Lamentations 1
1Tazama jinsi mji ulivyoachwa ukiwa, 2 mji ambao zamani ulikuwa umejaa watu! 1 Jinsi ambavyo umekuwa kama mama mjane, 2 ambaye wakati fulani alikuwa maarufu miongoni mwa mataifa! 1 Yule ambaye alikuwa malkia miongoni mwa majimbo 2 sasa amekuwa mtumwa. 1
2Kwa uchungu, hulia sana usiku, 2 machozi yapo kwenye mashavu yake. 1 Miongoni mwa wapenzi wake wote 2 hakuna yeyote wa kumfariji. 1 Rafiki zake wote wamemsaliti, 2 wamekuwa adui zake. 1
3Baada ya mateso na kufanyishwa kazi kikatili, 2 Yuda amekwenda uhamishoni. 1 Anakaa miongoni mwa mataifa, 2 hapati mahali pa kupumzika. 1 Wote ambao wanamsaka wamemkamata 2 katikati ya dhiki yake. 1
4Barabara zielekeazo Sayuni zaomboleza, 2 kwa kuwa hakuna yeyote anayekuja 2 kwenye sikukuu zake zilizoamriwa. 1 Malango yake yote yamekuwa ukiwa, 2 makuhani wake wanalia kwa uchungu, 1 wanawali wake wanahuzunika, 2 naye yuko katika uchungu wa maumivu makuu. 1
5Adui zake wamekuwa mabwana zake, 2 watesi wake wana raha. 1 Bwana amemletea huzuni 2 kwa sababu ya dhambi zake nyingi. 1 Watoto wake wamekwenda uhamishoni, 2 mateka mbele ya adui. 1
6Fahari yote imeondoka 2 kutoka kwa Binti Sayuni. 1 Wakuu wake wako kama ayala 2 ambaye hapati malisho, 1 katika udhaifu wamekimbia 2 mbele ya anayewasaka. 1
7Katika siku za mateso yake na kutangatanga, 2 Yerusalemu hukumbuka hazina zote 2 ambazo zilikuwa zake siku za kale. 1 Wakati watu wake walipoanguka katika mikono ya adui, 2 hapakuwepo na yeyote wa kumsaidia. 1 Watesi wake walimtazama 2 na kumcheka katika maangamizi yake. 1
8Yerusalemu ametenda dhambi sana 2 kwa hiyo amekuwa najisi. 1 Wote waliomheshimu wanamdharau, 2 kwa maana wameuona uchi wake. 1 Yeye mwenyewe anapiga kite 2 na kugeukia mbali. 1
9Uchafu wake umegandamana na nguo zake; 2 hakuwaza juu ya maisha yake ya baadaye. 1 Anguko lake lilikuwa la kushangaza, 2 hapakuwepo na yeyote wa kumfariji. 1 “Tazama, Ee Bwana, teso langu, 2 kwa maana adui ameshinda.” 1
10Adui ametia mikono 2 juu ya hazina zake zote, 1 aliona mataifa ya kipagani 2 wakiingia mahali patakatifu pake, 1 wale uliowakataza kuingia 2 kwenye kusanyiko lako. 1
11Watu wake wote wanalia kwa uchungu 2 watafutapo chakula; 1 wanabadilisha hazina zao kwa chakula 2 ili waweze kuendelea kuishi. 1 “Tazama, Ee Bwana, ufikiri, 2 kwa maana nimedharauliwa.” 1
12“Je, si kitu kwenu, ninyi nyote mpitao kando? 2 Angalieni kote mwone. 1 Je, kuna maumivu kama maumivu yangu 2 yale yaliyotiwa juu yangu, 1 yale Bwana aliyoyaleta juu yangu 2 katika siku ya hasira yake kali? 1
13“Kutoka juu alipeleka moto, 2 akaushusha katika mifupa yangu. 1 Aliitandia wavu miguu yangu 2 na akanirudisha nyuma. 1 Akanifanya mkiwa, 2 na mdhaifu mchana kutwa. 1
14“Dhambi zangu zimefungwa kwenye nira, 2 kwa mikono yake zilifumwa pamoja. 1 Zimefika shingoni mwangu 2 na Bwana ameziondoa nguvu zangu. 1 Amenitia mikononi mwa wale 2 ambao siwezi kushindana nao. 1
15“Bwana amewakataa wapiganaji wa vita 2 wote walio kati yangu, 1 ameagiza jeshi dhidi yangu 2 kuwaponda vijana wangu wa kiume. 1 Katika shinikizo lake la divai Bwana amemkanyaga 2 Bikira Binti Yuda. 1
16“Hii ndiyo sababu ninalia 2 na macho yangu yanafurika machozi. 1 Hakuna yeyote aliye karibu kunifariji, 2 hakuna yeyote wa kuhuisha roho yangu. 1 Watoto wangu ni wakiwa 2 kwa sababu adui ameshinda.” 1
17Sayuni ananyoosha mikono yake, 2 lakini hakuna yeyote wa kumfariji. 1 Bwana ametoa amri kwa ajili ya Yakobo 2 kwamba majirani zake wawe adui zake; 2 Yerusalemu umekuwa 2 kitu najisi miongoni mwao. 1
18“ Bwana ni mwenye haki, 2 hata hivyo niliasi dhidi ya amri yake. 1 Sikilizeni, enyi mataifa yote, 2 tazameni maumivu yangu. 1 Wavulana wangu na wasichana wangu 2 wamekwenda uhamishoni. 1
19“Niliita washirika wangu 2 lakini walinisaliti. 1 Makuhani wangu na wazee wangu 2 waliangamia mjini 1 walipokuwa wakitafuta chakula 2 ili waweze kuishi. 1
20“Angalia, Ee Bwana, jinsi nilivyo katika dhiki! 2 Nina maumivu makali ndani yangu, 1 nami ninahangaika moyoni mwangu, 2 kwa kuwa nimekuwa mwasi sana. 1 Huko nje, upanga unaua watu, 2 ndani, kipo kifo tu. 1
21“Watu wamesikia ninavyolia kwa uchungu, 2 lakini hakuna yeyote wa kunifariji. 1 Adui zangu wote wamesikia juu ya dhiki yangu, 2 wanafurahia lile ulilolitenda. 1 Naomba uilete siku uliyoitangaza 2 ili wawe kama mimi. 1
22“Uovu wao wote na uje mbele zako; 2 uwashughulikie wao 1 kama vile ulivyonishughulikia mimi 2 kwa sababu ya dhambi zangu zote. 1 Kulia kwangu kwa uchungu ni kwingi 2 na moyo wangu umedhoofika.”