Amos · Biblia (Kiswahili)

Amos 4

1Sikilizeni neno hili, ninyi ngʼombe wa Bashani 2 mlioko juu ya Mlima Samaria, 1 ninyi wanawake mnaowaonea maskini, 2 na kuwagandamiza wahitaji, 1 na kuwaambia wanaume wenu, 2 “Tuleteeni vinywaji!” 1

2Bwana Mwenyezi ameapa kwa utakatifu wake: 2 “Hakika wakati utakuja 1 mtakapochukuliwa na kulabu, 2 na wanaosalia kwa ndoana za samaki. 1

3Nanyi mtakwenda moja kwa moja 2 kupitia mahali palipobomolewa kwenye ukuta, 2 nanyi mtatupwa nje kuelekea Harmoni,” 4 asema Bwana. 1

4“Nendeni Betheli mkatende dhambi; 2 nendeni Gilgali mkazidi kutenda dhambi. 1 Leteni dhabihu zenu kila asubuhi, 2 zaka zenu kila mwaka wa tatu. 1

5Mchome mkate uliotiwa chachu kama sadaka ya shukrani, 2 jisifuni kuhusu sadaka zenu za hiari: 1 jigambeni kwa ajili ya sadaka hizo, enyi Waisraeli, 2 kwa kuwa hili ndilo mnalopenda kulitenda,” 4 asema Bwana Mwenyezi. 1

6“Niliwapa njaa kwenye kila mji, 2 na ukosefu wa chakula katika kila mji, 2 hata hivyo bado hamjanirudia mimi,” 4 asema Bwana. 1

7“Pia niliwazuilia ninyi mvua miezi mitatu 2 kabla ya kufikia mavuno. 1 Nilinyesha mvua kwenye mji mmoja, 2 lakini niliizuia mvua isinyeshe mji mwingine. 1 Shamba moja lilipata mvua, 2 na lingine halikupata, nalo likakauka. 1

8Watu walitangatanga mji hata mji kutafuta maji, 2 lakini hawakupata ya kuwatosha kunywa, 2 hata hivyo hamjanirudia mimi,” 4 asema Bwana. 1

9“Mara nyingi nilizipiga bustani zenu na mashamba ya mizabibu, 2 niliyapiga kwa kutu na ukungu. 1 Nzige walitafuna tini zenu na miti ya mizeituni, 2 hata hivyo hamjanirudia mimi,” 4 asema Bwana. 1

10“Niliwapelekea tauni miongoni mwenu 2 kama nilivyofanya kule Misri. 1 Niliwaua vijana wenu wa kiume kwa upanga, 2 niliwachukua farasi wenu. 1 Nilijaza pua zenu kwa uvundo kutoka kwenye kambi zenu, 2 hata hivyo hamjanirudia mimi,” 4 asema Bwana. 1

11“Niliwaangamiza baadhi yenu kama 2 nilivyoangamiza Sodoma na Gomora. 1 Mlikuwa kama kijiti kiwakacho kilichonyakuliwa motoni, 2 hata hivyo hamjanirudia,” 4 asema Bwana. 1

12“Kwa hiyo hili ndilo nitakalowafanyia, Israeli, 2 na kwa sababu nitawafanyia hili, 2 jiandaeni kukutana na Mungu wenu, ee Israeli.” 1

13Yeye ambaye hufanya milima, anaumba upepo, 2 na kufunua mawazo yake kwa mwanadamu, 1 yeye ageuzaye asubuhi kuwa giza, 2 na kukanyaga mahali pa juu pa nchi: 2 Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.

← Amos 3Read In The App, Free →Amos 5 →

Study Amos 4

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789