Jeremiah · Biblia (Kiswahili)

Jeremiah 6

1“Kimbieni kwa usalama wenu, enyi watu wa Benyamini! 2 Kimbieni kutoka Yerusalemu! 1 Pigeni tarumbeta katika Tekoa! 2 Inueni ishara juu ya Beth-Hakeremu! 1 Kwa kuwa maafa yanaonekana yakitoka kaskazini, 2 na uharibifu wa kutisha. 1

2Nitamwangamiza Binti Sayuni, 2 aliye mzuri sana na mwororo. 1

3Wachungaji pamoja na makundi yao 2 watakuja dhidi yake; 1 watapiga mahema yao kumzunguka, 2 kila mmoja akichunga kundi lake mwenyewe.” 1

4“Jiandaeni kwa vita dhidi yake! 2 Inukeni tumshambulie mchana! 1 Lakini, ole wetu, mchana unaisha, 2 na vivuli vya jioni vinazidi kuwa virefu. 1

5Kwa hiyo inukeni, tufanye mashambulizi usiku, 2 na kuharibu ngome zake!”

6Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: 1 “Kateni miti mjenge boma 2 kuzunguka Yerusalemu. 1 Mji huu ni lazima uadhibiwe, 2 umejazwa na uonevu. 1

7Kama vile kisima kinavyomwaga maji yake, 2 ndivyo anavyomwaga uovu wake. 1 Ukatili na maangamizi yasikika ndani yake, 2 ugonjwa wake na majeraha yake viko mbele yangu daima. 1

8Pokea onyo, ee Yerusalemu, 2 la sivyo nitageukia mbali nawe 1 na kuifanya nchi yako kuwa ukiwa, 2 asiweze mtu kuishi ndani yake.”

9Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: 1 “Wao na wayakusanye mabaki ya Israeli 2 kwa uangalifu kama kwenye mzabibu; 1 pitisha mkono wako kwenye matawi tena, 2 kama yeye avunaye zabibu.” 1

10Niseme na nani na kumpa onyo? 2 Ni nani atakayenisikiliza mimi? 1 Masikio yao yameziba, + 6:10 Masikio yameziba kwa Kiebrania ina maana kwamba masikio yao hayajatahiriwa. 2 kwa hiyo hawawezi kusikia. 1 Neno la Bwana ni chukizo kwao, 2 hawalifurahii. 1

11Lakini nimejaa ghadhabu ya Bwana, 2 nami siwezi kuizuia. 1 “Wamwagie watoto walioko barabarani, 2 na juu ya vijana waume waliokusanyika; 1 mume na mke watakumbwa pamoja ndani yake, 2 hata nao wazee waliolemewa na miaka. 1

12Nyumba zao zitapewa watu wengine, 2 pamoja na mashamba yao na wake zao, 1 nitakapounyoosha mkono wangu 2 dhidi ya wale waishio katika nchi,” 4 asema Bwana. 1

13“Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkubwa kabisa, 2 wote wana tamaa ya kupata faida zaidi; 1 manabii na makuhani wanafanana, 2 wote wanafanya udanganyifu. 1

14Wanafunga majeraha ya watu wangu 2 bila uangalifu. 1 Wanasema, ‘Amani, amani,’ 2 wakati hakuna amani. 1

15Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao 2 inayochukiza mno? 1 Hapana, hawana aibu hata kidogo; 2 hawajui hata kuona haya. 1 Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka, 2 watashushwa chini nitakapowaadhibu,” 4 asema Bwana.

16Hivi ndivyo asemavyo Bwana: 1 “Simama kwenye njia panda utazame, 2 ulizia mapito ya zamani, 1 ulizia wapi ilipo njia nzuri, uifuate hiyo, 2 nanyi mtapata raha nafsini mwenu. 2 Lakini ninyi mlisema, ‘Hatutaipita hiyo.’ 1

17Niliweka walinzi juu yenu na kusema, 2 ‘Sikieni sauti ya tarumbeta!’ 2 Lakini mkasema, ‘Hatutasikiliza.’ 1

18Kwa hiyo sikilizeni, enyi mataifa, 2 angalieni, enyi mashahidi, 2 lile litakalowatokea. 1

19Sikia, ee nchi: 1 Ninaleta maafa juu ya watu hawa, 2 matunda ya mipango yao, 1 kwa sababu hawakusikiliza maneno yangu 2 na wameikataa sheria yangu. 1

20Unanifaa nini uvumba kutoka Sheba, 2 au udi wa harufu nzuri kutoka nchi ya mbali? 1 Sadaka zako za kuteketezwa hazikubaliki, 2 dhabihu zako hazinifurahishi mimi.”

21Kwa hiyo hivi ndivyo asemavyo Bwana: 1 “Nitaweka vikwazo mbele ya watu hawa. 2 Baba na wana wao watajikwaa juu yake, 2 majirani na marafiki wataangamia.”

22Hivi ndivyo asemavyo Bwana: 1 “Tazama, jeshi linakuja 2 kutoka nchi ya kaskazini, 1 taifa kubwa linaamshwa 2 kutoka miisho ya dunia. 1

23Wamejifunga pinde na mkuki, 2 ni wakatili na hawana huruma. 1 Wanatoa sauti kama bahari inayonguruma 2 wanapoendesha farasi zao. 1 Wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita 2 ili kukushambulia, ee Binti Sayuni.” 1

24Tumesikia taarifa zao, 2 nayo mikono yetu imelegea. 1 Uchungu umetushika, 2 maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa. 1

25Usitoke kwenda mashambani 2 au kutembea barabarani, 1 kwa kuwa adui ana upanga, 2 na kuna vitisho kila upande. 1

26Enyi watu wangu, vaeni magunia 2 mjivingirishe kwenye majivu, 1 ombolezeni kwa kilio cha uchungu 2 kama amliliaye mwana pekee, 1 kwa maana ghafula 2 mharabu atatujia. 1

27“Nimekufanya wewe kuwa kitu cha kujaribu chuma, 2 nao watu wangu kama mawe yenye madini, 2 ili upate kuzijua na kuzijaribu njia zao. 1

28Wote ni waasi sugu, 2 wakienda huku na huko kusengenya. 1 Wao ni shaba na chuma, 2 wote wanatenda upotovu. 1

29Mivuo inavuma kwa nguvu, 2 kinachoungua kwa huo moto ni risasi, 1 lakini pamoja na kusafisha kote huku ni bure; 2 waovu hawaondolewi. 1

30Wanaitwa fedha iliyokataliwa, 2 kwa sababu Bwana amewakataa.”

← Jeremiah 5Read In The App, Free →Jeremiah 7 →

Study Jeremiah 6

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345678910111213141516171819202122232425262728293031323334353637383940414243444546474849505152