Amos 8
1Hili ndilo alilonionyesha Bwana Mwenyezi katika maono: kikapu cha matunda yaliyoiva.
2Akaniuliza, “Amosi, unaona nini?” Nikajibu, “Kikapu chenye matunda yaliyoiva.” Ndipo Bwana akaniambia, “Wakati umewadia kwa watu wangu Israeli; sitawahurumia zaidi.”
3Bwana Mwenyezi asema, “Katika siku ile, nyimbo katika Hekalu zitageuka kuwa maombolezo. Miili mingi, mingi sana: itatupwa kila mahali! Kimya!” 1
4Lisikieni hili, ninyi ambao mnawagandamiza wahitaji, 2 na kuwaonea maskini wa nchi,
5mkisema, 1 “Ni lini Mwezi Mwandamo utakapopita 2 ili tupate kuuza nafaka, 1 na Sabato itakwisha lini 2 ili tuweze kuuza ngano?” 1 Mkipunguza vipimo, 2 na kuongeza bei, 2 na kudanganya kwa mizani zisizo sawa, 1
6mkiwanunua maskini kwa fedha, 2 na wahitaji kwa jozi ya viatu, 1 na mkiuza hata takataka za ngano 2 pamoja na ngano.
7Bwana ameapa kwake mwenyewe, aliye Kiburi cha Yakobo: “Kamwe sitasahau chochote ambacho wamefanya. 1
8“Je, nchi haitatetemeka kwa ajili ya hili, 2 nao wote waishio ndani mwake hawataomboleza? 1 Nchi yote itainuka kama Naili; 2 itapanda na kushuka kama mto wa Misri.
9“Katika siku ile,” asema Bwana Mwenyezi, 1 “Nitalifanya jua litue alasiri na kuifanya dunia 2 iwe giza wakati wa mchana mwangavu. 1
10Nitageuza sikukuu zenu za kidini kuwa maombolezo, 2 na kuimba kwenu kote kuwe kilio. 1 Nitawafanya ninyi nyote mvae nguo ya gunia 2 na kunyoa nywele zenu. 1 Nitaufanya wakati ule uwe kama wa kuombolezea mwana wa pekee, 2 na mwisho wake kama siku ya uchungu. 1
11“Siku zinakuja,” asema Bwana Mwenyezi, 2 “wakati nitakapotuma njaa katika nchi yote: 1 si njaa ya chakula wala kiu ya maji, 2 lakini njaa ya kusikia maneno ya Bwana. 1
12Wanaume watayumbayumba kutoka bahari hadi bahari 2 na kutangatanga kutoka kaskazini mpaka mashariki, 1 wakitafuta neno la Bwana, 2 lakini hawatalipata.
13“Katika siku ile 1 “wasichana wazuri na vijana wanaume wenye nguvu 2 watazimia kwa sababu ya kiu. 1
14Wale waapao kwa aibu ya Samaria, 2 au kusema, ‘Hakika kama miungu yenu iishivyo, ee Dani,’ 1 au ‘Hakika kama mungu wa Beer-Sheba aishivyo’: 2 wataanguka, wala hawatasimama tena.”