Jeremiah 48
1Kuhusu Moabu: Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: 1 “Ole wake Nebo, kwa maana utaharibiwa. 2 Kiriathaimu utaaibishwa na kutekwa; 2 Misgabu itaaibishwa na kuvunjavunjwa. 1
2Moabu haitasifiwa tena; 2 huko Heshboni watu watafanya shauri baya la anguko lake: 2 ‘Njooni na tuangamize taifa lile.’ 1 Wewe nawe, ee Madmena, utanyamazishwa; 2 upanga utakufuatia. 1
3Sikiliza kilio kutoka Horonaimu, 2 kilio cha maangamizi makuu na uharibifu. 1
4Moabu utavunjwa, 2 wadogo wake watapiga kelele. 1
5Wanapanda kwenda njia ya kuelekea Luhithi, 2 wakilia kwa uchungu wanapotembea, 1 kwenye njia inayoshuka kwenda Horonaimu, 2 kilio cha uchungu kwa ajili ya uharibifu kinasikika. 1
6Kimbieni! Okoeni maisha yenu, 2 kuweni kama kichaka jangwani. 1
7Kwa kuwa mmetumainia matendo yenu na mali zenu, 2 ninyi pia mtachukuliwa mateka, 1 naye Kemoshi + 48:7 Kemoshi alikuwa mungu wa Wamoabu. atakwenda uhamishoni, 2 pamoja na makuhani wake na maafisa wake. 1
8Mharabu atakuja dhidi ya kila mji, 2 wala hakuna mji utakaookoka. 1 Bonde litaangamizwa na uwanda utaharibiwa, 2 kwa sababu Bwana amesema. 1
9Wekeni chumvi kwa ajili ya Moabu, 2 kwa kuwa ataangamizwa; 1 miji yake itakuwa ukiwa, 2 pasipo kuwa na mtu atakayeishi ndani yake. 1
10“Alaaniwe yeye afanyaye kazi ya Bwana kwa hila! 2 Alaaniwe yeye auzuiaye upanga wake usimwage damu! 1
11“Moabu amestarehe tangu ujana wake, 2 kama divai iliyoachwa kwenye machujo yake, 1 haikumiminwa kutoka chombo kimoja hadi kingine, 2 hajaenda uhamishoni. 1 Kwa hiyo ana ladha ile ile kama aliyokuwa nayo, 2 nayo harufu yake haijabadilika. 1
12Lakini siku zinakuja,” 2 asema Bwana, 1 “nitakapotuma watu wamiminao kutoka kwenye magudulia, 2 nao watamimina; 1 wataacha magudulia yake yakiwa matupu 2 na kuvunja mitungi yake. 1
13Kisha Moabu atamwonea aibu mungu wao Kemoshi, 2 kama vile nyumba ya Israeli walivyoona aibu 2 walipotegemea mungu wa Betheli. + 48:13 Betheli ina maana ya Nyumba ya Mungu; lakini pia ni mahali ambapo Mfalme Yeroboamu alisimamisha moja ya sanamu za ndama ili kuabudiwa; nyingine aliiweka huko Dani ( 1Fal 12:29-33 ). 1
14“Mwawezaje kusema, ‘Sisi ni mashujaa, 2 watu jasiri katika vita’? 1
15Moabu ataangamizwa na miji yake itavamiwa, 2 vijana wake waume walio bora sana watachinjwa,” 1 asema Mfalme, ambaye jina lake 2 ni Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote. 1
16“Kuanguka kwa Moabu kumekaribia, 2 janga kubwa litamjia kwa haraka. 1
17Ombolezeni kwa ajili yake, ninyi nyote mnaomzunguka, 2 ninyi nyote mnaojua sifa zake, 1 semeni, ‘Tazama jinsi ilivyovunjika fimbo ya kifalme yenye nguvu, 2 tazama jinsi ilivyovunjika fimbo iliyotukuka!’ 1
18“Shuka kutoka fahari yako 2 na uketi katika ardhi iliyokauka, 2 enyi wenyeji wa Binti wa Diboni, 1 kwa maana yeye aangamizaye Moabu atakuja dhidi yako, 2 na kuangamiza miji yako iliyozungushiwa maboma. 1
19Simama kando ya barabara na utazame, 2 wewe unayeishi Aroeri. 1 Muulize mwanaume anayekimbia 2 na mwanamke anayetoroka, 2 waulize, ‘Kumetokea nini?’ 1
20Moabu amefedheheshwa, kwa kuwa amevunjavunjwa. 2 Lieni kwa huzuni na kupiga kelele! 1 Tangazeni kando ya Arnoni 2 kwamba Moabu ameangamizwa. 1
21Hukumu imefika kwenye uwanda wa juu: 2 katika Holoni, Yahasa na Mefaathi, 1
22katika Diboni, Nebo 2 na Beth-Diblathaimu, 1
23katika Kiriathaimu, Beth-Gamuli 2 na Beth-Meoni, 1
24katika Keriothi na Bosra; 2 kwa miji yote ya Moabu, 2 iliyoko mbali na karibu. 1
25Pembe + 48:25 Pembe hapa ni ishara ya nguvu. ya Moabu imekatwa, 2 mkono wake umevunjwa,” 4 asema Bwana. 1
26“Mlevye, 2 kwa kuwa amemdharau Bwana. 1 Moabu na agaegae katika matapishi yake, 2 yeye na awe kitu cha dhihaka. 1
27Je, Israeli hakuwa kitu chako cha kudhihakiwa? 2 Je, alikamatwa miongoni mwa wezi, 1 kiasi cha kutikisa kichwa chako kwa dharau 2 kila mara unapozungumza juu yake? 1
28Ondokeni kwenye miji yenu, mkaishi katikati ya miamba, 2 enyi mnaoishi Moabu. 1 Kuweni kama huwa ambaye hutengeneza kiota chake 2 kwenye mdomo wa pango. 1
29“Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu: 2 kutakabari kwake kwa kiburi na majivuno, 1 kiburi chake na ufidhuli wake, 2 na kujivuna kwa moyo wake. 1
30Ninaujua ujeuri wake, lakini ni bure,” 4 asema Bwana, 2 “nako kujisifu kwake hakumsaidii chochote. 1
31Kwa hiyo namlilia Moabu, 2 kwa ajili ya Moabu yote ninalia, 1 ninaomboleza kwa ajili 2 ya watu wa Kir-Haresethi. 1
32Ninalia machozi kwa ajili yenu, kama Yazeri aliavyo, 2 enyi mizabibu ya Sibma. 1 Matawi yako yameenea hadi baharini; 2 yamefika hadi bahari ya Yazeri. 1 Mharabu ameyaangukia matunda yako yaliyoiva 2 na mizabibu yako iliyoiva. 1
33Shangwe na furaha vimetoweka 2 kutoka bustani na mashamba ya Moabu. 1 Nimekomesha kutiririka kwa divai kutoka mashinikizo; 2 hakuna hata mmoja ayakanyagaye kwa kelele za shangwe. 1 Ingawa kuna kelele, 2 sio kelele za shangwe. 1
34“Sauti ya kilio chao inapanda 2 kutoka Heshboni hadi Eleale na Yahazi, 1 kutoka Soari hadi Horonaimu na Eglath-Shelishiya, 2 kwa kuwa hata maji ya Nimrimu yamekauka. 1
35Nitakomesha wale wote katika Moabu 2 watoao sadaka mahali pa juu, 2 na kufukiza uvumba kwa miungu yao,” 4 asema Bwana. 1
36“Kwa hiyo moyo wangu unaomboleza kwa ajili ya Moabu kama filimbi; 2 unaomboleza kama filimbi kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi. 2 Utajiri waliojipatia umetoweka. 1
37Kila kichwa kimenyolewa 2 na kila mwenye ndevu zimekatwa; 1 kila mkono umekatwa 2 na kila kiuno kimefunikwa kwa nguo ya gunia. 1
38Juu ya mapaa yote katika Moabu 2 na katika viwanja 1 hakuna kitu chochote isipokuwa maombolezo, 2 kwa kuwa nimemvunja Moabu 2 kama gudulia ambalo hakuna mtu yeyote anayelitaka,” 4 asema Bwana. 1
39“Tazama jinsi alivyovunjikavunjika! 2 Jinsi wanavyolia kwa huzuni! 1 Tazama jinsi Moabu anavyogeuka kwa aibu! 2 Moabu amekuwa kitu cha kudhihakiwa, 1 kitu cha kutisha kwa wale wote 2 wanaomzunguka.”
40Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Tazama! Tai anashuka chini, 2 akitanda mabawa yake juu ya Moabu. 1
41Miji itatekwa na ngome zake 2 zitatwaliwa. 1 Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Moabu 2 itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wa kuzaa. 1
42Moabu ataangamizwa kama taifa 2 kwa sababu amemdharau Bwana. 1
43Hofu kuu, shimo na mtego vinawangojea, 2 enyi watu wa Moabu,” 4 asema Bwana. 1
44“Yeyote atakayeikimbia hiyo hofu kuu 2 ataanguka ndani ya shimo, 1 yeyote atakayepanda kutoka shimoni, 2 atanaswa katika mtego, 1 kwa sababu nitaletea Moabu 2 mwaka wa adhabu yake,” 4 asema Bwana. 1
45“Katika kivuli cha Heshboni, 2 wakimbizi wamesimama pasipo msaada, 1 kwa kuwa moto umezimika huko Heshboni, 2 mwali wa moto kutoka katikati ya Sihoni; 1 unaunguza vipaji vya nyuso za Moabu, 2 mafuvu yao wenye kujivuna kwa kelele. 1
46Ole wako, ee Moabu! 2 Watu wa Kemoshi wameangamizwa; 1 wana wako wamepelekwa uhamishoni 2 na binti zako wamechukuliwa mateka. 1
47“Lakini nitarudisha mateka wa Moabu, 2 katika siku zijazo,” 4 asema Bwana. Huu ndio mwisho wa hukumu juu ya Moabu.