Lamentations · Biblia (Kiswahili)

Lamentations 5

1Kumbuka, Ee Bwana, yaliyotupata, 2 tazama, nawe uione aibu yetu. 1

2Urithi wetu umegeuziwa kwa wageni, 2 na nyumba zetu kwa wageni. 1

3Tumekuwa yatima wasio na baba, 2 mama zetu wamekuwa kama wajane. 1

4Ni lazima tununue maji tunayokunywa, 2 kuni zetu zapatikana tu kwa kununua. 1

5Wanaotufuatilia wapo kwenye visigino vyetu, 2 tumechoka na hakuna pumziko. 1

6Tumejitolea kwa Misri na Ashuru 2 tupate chakula cha kutosha. 1

7Baba zetu walitenda dhambi na hawapo tena, 2 na sisi tunachukua adhabu yao. 1

8Watumwa wanatutawala 2 na hakuna wa kutuokoa mikononi yao. 1

9Tunapata chakula chetu kwa kuhatarisha maisha yetu 2 kwa sababu ya upanga jangwani. 1

10Ngozi yetu ina joto kama tanuru, 2 kwa sababu ya fadhaa itokanayo na njaa. 1

11Wanawake wametendwa jeuri katika Sayuni, 2 na mabikira katika miji ya Yuda. 1

12Wakuu wametungikwa juu kwa mikono yao, 2 wazee hawapewi heshima. 1

13Vijana wanataabika kwenye mawe ya kusagia, 2 wavulana wanayumbayumba chini ya mizigo ya kuni. 1

14Wazee wameondoka langoni la mji, 2 vijana wameacha kuimba nyimbo zao. 1

15Furaha imeondoka mioyoni mwetu, 2 kucheza kwetu kumegeuka maombolezo. 1

16Taji imeanguka kutoka kichwani petu. 2 Ole wetu, kwa maana tumetenda dhambi! 1

17Kwa sababu hiyo, mioyo yetu inazimia, 2 kwa sababu ya hayo, macho yetu yamefifia, 1

18kwa ajili ya Mlima Sayuni, ambao unakaa ukiwa, 2 nao mbweha wanatembea juu yake. 1

19Wewe, Ee Bwana unatawala milele, 2 kiti chako cha enzi chadumu kizazi hadi kizazi. 1

20Kwa nini watusahau siku zote? 2 Kwa nini umetuacha kwa muda mrefu? 1

21Turudishe kwako mwenyewe, Ee Bwana, 2 ili tupate kurudi. 2 Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale, 1

22isipokuwa uwe umetukataa kabisa 2 na umetukasirikia pasipo kipimo.

← Lamentations 4Read In The App, Free →Ezekiel 1 →

Study Lamentations 5

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345