Lamentations · Biblia (Kiswahili)

Lamentations 3

1Mimi ndiye mtu aliyeona mateso 2 kwa fimbo ya ghadhabu yake. 1

2Amenifukuzia mbali na kunifanya nitembee 2 gizani wala si katika nuru; 1

3hakika, amegeuza mkono wake dhidi yangu 2 tena na tena, mchana kutwa. 1

4Amefanya ngozi yangu na nyama yangu kuchakaa 2 na ameivunja mifupa yangu. 1

5Amenizingira na kunizunguka 2 kwa uchungu na taabu. 1

6Amenifanya niishi gizani 2 kama wale waliokufa. 1

7Amenizungushia ukuta ili nisiweze kutoroka, 2 amenifunga kwa minyororo mizito. 1

8Hata ninapoita au kulia ili kuomba msaada, 2 anakataa kupokea maombi yangu. 1

9Ameizuia njia yangu kwa mapande ya mawe, 2 amepotosha njia zangu. 1

10Kama dubu aviziaye, 2 kama simba mafichoni, 1

11ameniburuta kutoka njia, 2 akanirarua na kuniacha bila msaada. 1

12Amevuta upinde wake 2 na kunifanya mimi niwe lengo 2 kwa ajili ya mishale yake. 1

13Alinichoma moyo wangu kwa mishale 2 iliyotoka kwenye podo lake. 1

14Nimekuwa kichekesho kwa watu wangu wote, 2 wananidhihaki kwa wimbo mchana kutwa. 1

15Amenijaza kwa majani machungu 2 na kunishibisha kwa nyongo. 1

16Amevunja meno yangu kwa changarawe, 2 amenikanyagia mavumbini. 1

17Amani yangu imeondolewa, 2 nimesahau kufanikiwa ni nini. 1

18Kwa hiyo nasema, “Fahari yangu imeondoka 2 na yale yote niliyokuwa nimetarajia kutoka kwa Bwana.” 1

19Nayakumbuka mateso yangu na kutangatanga kwangu, 2 uchungu na nyongo. 1

20Ninayakumbuka vyema, 2 nayo nafsi yangu imezimia ndani yangu. 1

21Hata hivyo najikumbusha neno hili 2 na kwa hiyo ninalo tumaini. 1

22Kwa sababu ya upendo mkuu wa Bwana, hatuangamii, 2 kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe. 1

23Ni mpya kila asubuhi, 2 uaminifu wako ni mkuu. 1

24Nimeiambia nafsi yangu, “ Bwana ni fungu langu, 2 kwa hiyo nitamngojea.” 1

25Bwana ni mwema kwa wale ambao tumaini lao ni kwake, 2 kwa yule ambaye humtafuta; 1

26ni vyema kungojea kwa utulivu 2 kwa ajili ya wokovu wa Bwana. 1

27Ni vyema mtu kuchukua nira 2 bado angali kijana. 1

28Na akae peke yake awe kimya, 2 kwa maana Bwana ameiweka juu yake. 1

29Na azike uso wake mavumbini 2 bado panawezekana kuwa na matumaini. 1

30Na atoe shavu lake kwa yule ampigaye, 2 na ajazwe na aibu. 1

31Kwa kuwa watu hawakatiliwi mbali 2 na Bwana milele. 1

32Ingawa huleta huzuni, ataonyesha huruma, 2 kwa kuwa upendo wake usiokoma ni mkuu. 1

33Kwa maana hapendi kuwaletea mateso 2 au huzuni watoto wa wanadamu. 1

34Kuwaponda chini ya nyayo 2 wafungwa wote katika nchi, 1

35Kumnyima mtu haki zake 2 mbele za Aliye Juu Sana, 1

36kumnyima mtu haki: 2 Je, Bwana asione mambo kama haya? 1

37Nani awezaye kusema nalo likatendeka 2 kama Bwana hajaamuru? 1

38Je, si ni kwenye kinywa cha Aliye Juu Sana 2 ndiko yatokako maafa na mambo mema? 1

39Mwanadamu yeyote aliye hai aweza kulalamika 2 wakati anapoadhibiwa kwa ajili ya dhambi zake? 1

40Tuzichunguze njia zetu na kuzijaribu, 2 na tumrudie Bwana Mungu. 1

41Tuinue mioyo yetu pamoja na mikono yetu 2 kwa Mungu mbinguni, na tuseme: 1

42“Tumetenda dhambi na kuasi 2 nawe hujasamehe. 1

43“Umejifunika mwenyewe kwa hasira na kutufuatilia; 2 umetuchinja bila huruma. 1

44Unajifunika mwenyewe kwa wingu, 2 ili pasiwe na ombi 2 litakaloweza kupenya. 1

45Umetufanya takataka na uchafu 2 miongoni mwa mataifa. 1

46“Adui zetu wote wamefumbua vinywa vyao 2 wazi dhidi yetu. 1

47Tumeteseka kwa hofu kuu na shida ya ghafula, 2 uharibifu na maangamizi.” 1

48Vijito vya machozi vinatiririka kutoka machoni mwangu, 2 kwa sababu watu wangu wameangamizwa. 1

49Macho yangu yatatiririka machozi bila kukoma, 2 bila kupata nafuu, 1

50hadi Bwana atazame chini 2 kutoka mbinguni na kuona. 1

51Lile ninaloliona huniletea huzuni nafsini 2 kwa sababu ya wanawake wote wa mji wangu. 1

52Wale waliokuwa adui zangu bila sababu 2 wameniwinda kama ndege. 1

53Walijaribu kukomesha maisha yangu ndani ya shimo 2 na kunitupia mawe; 1

54maji yalifunika juu ya kichwa changu, 2 nami nikafikiri nilikuwa karibu 2 kukatiliwa mbali. 1

55Nililiitia jina lako, Ee Bwana, 2 kutoka vina vya shimo. 1

56Ulisikia ombi langu: “Usikizibie masikio yako 2 kilio changu nikuombapo msaada.” 1

57Ulikuja karibu nilipokuita, 2 nawe ukasema, “Usiogope.” 1

58Ee Bwana, ulichukua shauri langu, 2 ukaukomboa uhai wangu. 1

59Umeona, Ee Bwana, ubaya niliotendewa. 2 Tetea shauri langu! 1

60Umeona kina cha kisasi chao, 2 mashauri yao yote mabaya dhidi yangu. 1

61Ee Bwana, umesikia matukano yao, 2 mashauri yao yote mabaya dhidi yangu: 1

62kile adui zangu wanachonongʼona na kunungʼunikia 2 dhidi yangu mchana kutwa. 1

63Watazame! Wakiwa wameketi au wamesimama, 2 wananidhihaki katika nyimbo zao. 1

64Uwalipe kile wanachostahili, Ee Bwana, 2 kwa yale ambayo mikono yao imetenda. 1

65Weka pazia juu ya mioyo yao, 2 laana yako na iwe juu yao! 1

66Wafuatilie katika hasira na uwaangamize 2 kutoka chini ya mbingu za Bwana.

← Lamentations 2Read In The App, Free →Lamentations 4 →

Study Lamentations 3

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

12345