Micah · Biblia (Kiswahili)

Micah 1

1Neno la Bwana lilimjia Mika, Mmoreshethi, wakati wa utawala wa Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda; ufunuo aliouona kuhusu Samaria na Yerusalemu. 1

2Sikieni, enyi mataifa, enyi nyote, 2 sikilizeni, ee dunia na wote mliomo ndani yake, 1 ili Bwana Mwenyezi ashuhudie dhidi yenu, 2 Bwana kutoka Hekalu lake takatifu. 1 Hukumu Dhidi Ya Samaria Na Yerusalemu 1

3Tazama! Bwana anakuja kutoka mahali pake; 2 anashuka na kukanyaga 2 mahali palipoinuka juu pa dunia. 1

4Milima inayeyuka chini yake 2 na mabonde yanagawanyika 1 kama nta mbele ya moto, 2 kama maji yatiririkayo kasi 2 kwenye mteremko. 1

5Yote haya ni kwa sababu ya kosa la Yakobo, 2 ni kwa sababu ya dhambi za nyumba ya Israeli. 1 Kosa la Yakobo ni lipi? 2 Je, sio Samaria? 1 Je, mahali pa juu pa Yuda pa kuabudia miungu ni nini? 2 Je, sio Yerusalemu? 1

6“Kwa hiyo nitaufanya Samaria kuwa lundo la kokoto, 2 mahali pa kuotesha mizabibu. 1 Nitayamwaga mawe yake katika bonde 2 na kuacha wazi misingi yake. 1

7Sanamu zake zote 2 zitavunjwa vipande vipande; 1 zawadi zake zote za Hekalu 2 zitachomwa kwa moto; 2 nitaharibu vinyago vyake vyote. 1 Kwa kuwa alikusanya zawadi zake 2 kutokana na ujira wa kahaba, 1 nazo zitatumika tena 2 kulipa mishahara ya kahaba.” 1 Kulia Na Kuomboleza 1

8Kwa ajili ya hili nitalia na kuomboleza; 2 nitatembea bila viatu na tena uchi. 1 Nitabweka kama mbweha 2 na kuomboleza kama bundi. 1

9Kwa sababu jeraha lake halitibiki; 2 limekuja Yuda. 1 Limefika hasa kwenye lango la watu wangu, 2 hata Yerusalemu kwenyewe. 1

10Usiliseme hili huko Gathi; 2 usilie hata kidogo. 1 Huko Beth-le-Afra 2 gaagaa mavumbini. 1

11Piteni mkiwa uchi na wenye aibu, 2 ninyi mkaao Shafiri. 1 Wale waishio Saanani 2 hawatatoka nje. 1 Beth-Eseli iko katika maombolezo; 2 kinga yake imeondolewa kwako. 1

12Wale waishio Marothi wanagaagaa kwa maumivu 2 wakingoja msaada, 1 kwa sababu maangamizi yamekuja 2 kutoka kwa Bwana, 2 hata katika lango la Yerusalemu. 1

13Enyi mkaao Lakishi, 2 fungeni farasi kwenye magari ya vita. 1 Mlikuwa chanzo cha dhambi 2 kwa Binti Sayuni, 1 kwa kuwa makosa ya Israeli 2 yalikutwa kwako. 1

14Kwa hiyo utaipa Moresheth-Gathi 2 zawadi za kuagana. 1 Mji wa Akzibu utaonyesha wazi udanganyifu 2 kwa wafalme wa Israeli. 1

15Nitawaleteeni atakayewashinda 2 ninyi mnaoishi Maresha. 1 Yeye aliye utukufu wa Israeli 2 atakuja Adulamu. 1

16Nyoeni nywele zenu katika kuomboleza 2 kwa ajili ya watoto wenu mnaowafurahia; 1 jifanyieni upara kama tai, 2 kwa kuwa watawaacha 2 na kwenda uhamishoni.

← Jonah 4Read In The App, Free →Micah 2 →

Study Micah 1

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

1234567