Amos 2
1Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Kwa dhambi tatu za Moabu, 2 hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. 1 Kwa sababu alichoma mifupa ya mfalme wa Edomu, 2 ikawa kama chokaa. 1
2Nitatuma moto juu ya Moabu 2 ambao utateketeza ngome za Keriothi. 1 Moabu ataanguka kwa ghasia kubwa 2 katikati ya vilio vya vita na mlio wa tarumbeta. 1
3Nitamwangamiza mtawala wake 2 na kuwaua maafisa wake wote pamoja naye,” 4 asema Bwana.
4Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Kwa dhambi tatu za Yuda, 2 hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. 1 Kwa sababu wameikataa sheria ya Bwana 2 na hawakuzishika amri zake, 1 kwa sababu wamepotoshwa na miungu ya uongo, 2 miungu ambayo babu zao waliifuata. 1
5Nitatuma moto juu ya Yuda 2 ambao utateketeza ngome za Yerusalemu.” 1 Hukumu Juu Ya Israeli
6Hili ndilo asemalo Bwana: 1 “Kwa dhambi tatu za Israeli, 2 hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. 1 Wanawauza wenye haki kwa fedha, 2 na maskini kwa jozi ya viatu. 1
7Wanakanyaga juu ya vichwa vya maskini, 2 kama vile juu ya mavumbi ya nchi, 2 na kukataa haki kwa walioonewa. 1 Baba na mwanawe hushiriki msichana mmoja, 2 kwa hivyo hulinajisi Jina langu takatifu. 1
8Watu hulala kando ya kila madhabahu 2 juu ya nguo zilizowekwa rehani. 1 Katika nyumba ya mungu wao hunywa mvinyo 2 ulionunuliwa kwa fedha walizotozwa watu. 1
9“Nilimwangamiza Mwamori mbele yao, 2 ingawa alikuwa mrefu kama mierezi, 2 na mwenye nguvu kama mialoni. 1 Niliyaangamiza matunda yake juu 2 na mizizi yake chini. 1
10“Niliwapandisha toka Misri, 2 na nikawaongoza miaka arobaini jangwani 2 niwape nchi ya Waamori. 1
11Pia niliinua manabii kutoka miongoni mwa wana wenu 2 na Wanadhiri kutoka miongoni mwa vijana wenu. 1 Je, hii si kweli, enyi watu wa Israeli?” 4 asema Bwana. 1
12“Lakini mliwafanya Wanadhiri kunywa mvinyo 2 na kuwaamuru manabii wasitoe unabii. 1
13“Sasa basi, nitawaponda 2 kama gari lipondavyo wakati limejazwa nafaka. 1
14Mkimbiaji hodari hatanusurika, 2 wenye nguvu wataishiwa nguvu zao, 2 na shujaa hataweza kuokoa maisha yake. 1
15Mpiga upinde atakimbia, 2 askari wapiga mbio hawataweza kutoroka, 2 na mpanda farasi hataokoa maisha yake. 1
16Hata askari walio mashujaa sana 2 siku hiyo watakimbia uchi,” 4 asema Bwana.