2 ondokeni katika nchi ya Wakaldayo 2 tena kuweni kama mbuzi wale waongozao kundi. 1

9Kwa maana nitaamsha na kuleta dhidi ya Babeli 2 muungano wa mataifa makubwa kutoka nchi ya kaskazini. 1 Watashika nafasi zao dhidi yake, 2 naye kutokea kaskazini atatekwa. 1 Mishale yao itakuwa kama mishale ya mashujaa walio hodari, 2 ambao hawawezi kurudi mikono mitupu. 1

10Kwa hiyo Ukaldayo utatekwa nyara; 2 wote wamtekao nyara watapata za kutosha,” 4 asema Bwana. 1

11“Kwa sababu hushangilia na kufurahi, 2 wewe utekaye urithi wangu, 1 kwa sababu unachezacheza kama mtamba anayepura nafaka, 2 na kulia kama farasi dume, 1

12mama yako ataaibika mno, 2 yeye aliyekuzaa atatahayari. 1 Atakuwa mdogo kuliko mataifa mengine yote, 2 atakuwa nyika, nchi kame na jangwa. 1

13Kwa sababu ya hasira ya Bwana hatakaliwa na mtu, 2 lakini ataachwa ukiwa kabisa. 1 Wote watakaopita Babeli watatiwa hofu na kudhihaki 2 kwa sababu ya majeraha yake yote. 1

14“Shikeni nafasi zenu kuzunguka Babeli, 2 enyi nyote mvutao upinde. 1 Mpigeni! Msibakize mshale wowote, 2 kwa kuwa ametenda dhambi dhidi ya Bwana. 1

15Piga kelele dhidi yake kila upande! 2 Anajisalimisha, minara yake inaanguka, 2 kuta zake zimebomoka. 1 Kwa kuwa hiki ni kisasi cha Bwana, 2 mlipizeni kisasi; 2 mtendeeni kama alivyowatendea wengine. 1

16Katilieni mbali mpanzi kutoka Babeli, 2 pamoja na mvunaji na mundu wake akivuna. 1 Kwa sababu ya upanga wa mdhalimu 2 kila mmoja na arejee kwa watu wake mwenyewe, 1 kila mmoja na akimbilie 2 kwenye nchi yake mwenyewe. 1

17“Israeli ni kundi lililotawanyika 2 ambalo simba wamelifukuzia mbali. 1 Wa kwanza kumla alikuwa mfalme wa Ashuru, 2 wa mwisho kuponda mifupa yake 2 alikuwa Nebukadneza mfalme wa Babeli.”

18Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: 1 “Nitamwadhibu mfalme wa Babeli na nchi yake 2 kama nilivyomwadhibu mfalme wa Ashuru. 1

19Lakini nitamrudisha Israeli katika malisho yake mwenyewe 2 naye atalisha huko Karmeli na Bashani; 1 njaa yake itashibishwa 2 juu ya vilima vya Efraimu na Gileadi. 1

20Katika siku hizo, wakati huo,” 2 asema Bwana, 1 “uchunguzi utafanyika kwa ajili ya kosa la Israeli, 2 lakini halitakuwepo, 1 kwa ajili ya dhambi za Yuda, 2 lakini haitapatikana hata moja, 1 kwa kuwa nitawasamehe 2 mabaki nitakaowaacha. 1

21“Shambulieni nchi ya Merathaimu 2 na wale waishio huko Pekodi. 1 Wafuatieni, waueni 2 na kuwaangamiza kabisa,” 4 asema Bwana. 2 “Fanyeni kila kitu nilichowaamuru. 1

22Kelele ya vita iko ndani ya nchi, 2 kelele ya maangamizi makuu! 1

23Tazama jinsi nyundo ya dunia yote 2 ilivyovunjika na kuharibika! 1 Tazama jinsi Babeli ilivyokuwa ukiwa 2 miongoni mwa mataifa! 1

24Nimetega mtego kwa ajili yako, ee Babeli, 2 nawe ukakamatwa kabla haujafahamu; 1 ulipatikana na ukakamatwa 2 kwa sababu ulimpinga Bwana. 1

25Bwana amefungua ghala lake la silaha 2 na kuzitoa silaha za ghadhabu yake, 1 kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mwenye Nguvu Zote 2 anayo kazi ya kufanya 2 katika nchi ya Wakaldayo. 1

26Njooni dhidi yake kutoka mbali. 2 Zifungueni ghala zake za nafaka; 2 mlundikeni kama lundo la nafaka. 1 Mwangamizeni kabisa 2 na msimwachie mabaki yoyote. 1

27Waueni mafahali wake wachanga wote; 2 waacheni washuke machinjoni! 1 Ole wao! Kwa kuwa siku yao imewadia, 2 wakati wao wa kuadhibiwa. 1

28Wasikilizeni watoro na wakimbizi kutoka Babeli 2 wakitangaza katika Sayuni 1 jinsi Bwana, Mungu wetu alivyolipiza kisasi, 2 kisasi kwa ajili ya Hekalu lake. 1

29“Waiteni wapiga mishale dhidi ya Babeli, 2 wote wale wavutao upinde. 1 Pigeni kambi kumzunguka kabisa, 2 asitoroke mtu yeyote. 1 Mlipizeni kwa matendo yake; 2 mtendeeni kama alivyotenda. 1 Kwa kuwa alimdharau Bwana, 2 yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. 1

30Kwa hiyo, vijana wake wanaume wataanguka barabarani; 2 askari wake wote watanyamazishwa siku ile,” 4 asema Bwana. 1

31“Tazama, niko kinyume nawe, ewe mwenye majivuno,” 2 asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, 1 “kwa kuwa siku yako imewadia, 2 yaani, wakati wako wa kuadhibiwa. 1

32Mwenye majivuno atajikwaa na kuanguka, 2 wala hakuna yeyote atakayemuinua; 1 nitawasha moto katika miji yake, 2 utakaowateketeza wote wanaomzunguka.”

33Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: 1 “Watu wa Israeli wameonewa, 2 nao watu wa Yuda pia. 1 Wote waliowateka wamewashikilia sana, 2 wanakataa kuwaachia waende. 1

34Lakini Mkombozi wao ana nguvu; 2 Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake. 1 Atatetea kwa nguvu shauri lao 2 ili alete raha katika nchi yao, 1 lakini ataleta msukosuko 2 kwa wale waishio Babeli. 1

35“Upanga dhidi ya Wakaldayo!” 2 asema Bwana, 1 “dhidi ya wale waishio Babeli 2 na dhidi ya maafisa wake na watu wenye busara! 1

36Upanga dhidi ya manabii wake wa uongo! 2 Watakuwa wapumbavu. 1 Upanga dhidi ya mashujaa wake! 2 Watajazwa na hofu kuu 1

37Upanga dhidi ya farasi na magari yake ya vita 2 pamoja na askari wake wote wa kigeni katika safu zake! 2 Wao watakuwa kama wanawake. 1 Upanga dhidi ya hazina zake! 2 Hizo zitatekwa nyara. 1

38Ukame juu ya maji yake! 2 Nayo yatakauka. 1 Kwa kuwa ni nchi ya sanamu, 2 wao wanaenda wazimu kwa ajili ya sanamu. 1

39“Kwa hiyo, viumbe vya jangwani na fisi wataishi humo, 2 nao bundi watakaa humo. 1 Kamwe haitakaliwa tena 2 wala watu hawataishi humo kutoka kizazi hadi kizazi. 1

40Kama vile Mungu alivyoangamiza Sodoma na Gomora 2 pamoja na miji iliyokuwa jirani nayo,” 4 asema Bwana, 1 “vivyo hivyo hakuna mtu yeyote 2 atakayeishi humo. 1 Naam, hakuna mtu yeyote 2 atakayekaa humo. 1

41“Tazama! Jeshi linakuja kutoka kaskazini; 2 taifa kubwa na wafalme wengi 2 wanaamshwa kutoka miisho ya dunia. 1

42Wamejifunga pinde na mikuki; 2 ni wakatili na wasio na huruma. 1 Wanatoa sauti kama bahari inayonguruma 2 wanapoendesha farasi zao; 1 wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita 2 ili kukushambulia, ee Binti Babeli. 1

43Mfalme wa Babeli amesikia habari kuwahusu, 2 nayo mikono yake imelegea. 1 Uchungu umemshika, 2 maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa. 1

44Kama simba anayepanda kutoka vichaka vya Yordani 2 kuja kwenye nchi ya malisho mengi, 1 ndivyo nitamfukuza Babeli kutoka nchi yake ghafula. 2 Ni nani aliye mteule, 2 nitakayemweka kwa ajili ya jambo hili? 1 Ni nani aliye kama mimi, 2 na ni nani awezaye kunipinga? 1 Tena ni mchungaji yupi 2 awezaye kusimama kinyume nami?” 1

45Kwa hiyo, sikia kile Bwana alichokipanga dhidi ya Babeli, 2 kile alichokusudia dhidi ya nchi ya Wakaldayo: 1 Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali. 2 Yeye ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao. 1

46Kwa sauti ya kutekwa kwa Babeli, dunia itatetemeka; 2 kilio chake kitasikika pote miongoni mwa mataifa.

← Jeremiah 49Read In The App, Free →Jeremiah 51 →

Study Jeremiah 50

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345678910111213141516171819202122232425262728293031323334353637383940414243444546474849505152