Amos 3
1Sikilizeni neno hili alilosema Bwana dhidi yenu, enyi watu wa Israeli, dhidi ya jamaa nzima niliowapandisha toka Misri: 1
2“Ni ninyi tu niliowachagua 2 kati ya jamaa zote za dunia; 1 kwa hiyo nitawaadhibu 2 kwa ajili ya dhambi zenu zote.” 1
3Je, watu wawili hutembea pamoja 2 wasipokubaliana kufanya hivyo? 1
4Je, simba hunguruma katika kichaka 2 wakati hana mawindo? 1 Aweza kuvuma katika pango 2 wakati ambao hajakamata chochote? 1
5Je, ndege aweza kuanguka kwenye mtego ulio ardhini 2 ambapo hajategewa chambo? 1 Je, mtego unaweza kufyatuka toka ardhini 2 wakati ambapo hakuna chochote cha kunasa? 1
6Je, tarumbeta inapopigwa mjini kujulisha hatari, 2 watu hawatetemeki? 1 Mji upatwapo na maafa, 2 je, si Bwana amesababisha? 1
7Hakika Bwana Mwenyezi hatafanya neno lolote 2 bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake. 1
8Simba amenguruma: 2 je, ni nani ambaye hataogopa? 1 Bwana Mwenyezi ametamka: 2 je, ni nani awezaye kukosa kutoa unabii? 1
9Tangazeni katika ngome za Ashdodi 2 na katika ngome za Misri: 1 “Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria; 2 angalieni wingi wa wasiwasi ulio ndani yake, 2 na uonevu ulio miongoni mwa watu wake.” 1
10Bwana asema: “Hawajui kutenda lililo jema, 2 wale ambao hujilundikia nyara 2 na vitu vilivyotekwa katika ngome zao.”
11Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi: 1 “Adui ataizingira nchi; 2 ataangusha chini ngome zenu 2 na kuteka nyara maboma yenu.”
12Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Kama vile mchungaji aokoavyo kinywani mwa simba 2 vipande viwili tu vya mfupa wa mguu 2 au kipande cha sikio, 1 hivyo ndivyo Waisraeli watakavyookolewa, 2 wale wakaao Samaria 2 kwenye kingo za vitanda vyao, 1 na katika Dameski 2 kwenye viti vyao vya fahari.”
13“Sikia hili na ushuhudie dhidi ya nyumba ya Yakobo,” asema Bwana, Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote. 1
14“Siku nitakapomwadhibu Israeli kwa sababu ya dhambi zake, 2 nitaharibu madhabahu za Betheli; 1 pembe za madhabahu zitakatiliwa mbali 2 na kuanguka chini. 1
15Nitabomoa nyumba ya wakati wa masika, 2 pamoja na nyumba ya wakati wa kiangazi; 1 nyumba zilizonakshiwa kwa pembe za ndovu 2 na majumba makubwa ya fahari yatabomolewa,” 4 asema Bwana.