Lamentations 2
1Tazama jinsi Bwana alivyomfunika Binti Sayuni 2 kwa wingu la hasira yake! 1 Ameitupa chini fahari ya Israeli 2 kutoka mbinguni mpaka duniani, 1 hakukumbuka kiti chake cha kuwekea miguu 2 katika siku ya hasira yake. 1
2Bila huruma Bwana ameyameza 2 makao yote ya Yakobo; 1 katika ghadhabu yake amebomoa 2 ngome za Binti Yuda. 1 Ameuangusha ufalme wake na wakuu wake 2 chini kwa aibu. 1
3Katika hasira kali amevunja 2 kila pembe + 2:3 Pembe inawakilisha nguvu; pia 2:17. ya Israeli. 1 Ameuondoa mkono wake wa kuume 2 alipokaribia adui. 1 Amemteketeza Yakobo kama moto uwakao 2 ule uteketezao kila kitu kinachouzunguka. 1
4Ameupinda upinde wake kama adui, 2 mkono wake wa kuume uko tayari. 1 Kama vile adui amewachinja 2 wote waliokuwa wanapendeza jicho, 1 amemwaga ghadhabu yake kama moto 2 juu ya hema la Binti Sayuni. 1
5Bwana ni kama adui; 2 amemmeza Israeli. 1 Amemeza majumba yake yote ya kifalme 2 na kuangamiza ngome zake. 1 Ameongeza huzuni na maombolezo 2 kwa ajili ya Binti Yuda. 1
6Ameharibu maskani yake kama bustani, 2 ameharibu mahali pake pa mkutano. 1 Bwana amemfanya Sayuni kusahau 2 sikukuu zake zilizoamriwa na Sabato zake; 1 katika hasira yake kali amewadharau 2 mfalme na kuhani. 1
7Bwana amekataa madhabahu yake 2 na kuacha mahali patakatifu pake. 1 Amemkabidhi adui kuta 2 za majumba yake ya kifalme; 1 wamepiga kelele katika nyumba ya Bwana 2 kama katika siku ya sikukuu iliyoamriwa. 1
8Bwana alikusudia kuangusha 2 ukuta uliomzunguka Binti Sayuni. 1 Ameinyoosha kamba ya kupimia 2 na hakuuzuia mkono wake usiangamize. 1 Alifanya maboma na kuta ziomboleze, 2 vyote vikaharibika pamoja. 1
9Malango yake yamezama ardhini, 2 makomeo yake ameyavunja na kuyaharibu. 1 Mfalme wake na wakuu wake wamepelekwa uhamishoni 2 miongoni mwa mataifa, 2 sheria haipo tena, 1 na manabii wake hawapati tena 2 maono kutoka kwa Bwana. 1
10Wazee wa Binti Sayuni 2 wanaketi chini kimya, 1 wamenyunyiza mavumbi kwenye vichwa vyao 2 na kuvaa nguo za gunia. 1 Wanawali wa Yerusalemu 2 wamesujudu hadi ardhini. 1
11Macho yangu yamedhoofika kwa kulia, 2 nina maumivu makali ndani, 1 moyo wangu umemiminwa ardhini 2 kwa sababu watu wangu wameangamizwa, 1 kwa sababu watoto na wanyonyao wanazimia 2 kwenye barabara za mji. 1
12Wanawaambia mama zao, 2 “Wapi mkate na divai?” 1 wazimiapo kama watu waliojeruhiwa 2 katika barabara za mji, 1 maisha yao yadhoofikavyo 2 mikononi mwa mama zao. 1
13Ninaweza kusema nini kwa ajili yako? 2 Nikulinganishe na nini, 2 ee Binti Yerusalemu? 1 Nitakufananisha na nini, 2 ili nipate kukufariji, 2 ee Bikira Binti Sayuni? 1 Jeraha lako lina kina kama bahari. 2 Ni nani awezaye kukuponya? 1
14Maono ya manabii wako 2 yalikuwa ya uongo na yasiyofaa kitu, 1 hawakuifunua dhambi yako 2 ili kukuzuilia kwenda utumwani. 1 Maneno waliyokupa 2 yalikuwa ya uongo na ya kupotosha. 1
15Wote wapitiao njia yako 2 wanakupigia makofi, 1 wanakudhihaki na kutikisa vichwa vyao 2 kwa Binti Yerusalemu: 1 “Huu ndio ule mji ulioitwa 2 mkamilifu wa uzuri, 2 furaha ya dunia yote?” 1
16Adui zako wote wanapanua 2 vinywa vyao dhidi yako, 1 wanadhihaki na kusaga meno yao 2 na kusema, “Tumemmeza. 1 Hii ndiyo siku tuliyoingojea, 2 tumeishi na kuiona.” 1
17Bwana amefanya lile alilolipanga; 2 ametimiza neno lake 2 aliloliamuru siku za kale. 1 Amekuangusha bila huruma, 2 amewaacha adui wakusimange, 2 ametukuza pembe ya adui yako. 1
18Mioyo ya watu 2 inamlilia Bwana. 1 Ee ukuta wa Binti Sayuni, 2 machozi yako na yatiririke kama mto 2 usiku na mchana; 1 usijipe nafuu, 2 macho yako yasipumzike. 1
19Inuka, lia usiku, 2 zamu za usiku zianzapo; 1 mimina moyo wako kama maji 2 mbele za Bwana. 1 Mwinulie yeye mikono yako 2 kwa ajili ya maisha ya watoto wako, 1 ambao wanazimia kwa njaa 2 kwenye kila mwanzo wa barabara. 1
20“Tazama, Ee Bwana, ufikirie: 2 Ni nani ambaye umepata 2 kumtendea namna hii? 1 Je, wanawake wakule wazao wao, 2 watoto waliowalea? 1 Je, kuhani na nabii auawe 2 mahali patakatifu pa Bwana? 1
21“Vijana na wazee hujilaza pamoja 2 katika mavumbi ya barabarani, 1 wavulana wangu na wasichana 2 wameanguka kwa upanga. 1 Umewaua katika siku ya hasira yako, 2 umewachinja bila huruma. 1
22“Kama ulivyoita siku ya karamu, 2 ndivyo ulivyoagiza hofu kuu 2 dhidi yangu kila upande. 1 Katika siku ya hasira ya Bwana 2 hakuna yeyote aliyekwepa au kupona; 1 wale niliowatunza na kuwalea, 2 adui yangu amewaangamiza.”