Amos · Biblia (Kiswahili)

Amos 1

1Maneno ya Amosi, mmoja wa wachunga wanyama wa Tekoa: yale aliyoyaona kuhusu Israeli miaka miwili kabla ya tetemeko la ardhi, wakati Uzia alikuwa mfalme wa Yuda, na Yeroboamu mwana wa Yehoashi alikuwa mfalme wa Israeli.

2Alisema: 1 “ Bwana ananguruma toka Sayuni, 2 pia ananguruma kutoka Yerusalemu; 1 malisho ya wachunga wanyama yanakauka, 2 kilele cha Karmeli kinanyauka.” 1 Hukumu Juu Ya Majirani Wa Israeli

3Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Kwa dhambi tatu za Dameski, 2 hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. 1 Kwa sababu aliipura Gileadi 2 kwa vyombo vya chuma vyenye meno. 1

4Nitatuma moto juu ya nyumba ya Hazaeli 2 ambao utateketeza ngome za Ben-Hadadi. 1

5Nitalivunja lango la Dameski; 2 nitamwangamiza mfalme aliyeko katika Bonde la Aveni, + 1:5 Bonde la Aveni maana yake Bonde la Uovu. 1 na yeye ambaye anaishika fimbo ya utawala katika Beth-Edeni. 2 Watu wote wa Aramu watakwenda uhamishoni huko Kiri,” 4 asema Bwana.

6Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Kwa dhambi tatu za Gaza, 2 hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. 1 Kwa sababu walichukua mateka jumuiya nzima 2 na kuwauza kwa Edomu, 1

7nitatuma moto juu ya kuta za Gaza 2 ambao utateketeza ngome zake. 1

8Nitamwangamiza mfalme wa Ashdodi 2 na yeye aishikaye fimbo ya utawala katika Ashkeloni. 1 Nitaugeuza mkono wangu dhidi ya Ekroni, 2 hadi Mfilisti wa mwisho atakapokufa,” 4 asema Bwana Mwenyezi.

9Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Kwa dhambi tatu za Tiro, 2 hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. 1 Kwa sababu ameuza jumuiya nzima ya mateka kwa Edomu, 2 na kutokujali mapatano ya undugu, 1

10Nitatuma moto kwenye kuta za Tiro 2 ambao utateketeza ngome zake.”

11Hili ndilo Bwana asemalo: 1 “Kwa dhambi tatu za Edomu, 2 hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. 1 Kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga, 2 alikataa kuonyesha huruma yoyote, 1 kwa sababu hasira yake kali iliendelea kupanda wakati wote 2 na ghadhabu iliwaka bila kuzuiliwa. 1

12Nitatuma moto juu ya Temani 2 ambao utateketeza ngome za Bosra.”

13Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Kwa dhambi tatu za Amoni, 2 hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. 1 Kwa sababu aliwatumbua wanawake wajawazito wa Gileadi 2 ili kuongeza mipaka yake. 1

14Nitatuma moto kwenye kuta za Raba 2 ambao utateketeza ngome zake 1 katikati ya vilio vya vita katika siku ya mapigano, 2 katikati ya upepo mkali katika siku ya dhoruba. 1

15Mfalme wake atakwenda uhamishoni, 2 yeye pamoja na maafisa wake,” 4 asema Bwana.

← Joel 3Read In The App, Free →Amos 2 →

Study Amos 1

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789