Amos 5
1Sikia neno hili, ee nyumba ya Israeli, ombolezo hili ninalifanya kuwahusu ninyi: 1
2“Bikira Israeli ameanguka, 2 kamwe hatainuka tena, 1 ameachwa pweke katika nchi yake, 2 hakuna yeyote wa kumwinua.”
3Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: 1 “Wakati mmoja wa miji yako utakapopeleka watu elfu moja vitani kwa ajili ya Israeli, 2 mia moja tu watarudi; 1 wakati mji utakapopeleka mia moja, 2 kumi tu ndio watarudi hai.”
4Hili ndilo Bwana asemalo kwa nyumba ya Israeli: 1 “Nitafuteni mpate kuishi; 2
5msitafute Betheli, 1 msiende Gilgali, 2 msisafiri kwenda Beer-Sheba. 1 Kwa maana kwa hakika Gilgali itakwenda uhamishoni, 2 na Betheli itafanywa kuwa si kitu.” + 5:5 Yaani Aveni kwa Kiebrania, kumaanisha Beth-Aveni, jina lingine la Betheli kwa dhihaka. 1
6Mtafuteni Bwana mpate kuishi, 2 au atafagia nyumba ya Yosefu kama moto; 1 utawateketeza, nayo Betheli 2 haitakuwa na yeyote wa kuuzima. 1
7Ninyi ambao mnageuza haki kuwa uchungu 2 na kuiangusha haki chini 1
8(yeye ambaye alifanya Kilimia na Orioni, 2 ambaye hugeuza giza kuwa mapambazuko 2 na mchana kuwa usiku, 1 ambaye huyaita maji ya bahari 2 na kuyamwaga juu ya uso wa nchi: 2 Bwana ndilo jina lake; 1
9yeye hufanya maangamizo kwenye ngome 2 na kufanya mji uliozungushiwa ngome kuwa ukiwa), 1
10mnamchukia yule akemeaye mahakamani, 2 na kumdharau yule ambaye husema kweli. 1
11Mnamgandamiza maskini 2 na kumlazimisha awape nafaka. 1 Kwa hiyo, ingawa mmejenga majumba ya mawe ya fahari, 2 hamtaishi ndani yake; 1 ingawa mmepanda mashamba mazuri ya mizabibu, 2 hamtakunywa divai yake. 1
12Kwa kuwa ninajua hesabu ya makosa yenu 2 na ukubwa wa dhambi zenu. 1 Mmewaonea wenye haki na kupokea rushwa 2 na kuzuia haki ya maskini mahakamani. 1
13Kwa hiyo mtu mwenye busara hunyamaza kimya nyakati kama hizo, 2 kwa kuwa nyakati ni mbaya. 1
14Tafuteni mema, wala si mabaya, 2 ili mpate kuishi. 1 Ndipo Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote atakuwa pamoja nanyi, 2 kama msemavyo yupo nanyi. 1
15Yachukieni maovu, yapendeni mema; 2 dumisheni haki mahakamani. 1 Yamkini Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote 2 atawahurumia mabaki ya Yosefu.
16Kwa hiyo hili ndilo Bwana, Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, asemalo: 1 “Kutakuwepo maombolezo katika barabara zote 2 na vilio vya uchungu katika njia kuu zote. 1 Wakulima wataitwa kuja kulia, 2 na waombolezaji waje kuomboleza. 1
17Kutakuwepo kuomboleza katika mashamba yote ya mizabibu, 2 kwa kuwa nitapita katikati yenu,” 4 asema Bwana. 1 Siku Ya Bwana 1
18Ole wenu ninyi mnaoitamani 2 siku ya Bwana! 1 Kwa nini mnaitamani siku ya Bwana? 2 Siku hiyo itakuwa giza, si nuru. 1
19Itakuwa kama vile mtu aliyemkimbia simba 2 kumbe akakutana na dubu, 1 kama vile mtu aliyeingia nyumbani mwake 2 na kuupumzisha mkono wake kwenye ukuta, 2 kumbe akaumwa na nyoka. 1
20Je, siku ya Bwana haitakuwa giza, na si nuru: 2 giza nene, bila mwonzi wa mwanga? 1
21“Ninachukia, ninazidharau sikukuu zenu za dini; 2 siwezi kuvumilia makusanyiko yenu. 1
22Hata ingawa mnaniletea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka za nafaka, 2 sitazikubali. 1 Ingawa mnaniletea sadaka nzuri za amani, 2 sitazitambua. 1
23Niondoleeni kelele za nyimbo zenu! 2 Sitasikiliza sauti za vinubi vyenu. 1
24Lakini acheni haki itiririke kama mto, 2 na uadilifu uwe kama kijito kisichokauka! 1
25“Je, mliniletea dhabihu na sadaka 2 kwa miaka arobaini kule jangwani, 2 ee nyumba ya Israeli? 1
26Mmeyainua madhabahu ya mfalme wenu, 2 Sikuthi mungu wenu mtawala, 1 na Kiuni mungu wenu wa nyota, 2 ambao mliwatengeneza wenyewe. 1
27Kwa sababu hiyo nitawapeleka uhamishoni mbali kupita Dameski,” 2 asema Bwana, ambaye jina lake ni Mungu Mwenye Nguvu Zote.