Lamentations · Biblia (Kiswahili)

Lamentations 4

1Jinsi dhahabu ilivyopoteza mngʼao wake, 2 dhahabu iliyo safi haingʼai! 1 Vito vya thamani vimetawanywa 2 kwenye mwanzo wa kila barabara. 1

2Wana wa Sayuni wenye thamani, 2 ambao mwanzo uzito wa thamani yao 2 ulikuwa wa dhahabu, 1 sasa wanaangaliwa kama vyungu vya udongo, 2 kazi ya mikono ya mfinyanzi! 1

3Hata mbweha hutoa matiti yao 2 kunyonyesha watoto wao, 1 lakini watu wangu wamekuwa wasio na huruma 2 kama mbuni jangwani. 1

4Kwa sababu ya kiu ulimi wa mtoto mchanga 2 umegandamana na kaakaa la kinywa chake, 1 watoto huomba mkate, 2 lakini hakuna yeyote awapaye. 1

5Wale waliokula vyakula vya kifahari 2 ni maskini barabarani. 1 Wale waliokuzwa wakivaa nguo za zambarau 2 sasa wanalalia majivu. 1

6Adhabu ya watu wangu 2 ni kubwa kuliko ile ya Sodoma, 1 ambayo ilipinduliwa ghafula 2 bila kuwepo mkono wa msaada. 1

7Wakuu wao walikuwa wamengʼaa kuliko theluji 2 na weupe kuliko maziwa, 1 miili yao ilikuwa myekundu kuliko marijani, 2 kuonekana kwao kama yakuti samawi. 1

8Lakini sasa ni weusi kuliko masizi; 2 hawatambulikani barabarani. 1 Ngozi yao imeshikamana juu ya mifupa yao, 2 imekuwa mikavu kama fimbo. 1

9Wale waliouawa kwa upanga ni bora 2 kuliko wale wanaokufa njaa; 1 wanateseka kwa njaa, wanatokomea 2 kwa kukosa chakula kutoka shambani. 1

10Kwa mikono yao wenyewe wanawake wenye huruma 2 wanapika watoto wao wenyewe, 1 waliokuwa chakula chao 2 watu wangu walipoangamizwa. 1

11Bwana ametoa nafasi kamilifu ya ghadhabu yake; 2 ameimwaga hasira yake kali. 1 Amewasha moto katika Sayuni 2 ambao umeteketeza misingi yake. 1

12Wafalme wa dunia hawakuamini, 2 wala mtu yeyote wa duniani, 1 kwamba adui na watesi wangeweza kuingia 2 kwenye malango ya Yerusalemu. 1

13Lakini hili lilitokea kwa sababu ya dhambi za manabii wake, 2 na maovu ya makuhani wake, 1 waliomwaga ndani yake 2 damu ya wenye haki. 1

14Sasa wanapapasa papasa barabarani 2 kama watu ambao ni vipofu. 1 Wamenajisiwa kabisa kwa damu, 2 hata hakuna anayethubutu kugusa mavazi yao. 1

15Watu wanawapigia kelele, “Ondokeni! Ninyi ni najisi! 2 Ondokeni! Ondokeni! Msituguse!” 1 Wanapokimbia na kutangatanga huku na huko, 2 watu miongoni mwa mataifa wanasema, 2 “Hawawezi kukaa hapa zaidi.” 1

16Bwana mwenyewe amewatawanya; 2 hawaangalii tena. 1 Makuhani hawaonyeshwi heshima, 2 wazee hawakubaliki. 1

17Zaidi ya hayo, macho yetu yalichoka, 2 kwa kutazamia bure msaada; 1 tuliangalia kutoka minara yetu 2 kwa taifa lisiloweza kutuokoa. 1

18Watu walituvizia katika kila hatua 2 hata hatukuweza kutembea katika barabara zetu. 1 Mwisho wetu ulikuwa karibu, siku zetu zilikuwa zimetimia, 2 kwa maana mwisho wetu ulikuwa umefika. 1

19Waliotufuatia walikuwa wepesi 2 kuliko tai angani; 2 walitusaka juu milimani 2 na kutuvizia jangwani. 1

20Mpakwa mafuta wa Bwana, pumzi ya uhai wetu hasa, 2 alinaswa katika mitego yao. 1 Tulifikiri kwamba chini ya kivuli chake 2 tungeliweza kuishi miongoni mwa mataifa. 1

21Shangilia na ufurahi, ee Binti Edomu, 2 wewe unayeishi nchi ya Usi. 1 Lakini kwako pia kikombe kitapitishwa, 2 Utalewa na kuvuliwa nguo ubaki uchi. 1

22Ee Binti Sayuni, adhabu yako itaisha, 2 hatarefusha muda wako wa kukaa uhamishoni. 1 Lakini, ee Binti Edomu, ataadhibu dhambi yako, 2 na atafunua uovu wako.

← Lamentations 3Read In The App, Free →Lamentations 5 →

Study Lamentations 4

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345